Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

Nigeria inabebwa na wingi wa watu wa ndani na wa nje, lakini utaifa wake upo hoi, sababu ni hiyo ya kujitambulisha kimajimbo.

Nchi nyingi zenye sera hii zinakuwa na vuguvugu jingi sana la ubaguzi wa ndani haswa masuala ya ukabila.
US, UK, German, Kenya, South Africa, Nigeria zina majimbo tunazizidi nini.
 
Suluhisho la hasira zako haliwezi kuwa sera ya majimbo ya kukopi na kupesti kutoka nchi nyingine.

Nchi huwa haifanyiwi majaribio kwa sera zisizokuwa na msingi wa asili, watu wataumia.
 
Uwezo wako ni mdogo sana kuelewa. Hilo suala la gharama limeelezwa vizuri sana humu jf na sina sababu ya kulirudia. Ni kupoteza muda. Soma Uzi za wenzako kabla ya kukurupuka kuandika yako.
 
Kweli wewe ni kilambimkwidu.

Alokuambia singida Wanategemea alizeti tu ni nani?
Au ndo ushabiki mkuu
 
Hujajibu swali langu!!

Nimesema kama sera ya majimbo ni ya kichoyo na kibaguzi Sasa kwa nini na Sera yetu ya sasa ya mikoa Magufuli amesema mchana kweupe hawezi peleka maendeleo kwenye majimbo ya wapinzani?

Alisema jimboni kwa Bwege kabla hata ya kampeni na amesema maeneo mengi akiwa kwenye kampeni?

Huu ubaguzi na uchoyo nayo ni sera ya majimbo?
 
Suluhisho la hasira zako haliwezi kuwa sera ya majimbo ya kukopi na kupesti kutoka nchi nyingine.

Nchi huwa haifanyiwi majaribio kwa sera zisizokuwa na msingi wa asili, watu wataumia.
Unanilazimisha niendelee kuamini uwezo wako wa kufikiri ulivyo wa chini siku zote. Nimekupa mfano mmoja tu wa ubovu wa madc wa sasa na jinsi wanacyoumiza wananchi. Na nikuongeze la pili, Tanzania hakuna mkoa unaokaliwa na Kabila moja pekee, Tabora kuna Wanyamwezi, Waha, Wanyakyusa, Wangoni, Wakara, Wahaya nk! Ukabila utatoka wapi kwenye mkoa kama huo?
 
Nimekujibu kwa kukwambia kuwa upinzani umejikita kupinga kila kitu hata mambo ambayo ni progressive.

Upinzani unafanya siasa hata katika masuala yasiyohitaji siasa.

Huko kwa bwege kiusalama kuna masuala mabaya sana yalifanyika na yakataka kuivunja kabisa Tanzania, siwezi kuyaandika humu jukwaani.
 
Mwambie Gwajima atakuja kuwatembelea ila tambua matatizo ya bunju a na b yapo na Marais ni wa ccm Toka Uhuru unamlahum mdehe unachekesha kweli.
 
Nigeria inabebwa na wingi wa watu wa ndani na wa nje, lakini utaifa wake upo hoi, sababu ni hiyo ya kujitambulisha kimajimbo.

Nchi nyingi zenye sera hii zinakuwa na vuguvugu jingi sana la ubaguzi wa ndani haswa masuala ya ukabila.
Unapo sema utaifa wa nigeria upo hoi unamaanisha nini ? Nimeishi nigeria 2002 hadi 2011 sijaona hicho unacho kisema wewe kabisa au ni stori za vijiweni?
 
Hapana, hujaielewa. Hata mimi bado naitafakari kama inafaa, lakini nimejibidisha kuielewa.
Maana yake halisi ni kuwa watu wenyewe kwenye maeneo yao, yawe mikoa au wilaya, ndio wawe wanachagua au kuwateua viongozi wao, kama wakuu wa mikoa, wilaya na halmashauri.

Pia maeneo hayo, pamoja na Bunge, viongezewe madaraka ya kuamua badala ya Rais pekee.
 
2015 upinzani ndyo ulikuja na hoja ya elimu bure. Ccm walianza na kupinga sana uwezekano wa elimu bure ila mwisho ww siku wakaona isiwe shida na wao wakadandia hoja et elimu bure had 4m 4.

Sasa kabla ya uchaguzi kuisha utaona ccm itakavyodandia hii hoja.
 
Jibu swali tunazizidi nini??? Hivi huko CCM nako wanasema wana mjengaji hoja kwa ulivyo kilaza hivi???πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Suala ni Tanzania yetu na kesho yetu itakuwa vipi tukiruhusu sera ya majimbo.

Punguza unyonge wa kiakili ridhika na cha kwako ulichopewa na Mungu.
 
Unaizungumziaje USA?

Sent from my OPPO R11s using JamiiForums mobile app
 
Unajua gharama za kuendesha Wilaya?

- Mkuu wa wilaya
-Mbunge tena wilaya zingine wabunge ni wawili
- Mkurugenzi
-DAS
-Mwenyekiti wa Halimashauri

Hawa wote wanasimamia wilaya 1, mfumo wa kijima sana huu
Nilitaka nimwambie hivi thanks.
Huyu Yehodaya ukweli anaujua lkn alishaamua kujitoa ufahamu.
 
Mbona unafoka sana?
Kumbuka kuwa magavana wa majimbo ni viongozi wa kuchaguliwa na wananchi wa eneo husika.Are we togather?
 
Unapo sema utaifa wa nigeria upo hoi unamaanisha nini ? Nimeishi nigeria 2002 hadi 2011 sijaona hicho unacho kisema wewe kabisa au ni stori za vijiweni?
Nigeria kuna ukabila uliojengwa kwa msingi wa majimbo yao. Wanajitambulisha kwa ukabila wao.

Sera ya majimbo itaigawa nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…