Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi


Maisha hayaishii kwenye utawala pekee, tanashuka kwenye mahusiano ya wananchi.

Yanashuka kwenye matumizi ya rasilimali za nchi.

Ubaya ya mfumo wa majimbo ni ule uchoyo kwamba rasilimali hii isiguswe na majimbo mengine.

Kinachopatikana Mtwara kinatumika kwa faida ya nchi nzima.

Kinachopatikana Kagera kinatumiwa kwa faida ya nchi nzima na hiyo ndio maana ya umoja.
 
Hiyo inaeleweka dunia nzima kuna pato linaenda serikali kuu na kutawanywa nchi nzima na asilimia fulani inabaki jimboni. Na kuna vyanzo vya mapato ni vya jimbo na vingine serikali kuu kama ilivyo katika muungano, kuna mambo ya muungano na siyo ya muungano, ni swala la sheria kuamua. Rais tutamjua kwa jinsi alivyoongoza jimbo lake. Mfumo mzuri sana huu ndiyo uhuru wa kisiasa siyo sasa tunadanganywa tu na kuchagua wabunge mere representatives not leaders
 
Kwani mfumo tulionao tumeiga wapi chief? Serikali kuu imehodhi mamlaka yote,mapato yote lazima yaende serikali kuu,walioko juu hawajui vipaumbele vya busokelo huko. Devolution ndiyo the way forward tukiachana na milengo yetu ya kisiasa.
Busokelo wanae mbunge watakayempata kwa kumpigia kura, kazi yake ni kuwa karibu na wananchi.

Watachagua diwani pia, kazi yake ni kutetea maslahi ya wapiga kura.
 
Mkuu, hapa itakuwa ni uelewa wako mdogo kwenye hii issue. Unapotoa mfano wa USA ... yale siyo majimbo ni states. Yaani nchi zimeungana kuunda taifa la Marekani kama sisi tulivyoungana na Zanzibar.
 
Hata utawala wa majimbo unazo changamoto zake nyingi tu, nenda kazitembelee nchi zenye majimbo utazifahamu kwa ukaribu.
 
Mkuu, hapa itakuwa ni uelewa wako mdogo kwenye hii issue. Unapotoa mfano wa USA ... yale siyo majimbo ni states. Yaani nchi zimeungana kuunda taifa la Marekani kama sisi tulivyoungana na Zanzibar.

Mimi nitakuwa wa kwanza kuunga mkono jimbo la Tanzania iwapo wataibuka kina Kwame Nkrumah wa miaka ya sasa watakaoanzisha wazo la United States of Africa.
 
Hii hoja ya majimbo imewapagawisha sana aiseee

Huelewi hela zinatoka kwenye mapato yote ya jimbo zima yanabaki hapo hapo percent kidogo ndio inaenda federal government..

Nyie mnafanya kinyume,mapato yote yanaenda federal government kwanza halafu kijipercent kidogo ndio kinarudi kwenye mkoa...yaani mavi matupu..

Lissu kawamaliza na hii hoja mmechanganyikiwa sana..na anajua kuieleza vizuri na cha ajabu wananchi wametokea kuielewa vizuri sana mmebaki kupaniki

Lissu ni genius,hamumuwezi mamaeee zenu vilaza
 
Mimi nitakuwa wa kwanza kuunga mkono jimbo la Tanzania iwapo wataibuka kina Kwame Nkrumah wa miaka ya sasa watakaoanzisha wazo la United States of Africa.
Sababu zipi zinakufanya uunge mkono UNiated Staes of Africa. Hapa tu tayari tuna changamoto ya EAC ambayo kila siku tunalalamika kuwa Kenya wanataka ardhi na kazi zetu.
 
Sababu zipi zinakufanya uunge mkono UNiated Staes of Africa. Hapa tu tayari tuna changamoto ya EAC ambayo kila siku tunalalamika kuwa Kenya wanataka ardhi na kazi zetu.
Sera ya majimbo kwa bara zima ina mantiki na faida kwa waafrika kuliko hii ya ndani ya nchi moja moja.
 
Wakati kodi anachukua!!
 
tuanzie hapa ..
hela za kujengea uwanja wa ndege CHATO zimetoka wapi? unazani huu mradi hatujui kuwa MEKO na mme mwenzie wachota hela kushirikiana na MPWA wao kupitia mradi huu
hela za STIGILAZi JOJI🙄😛 hela za SGR miradi iliyododa hela zimetoka wapiii?
 

Bila ya matusi kichwa chako ni kama hakiwezi kufanya kazi.

Sera ya majimbo msingi wake ni ubinafsi na uchoyo haina upendo wa kitaifa ndani yake.

Wale wenye rasilimali chache wafe na umaskini wao na wale wenye utajiri waishi vizuri kivyao!!.

Nchi itasambaratika mapema sana kwani serikali kuu haitaweza kuyashinda malalamiko ya majimbo yatakayoachwa nyuma.
 
kwani hela za kuendesha mikoa na wilaya zinatoka wapi?
 
Kwani TSH ngapi Mkuu?
 

Serikali kuu ndio inayoleta ubinafsi, ukabila, udini na roho ya uchoyo.

Msikilize mgombea wako anavyowabagua wale wanaochagua upinzani. Mgombea wako ni sawa na nyoka mwenye ndimi mbili.

Zipo kanda zilizobaguliwa tokea nchi hii ipate Uhuru, ukienda kuwauliza suluhisha la kubaguliwa kwao watakwambia bora tujitenge.

Chadema kwa kuliona hilo inataka kwanza kuwapa Uhuru zaidi wa kujiamulia mambo yao, Uhuru zaidi kwenye uchumi wao na utamaduni wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…