Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Hao wananchi wanaopelekewa maamuzi karibu wanao wabunge na madiwani wanaowapigia kura wao wenyewe na wenye kuishi nao...kwani sasa hivi tunapounda mikoa huwa tunatazama kama mkoa unaweza kujitegemea au la?
..kuunda mamlaka za majimbo lengo lake ni kupeleka huduma za serikali na kiutawala karibu zaidi na wananchi, ili kuharakisha maendeleo.
..tutakapokuwa na mamlaka za majimbo kutakuwa na kodi za serikali kuu, na kodi za mamlaka nyingine kama jimbo na halmashauri.
..hivyo basi, kama ilivyo sasa hivi kutakuwa na maeneo wana makusanyo makubwa zaidi, na kutakuwa na maeneo yenye makusanyo madogo.
..eneo ambalo lina makusanyo madogo litapewa msaada mkubwa toka serikali kuu, as compared to eneo lenye makusanyo makubwa. hivyo ndivyo inavyofanyika sasa hivi, na ndivyo itakavyoendelea kufanyika wakati wa mfumo wa majimbo.
..Ubinywaji wa haki, ubaguzi, na ukatili, kama tunavyoshuhudia ktk utawala wa Jpm ndiyo mtego mbaya kabisa kwa utaifa wa Tanzania. Mfumo wa majimbo utatusaidia kupunguza makali ya watawala wabovu ikiwa tutafanya makosa ktk sanduku la kura. Tukichagua Raisi mbaguzi basi tutasalimikia kwenye utawalawa jimbo unaotenda haki. Watakaochagua kiongozi mzembe wa jimbo, serikali kuu itakuwa kimbilio lao.
NB:
..Dodoma imekuwa mji mkuu hivyo usitegemee kwamba jiji hilo na maeneo ya jirani litaendelea kuwa masikini kama tulivyozoea miaka ya nyuma. Singida nayo itafaidika kwa kuwepo kwake karibu na Dodoma, lakini zaidi Singida imegundulika kuwa na potential kubwa sana ktk kilimo cha Korosho.
Serikali ipo mpaka ngazi ya chini na ni hai siuoni umuhimu wa kuigawa nchi kiutawala wakati zipo njia za kidemokrasia za kuwakilisha maoni na matakwa ya mtu mmoja mmoja.
Kuamini kuwa mtu wa kawaida hawezi kufikiwa na maendeleo ni kutoamini katika uwezo wa wabunge na madiwani.