Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

Zipo nchi nyingi tu maskini zenye sera ya majimbo.
Kwani sera ya majimbo ndio utajiri?Nchi kuendelea Kuna factor nyingi kuwa tu na mfumo mzuri wa utawala haitoshi lakini kwa mazingira ya Tzn ,tukiweka mfumo huu nchi itapaa Sana kiuchumi.Leo hii Zanzibar iko hoi kiuchumi kuliko awali kwa sababu iko treated Kama mkoa
 
Mie naona wewe ndiye hujaelewa mantiki ya kile kinachoongelewa na Lissu! Hebu jiulize kidogo hivi mwaka 2015 ccm ilipokuwa inaahidi kutoa elimu bure, walikuwa wanabainisha fedha zitatoka wapi? Zipo mpaka pesa za kuendeshea kijiji na kata zikosekane vipi pesa za kuendeshea jimbo? Pia tunapojadili jambo hili tuelewe kwamba Lissu hamaanishi kwamba atajengelea ukuta kuziba kila jimbo kama ule mgodi wa Mererani, hapana ! Na wala hamaanishi kuwa kuyagawa majimbo manake hakuna kupeleka au kupokea fedha toka mfuko mkuu, hapana bali kuna baadhi ya vitega uchumi vitawekewa muongozo ili vinufaishe watanzania wote! Tuache upotoshaji ilimradi tu kutafta hoja ya kupinga mawazo mapya!
 
Hata utawala wa majimbo unazo changamoto zake nyingi tu, nenda kazitembelee nchi zenye majimbo utazifahamu kwa ukaribu.
Hakuna 100% solution of anything,kuna trade-offs..

Utawala wa mikoa ni most pathetic system ever happen..

Majimbo na mikoa,majimbo system ni afadhali kuliko huo uchafu wa kikoloni..

Pick your poison!
 
Lissu hajasema kuwa mkoa kama Singida ndio uwe jimbo. Wala hajasema kuwa kanda kama ya Kati ndiyo iwe jimbo. Kwa maelezo yake (msikilize vizuri kwenye video za Kagera), mikoa, wilaya na halmashauri zaweza kubaki zilivyo. Muhimu ni mambo matatu. 1. Mikoa, wilaya na halmashauri zipate madaraka zaidi ya maamuzi ya kiutawala na ya maendeleo kutoka hodhi ya Rais, ambaye anapoamua peke yake anaweza kuwa mbaguzi. 2. Watoa maamuzi muhimu kama Mkuu wa Mkoa, Wilaya na DED wapigiwe kura na wananchi ili wawajibike kwao. 3. Wabunge warudishiwe madaraka yao ya kikatiba ya kufanya maamuzi ya matumizi ya fedha na kupanga maendeleo ya nchi nzima, siyo ku rubber-stamp kila matakwa ya Rais. Ukiielewa hii dhana ya majimbo ya Lissu, hutakuwa na wasiwasi wa gharama tena kwa kuwa haziongezwi na mabadiliko haya ya uwajibikaji kwa wananchi.
 
Wabunge watabaki kuwa wawakilishi wa mhimili wa bunge kubwa katika serikali kuu,madiwani watakuwa wawakilishi katika mabunge ya majimbo,wakuu wa majimbo na watendaji wake watakuwa wawakilishi wa dola waliochaguliwa na wananchi katika majimbo yao.
Wabunge na madiwani wanachaguliwa na wananchi kumbuka kuhusu hilo jambo.

Cha muhimu ni hao wanaochaguliwa kuwa karibu na hao wanaowapigia kura.
 
Acha uongo,Vurugu za kikanda na za kikabila zilikuwepo kabla ya mfumo wa Kaunti,mfumo wa kaunti umemaliza tatizo hilo
 
Umeweka kwa mfano rahisi sana hata Meko ataelewa
 
mumeshabadilika baada ya kuwabana na hoja Za nguvu humu mwambieni afute aliyotamka Kwenye kampeni yahusuyo matumizi ya mapato

Sera lenu hata nyie wenyewe hamulielewi mnajikanyaga Kanyaga tu
 
Hakuna jimbo linalojitosheleza kwa kila kitu,majimbo lazima yatategemeana na yatashirikiana vizuri,yenye madini mengi yatahitaji chakula,barabara,na bandari kusafirisha madini yake n.k n.k
 
eti nchi itasambaratika ndio yule kichaa wenu kawaambia halafu mlivyo hamnazo you run with that nonsense!

Kama ni hivyo basi USA,South Africa,Kenya,Canada,India...na even your beloved stupid totalitarian China ungekuta washa sambaratika,lakini wapo na wanazidi prosper..

Hamna hoja kwenye hili,Lissu katoa msumari na wananchi seem to accept hapo ndio matako yanawauma sana..

Eti tutasambaratika,jibu la hovyo sana...halafu wananchi hawajawaelewa na majibu yenu kabisa mnabaki kuchanganyikiwa even more

Natukana yes,kashitaki kwa mawe!
 
Hakutakuwa tena na mambo nitampa kazi nyingine.
 
Wewe na mwenyekiti wako ni vichwa vya panzi hamna akili! Ukweli usemwe, CCM ina uhaba mkubwa sana wa vijana wenye akili!!
 
Kwamba tunaanzisha majimbo kwaajili ya mtu mmoja amesema hatapeleka maendelea sehemu Fulani?

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Ya
Yani ni ajabu wananchi wamekubali lakini ni viongozi pekee wa ccm ndiyo hawataki, tule tuvyeo twakupeana tunaenda kuisha
 
Ya

Yani ni ajabu wananchi wamekubali lakini ni viongozi pekee wa ccm ndiyo hawataki, tule tuvyeo twakupeana tunaenda kuisha
Wananchi walikubali wapi hiyo Kura walipiga wapi?
 
Hata mjifariji vipi ndio maana tuko kwenye uchaguzi watu ndio wataamua na sio wewe na wenzako mnaohofia njaa kwenye matumbo yenu.
Waende wakajiajiri maana hakutakuwa na vyeo vya kupeana bali itakuwa mwenye uwezo ndiyo anakuwa kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…