Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

Hakuna 100% solution of anything,kuna trade-offs..

Utawala wa mikoa ni most pathetic system ever happen..

Majimbo na mikoa,majimbo system ni afadhali kuliko huo uchafu wa kikoloni..

Pick your poison!
Halafu awamu hii au tuseme kuanzia awamu iliyopita value ya Ukuu wa Mkoa au Wilaya imeshushwa kwa kiasi kikubwa.

Hivi Imagine unaletewa Gambo, Makonda, sijui Mnyeti kuwa Wakuu wa mikoa. Actually, hiyo ni dharau kwa wananchi .... Hamna cha maana walichokuwa wanafanya zaidi ya kusubiri maelekezo, kupiga kelele na kujitutumua kuonyesha wana madaraka. They were incompetent at every level you could think about!

Sasa badala ya kuletewa mtu kutoka Dodoma, watu wachague mtu wanayemtaka kuwa mkuu wao wa Mkoa ... sijui watu wanashindwa kuelewa nini hapo. Kama wanaona sawa kuchagua Mbunge au diwani mkazi wa eneo husika kwa nini kuna tatizo kwenye mkuu wa Wilaya au Mkoa. Utafikiri Mkuu wa Mkoa na Wilaya ndiyo wanaotuunganisha Watanzania. Imagine mpaka Katibu Tarafa na Kata wanachaguliwa Dodoma!!
 
Na hii Sera ya majimbo inaonekana imewasika pabaya maana naona ngojera nyingi sana toeni Sera zenu mnaacha kunadi Sera zenu mnakomaa na za lisu
Tuelezeni basi hata ndege hizo tunafaidikaje sisi wananchi wa mgombe huku kasulu maana tunakula vumbi tu maji tope tu lomejaa
 
Nimekakuta sehemu.
Screenshot_20200923-103547.jpg
 
Concept ya majinbo ,ni kutolaliana kuwa mnachangia gharama za uendeshaji jimbo kwa mgawanyo sawa na hakuna eneo linamlalia mwenzie chake.

Jimbo hugawanywa kwa mikoa lakini kila mkoa chake chake sio kuwa singida ataponea pesa zitazoingizwa morogoro hata kama wako jimbo moja isipokuwa kwa ile miradi ya pamoja.

Ukiunda jimbo ni kuwa mfano umeunda jimbo lenye mikoa miwili wa singida na kilimanjaro usidhani hapo kuwa pesa za utalii za kilimanjaro zitaenda singida .Haiwezekani .kodi kila mkoa unakusanya zake asilimia fulani ndio wanapeleka mfuko wa jimbo hawapeleki zote kwa ajili ya kugharimia gharama za uendeshaji wa jimbo. Lakini hakuna mkoa ambao utabeba mkoa mwingine kwa pesa zake kila mmoja anajibeba mweyewe.
Tunajua mnatamani sana kuingia ikulu na ni haki yenu, ni bahati mbaya kwamba tayari mmesha feli kukamata dola, sababu zitazowafelisha ni ilani yenu. Kinachowafelisha ni hiki hapa;
!) kujipambanua kwamba serikali yenu haitakusanya kodi badala yake mta weka dhamana rasilimali za nchi ili muweze kukopa pesa za kuendesha serikali. hapa mme score 0%.

Kuweka dhamana mali za nchi ni hatari sana kwa usalama wan chi, hiyo ni sawa na kuweka rehani sovereignty ya Tanzania. Kwa lugha nyingine nyie mnakuja kuwa madalali wan kwa nchi yenu. Hapa hakuna ushindi ni kushindwa mapema sana

ii) Kuanzisha utawala wa majimbo ambao kwa tafsiri ya haraka ni kwamba serikali za majimbo ziundwe na wenyeji wa kanda ile ni kurudisha ukabila na halitawezekana kwa sababu ya mchanganyiko ya makabila ambayo yamehama kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Hapa tegemea mtifuano wa kikabila ambao hautamalizika na mwisho wake ni kugawana mbao. Mfumo huu pia utaleta changamoto kaatika kugawanya the little resources of the country. Hapa mtapata 0% score

Kwa ujumla ilani yenu ina mapungufu mengi sana kwani matarajio mliyoyaweka hayatekelezeki, nadhani ilani ilitayarishiwa bara tofauti na bara la Afrika

Kwa hayo mawili hapo juu tayari mmeikosa ikulu hata kambi rasmi ya upinzani bungeni hamtaipata. Tusubiri tarehe 28/10
 
Unakimbilia USA kabla ya kuweza Jumuiya ya Africa Mashariki kwanza ambayo M7 anataka awe Rais wake wa kwanza!
Mimi nitakuwa wa kwanza kuunga mkono jimbo la Tanzania iwapo wataibuka kina Kwame Nkrumah wa miaka ya sasa watakaoanzisha wazo la United States of Africa.
 
Kwani sera ya majimbo ndio utajiri?Nchi kuendelea Kuna factor nyingi kuwa tu na mfumo mzuri wa utawala haitoshi lakini kwa mazingira ya Tzn ,tukiweka mfumo huu nchi itapaa Sana kiuchumi.Leo hii Zanzibar iko hoi kiuchumi kuliko awali kwa sababu iko treated Kama mkoa
Mkuu nadharia na uhalisia ni vitu viwili tofauti.
 
Kwa sababu mfumo uliopo unakinufaisha zaidi chama chako na ndio waliohodhi mchakato wa katiba mpya ilikuwa lazima ipigwe chini

Naiangalia Tanzania kwa umuhimu wake kuliko vyama vya kisiasa, majimbo ni cha kike.
 
eti nchi itasambaratika ndio yule kichaa wenu kawaambia halafu mlivyo hamnazo you run with that nonsense!

Kama ni hivyo basi USA,South Africa,Kenya,Canada,India...na even your beloved stupid totalitarian China ungekuta washa sambaratika,lakini wapo na wanazidi prosper..

Hamna hoja kwenye hili,Lissu katoa msumari na wananchi seem to accept hapo ndio matako yanawauma sana..

Eti tutasambaratika,jibu la hovyo sana...halafu wananchi hawajawaelewa na majibu yenu kabisa mnabaki kuchanganyikiwa even more

Natukana yes,kashitaki kwa mawe!

Sera ya majimbo kwa Tanzania iliyoasisiwa na Nyerere aliyeijenga nchi kwa misingi ya umoja ni jambo lisilowezekana.
 
Hivi mnadhani kwa kuwa chama tawala nyie mna hatimiliki ya akili za Watanzania?

Kwamba sisi hatuelewi tunachoambiwa kuhusu majimbo yanayosemwa na kwamba tutapelekwa tu halutakuwa na vikao vya kuamua namna gani hayo majimbo yaendeshwe? Faida mojawapo ya majimbo tumeelezwa ni kuongozwa na Magavana wa kuchaguliwa, sasa hivi Wakuu wa mikoa na wilaya hawana tofauti na viongozi wa Kikoloni (Area commissioners) waliokuwa wanqogopwa kwa kukamata wananchi na kuwaweka ndani hata kwa makosa yasiyotajwa kwenye sheria.

Mmemsilkia Magufuli mwenyewe akisema wazi hata vitambulisho vya Machinga watu hawakupaswa kulazimishwa, lakini uliza mikoani Wakuu wa Wilaya ambao ni wateule wa Rais na Makada wa CCM wamewatendea nini Wananchi? Ni watumishi wangapi wamekamatwa kwa amri ya maDc kwa kosa la kuchelewa kikao cha mkubwa, huku sheria ikimtaka DC kukamata na kuweka ndani masaa 24 kwa makosa ya jinai na uvunjifu wa amani pekee na si makosa ya Nidhamu? Tumechoshwa na umyanyasaji wa "Wakoloni" wenu weusi.
Yaani hawa wakoloni weusi ni wabaya hata kuliko mzungu, wanakung'ata huku wanakuchekea.
 
Kwani gharama za kuendesha mikoa na wilaya kwa sasa zinatoka wapi?
 
Lisu anaongelea tu majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji jimbo litatoa wapi.

Anaeleza kijanja janja huku akificha kuwa uendeshaji jimbo unatakiwa uendeshwe kwa pesa za ndani ya jimbo ikiwemo miradi ya maendeleo.

Chukulia Singida tegemeo lake kuu la uchumi ni kuuza vidumu vya mafuta ya alizeti. Hivyo vyaweza jenga barabara za lami? Kilomita moja tu ya lami inasoma Gharama ya bilioni moja. Hivyo vidumu vya alizeti vyaweza jenga barabara na kulipa mishahara ya wafayakazi wa jimbo?

Afafanue pia kuhusu gharama za kuendesha jimbo asilaghai tu ohh mujiamulie wenyewe.

Ukimsikiliza uaona kabisa mlaghai kwenye gharama za uendeshaji na za miradi ya maendeleo zitakako toka hagusi anahamia hoja nyingine mbio.
Mbona logic ni.simple mkuu namna ya kuendesha shughuli za kijimbo. Ni hv ngazi ya jimbo inabebwa kuanzia mikoa miwili yaan kanda. Ktk hayo maeneo kuna shughuli za kiuchumi. Shughuli za kiuchumi huzalisha kodi za ndani ambazo hutumika kutatua kero ndani.ya hayo maeneo kabla.ya kuomba msaada serikali kuu. Serikali kuu.inabaki kudeal na mishahara ya wafanyakazi nchi nzima na majanga km tetemeko,mafuriko, dharura yyt ile. Vyanzo vyake vya mapato ni bandari zote, viwanja vya ndege, gas asilia, hifadhi za taifa na pori tengefu, viwanda vikubwa na makampuni ya kitaifa km.mitandao ya simu nk
 
Najua watanzania ni wavivu wa kusoma lakini tafuta na ujaribu kusoma mambo ya "Federal System of Government and its Principles of Governance", au utafute mtu akutafsiriye ili uelewe anachomaanisha Lissu.

Kwa sababu watu wengine mnaongea humu utafikiri huu mfumo ni ngeni duniani na haijawahi kutumiwa na nchi yoyote ile.

Kwa wale wanaopenda mfumo wa kidikteta au wenye maslahi nao hawawezi kuupenda huu mfumo kwani sio rafiki kwa matakwa yao.
 
Lisu anaongelea tu majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji jimbo litatoa wapi.

Anaeleza kijanja janja huku akificha kuwa uendeshaji jimbo unatakiwa uendeshwe kwa pesa za ndani ya jimbo ikiwemo miradi ya maendeleo.

Chukulia Singida tegemeo lake kuu la uchumi ni kuuza vidumu vya mafuta ya alizeti. Hivyo vyaweza jenga barabara za lami? Kilomita moja tu ya lami inasoma Gharama ya bilioni moja. Hivyo vidumu vya alizeti vyaweza jenga barabara na kulipa mishahara ya wafayakazi wa jimbo?

Afafanue pia kuhusu gharama za kuendesha jimbo asilaghai tu ohh mujiamulie wenyewe.

Ukimsikiliza uaona kabisa mlaghai kwenye gharama za uendeshaji na za miradi ya maendeleo zitakako toka hagusi anahamia hoja nyingine mbio.
Nchi zenye majimbo (Marekani, Ujerumani, Nigeria, DRC,...) zinafanye?

wakoloni walitutawala kwa mfumo wa majimbo hela za kuyaendeshea majimbo zilitoka wapi?
 
Decentralization ni muhimu kwa Nchi yetu tens itapunguza gharama
 
Lisu anaongelea tu majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji jimbo litatoa wapi.

Anaeleza kijanja janja huku akificha kuwa uendeshaji jimbo unatakiwa uendeshwe kwa pesa za ndani ya jimbo ikiwemo miradi ya maendeleo.

Chukulia Singida tegemeo lake kuu la uchumi ni kuuza vidumu vya mafuta ya alizeti. Hivyo vyaweza jenga barabara za lami? Kilomita moja tu ya lami inasoma Gharama ya bilioni moja. Hivyo vidumu vya alizeti vyaweza jenga barabara na kulipa mishahara ya wafayakazi wa jimbo?

Afafanue pia kuhusu gharama za kuendesha jimbo asilaghai tu ohh mujiamulie wenyewe.

Ukimsikiliza uaona kabisa mlaghai kwenye gharama za uendeshaji na za miradi ya maendeleo zitakako toka hagusi anahamia hoja nyingine mbio.

Nyie gharama za kuendesha mikoa na halmashauri mnapata wapi?

Mnahoji as if Lisu anaenda kuwa rais wa familia yake

Hiyo miradi mikubwa yote nyie pesa mlizitoa wapi?
 
Back
Top Bottom