SERIKALI YA MAJIMBO
Wakati naandaa somo kuhusu umuhimu wa serikali za majimbo kiuchumi; tuanze kutafakari jambo hili;
Nchi ya Rwanda ina ardhi yenye ukubwa karibu sawa na mkoa wa Tanga. Rwanda ina kilometa za mraba 26,338 wakati Tanga ina 26,677 (Tanga ni kubwa kidogo)
Rwanda ina idadi ya watu karibu milioni 13 wakati Tanga ina idadi ya watu milioni 2.
Tanga ina fursa zaidi za kiuchumi; kuna fursa ya kuingiza fedha za kigeni kama misitu mikubwa, na hifadhi za wanyama (Saadan, Mkomanzi) sambamba na vivutio vingi vya utalii kuliko Rwanda. Kuna bahari, kuna madini, kuna ardhi kubwa kwa ajili ya kilimo.
Lakini kwenye maeneo ya Uchumi, Elimu, Miundombinu, Michezo, Kilimo, Biashara... Utaona Tanga ni kama kitenisi kwenye uwanja wa Rwanda.
Nini sababu kubwa ya tofauti hizi?
Je! Vipi kama Rwanda ingekuwa ni mkoa mmojawapo wa Tanzania, na mfumo wa utawala ukawa kama ilivyo sasa kwa mikoa mingine ya Tanzania? Rwanda ingekuwa kama ilivyo Sasa?
Kumbuka Tanga ambayo ni kubwa kuliko Rwanda bado kuna mikoa 13 ya Tanzania ambayo ni mikubwa zaidi.
Tutafakari kwanza maswali haya.
R = Rwanda
T = Tanga
Dr. Christopher Cyrilo