Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

..kwani sasa hivi tunapounda mikoa huwa tunatazama kama mkoa unaweza kujitegemea au la?

..kuunda mamlaka za majimbo lengo lake ni kupeleka huduma za serikali na kiutawala karibu zaidi na wananchi, ili kuharakisha maendeleo.

..tutakapokuwa na mamlaka za majimbo kutakuwa na kodi za serikali kuu, na kodi za mamlaka nyingine kama jimbo na halmashauri.

..hivyo basi, kama ilivyo sasa hivi kutakuwa na maeneo wana makusanyo makubwa zaidi, na kutakuwa na maeneo yenye makusanyo madogo.

..eneo ambalo lina makusanyo madogo litapewa msaada mkubwa toka serikali kuu, as compared to eneo lenye makusanyo makubwa. hivyo ndivyo inavyofanyika sasa hivi, na ndivyo itakavyoendelea kufanyika wakati wa mfumo wa majimbo.

..Ubinywaji wa haki, ubaguzi, na ukatili, kama tunavyoshuhudia ktk utawala wa Jpm ndiyo mtego mbaya kabisa kwa utaifa wa Tanzania. Mfumo wa majimbo utatusaidia kupunguza makali ya watawala wabovu ikiwa tutafanya makosa ktk sanduku la kura. Tukichagua Raisi mbaguzi basi tutasalimikia kwenye utawalawa jimbo unaotenda haki. Watakaochagua kiongozi mzembe wa jimbo, serikali kuu itakuwa kimbilio lao.

NB:

..Dodoma imekuwa mji mkuu hivyo usitegemee kwamba jiji hilo na maeneo ya jirani litaendelea kuwa masikini kama tulivyozoea miaka ya nyuma. Singida nayo itafaidika kwa kuwepo kwake karibu na Dodoma, lakini zaidi Singida imegundulika kuwa na potential kubwa sana ktk kilimo cha Korosho.
Hao wananchi wanaopelekewa maamuzi karibu wanao wabunge na madiwani wanaowapigia kura wao wenyewe na wenye kuishi nao.

Serikali ipo mpaka ngazi ya chini na ni hai siuoni umuhimu wa kuigawa nchi kiutawala wakati zipo njia za kidemokrasia za kuwakilisha maoni na matakwa ya mtu mmoja mmoja.

Kuamini kuwa mtu wa kawaida hawezi kufikiwa na maendeleo ni kutoamini katika uwezo wa wabunge na madiwani.
 
..kinachokwenda kufanyika ni kuwapa mamlaka zaidi ya waliyonayo sasa hivi.

..Jpm amenyang'anya halmashauri mapato yote na kuyapeleka kwa serikali kuu.

..matokeo yake ndiyo tunamuona anatembea na majunia ya fedha akizigawa anavyojisikia.

..mfumo wa majimbo unakwenda kuwalinda wananchi na viongozi wa hovyo-hovyo kama Jpm.

..Tunakwenda kuzi-empower mamlaka za majimbo, halmashauri, wabunge, madiwani, ili waweze kuwatumikia kwa wakati wananchi.
 
Mfano jimbo la kawe lina hazina ya rasilimali watu ya kutosha lakini mbunge wetu Halima kwa miaka kumi hata mara moja hajawahi kuonekana bunju A wala B yeye muda wote ni kuzozana na watu Twitter.
Shida yenu nyie ni mambumbumbu sana ndiyo maana hata majibu yenu ni ya kishenzi
 
..kinachokwenda kufanyika ni kuwapa mamlaka zaidi ya waliyonayo sasa hivi.

..Jpm amenyang'anya halmashauri mapato yote na kuyapeleka kwa serikali kuu.

..matokeo yake ndiyo tunamuona anatembea na majunia ya fedha akizigawa anavyojisikia.

..mfumo wa majimbo unakwenda kuwalinda wananchi na viongozi wa hovyo-hovyo kama Jpm.

..Tunakwenda kuzi-empower mamlaka za majimbo, halmashauri, wabunge, madiwani, ili waweze kuwatumikia kwa wakati wananchi.
Well said mkuu. Umechambua vema sana. Nikipaki gari nitaongezea nyama
 
Usilazimishe Kutokuelewa Kwa Maksudi, unazidi kuudhihirisha ujuha wako.

Je, unayajua Majimbo yatakavyokua na mikoa itakayoyaunda hayo majimbo?

Hiyo singida uisemayo itakua katika jimbo la kati litakalojumuisha mikoa ya MOROGORO, DODOMA SINGIDA NA TABORA. haya hapo umasikini unatokea wapi ikiwa kuna vyanzo vingi vya mapato katk mikoa hiyo.

Mnakera hata kama mnalipwa, wengi ni mambumbumbu. Yaani weupe vichwani.
Akili ya mbu unatumia.
 
..kwani sasa hivi tunapounda mikoa huwa tunatazama kama mkoa unaweza kujitegemea au la?

..kuunda mamlaka za majimbo lengo lake ni kupeleka huduma za serikali na kiutawala karibu zaidi na wananchi, ili kuharakisha maendeleo.

..tutakapokuwa na mamlaka za majimbo kutakuwa na kodi za serikali kuu, na kodi za mamlaka nyingine kama jimbo na halmashauri.

..hivyo basi, kama ilivyo sasa hivi kutakuwa na maeneo wana makusanyo makubwa zaidi, na kutakuwa na maeneo yenye makusanyo madogo.

..eneo ambalo lina makusanyo madogo litapewa msaada mkubwa toka serikali kuu, as compared to eneo lenye makusanyo makubwa. hivyo ndivyo inavyofanyika sasa hivi, na ndivyo itakavyoendelea kufanyika wakati wa mfumo wa majimbo.

..Ubinywaji wa haki, ubaguzi, na ukatili, kama tunavyoshuhudia ktk utawala wa Jpm ndiyo mtego mbaya kabisa kwa utaifa wa Tanzania. Mfumo wa majimbo utatusaidia kupunguza makali ya watawala wabovu ikiwa tutafanya makosa ktk sanduku la kura. Tukichagua Raisi mbaguzi basi tutasalimikia kwenye utawalawa jimbo unaotenda haki. Watakaochagua kiongozi mzembe wa jimbo, serikali kuu itakuwa kimbilio lao.

NB:

..Dodoma imekuwa mji mkuu hivyo usitegemee kwamba jiji hilo na maeneo ya jirani litaendelea kuwa masikini kama tulivyozoea miaka ya nyuma. Singida nayo itafaidika kwa kuwepo kwake karibu na Dodoma, lakini zaidi Singida imegundulika kuwa na potential kubwa sana ktk kilimo cha Korosho.
Kuhusu federation naona kuna ushabiki mkubwa wa kinadharia kuliko ukweli. Federation kwa watanzania hawa haiwezekani.. hatujajiandaa kiakili na kiutamaduni kuelekea huko.

Ni mawazo yangu tu! Narudia mawazo haya ni yangu. Mfumo wa unitary system ni mfumo bora zaidi kwa Tanzania ukizingatia ukubwa wake na wingi wa watu. Watanzania sio wengi sana mpaka washindwe kujiongoza chini ya mwamvuli mmoja wa serikali ya umoja na wala nchi sio kubwa sana kushindwa kuongoza kutokea Dodoma.

Sasa makando kando yanatoka wapi mpaka maswala ya serikali za kijimbo yanajitokeza! Yako mambo mengi lakini nadhani makubwa zaidi ni yafuatayo.

1) Umasikini.
Kuongezeka kwa wimbi la umasikini na vijana wengi kukosa ajira kumefanya watu kuwa frustrated. Ukizingatia wamejengwa juu ya msingi wa Umoja walitaraji serikali iwabail kwa kuwapa ajira na hilo halijawezekana na ni wazi kuna sababu nyingi ambazo zimesababisha.

2) Uwezo mdogo wa Serikali kimapato.
Hii imepelekea serikali kujikuta inatakiwa kufanikisha miradi ya maendeleo kwa uchache na kwa maeneo eneo tu. Hivyo kuacha maeneo mengi yakisubiria miradi hii. Inahitaji moyo mgumu kufanya maamuzi yakutumia rasilimali chache kuwaletea maendeleo wengi..maana malalamiko hayatakosekana.

3) Ujinga (au Ukosefu wa taarifa sahihi)
Watanzania wengi tunadandia dandia vistori tunavyobeba mitandaoni bila kufanya upekuzi na kudadisi. Kila jambo lamfaa mtu kwa nafasi yake mahali pake na shida zake. Nadhani si sahihi sana kujilinganisha na mataifa mengine. Sisi ni watanzania ni lazima tuwe na solutions zetu.

Hayo juu kwa sehemu kubwa yamepelekea kuwa na chuki kubwa kati ya watanzania na watanzania. Ukifika Handeni wazigua wanalamika wachaga na wapare wamechukua ardhi yao. Ukweli ni chuki baada ya wachaga kutengeneza faida kubwa kutoka katika ardhi ambayo wazigua waliutekeleza na baadae kuiuza wakijua haina thamani.

Shida hizo ziko kila mahali, nchini lakini zinachagizwa na umasikini uliokithiri.. ambao ukiutazama ni swala la kimfumo ambalo halihitaji federal government na state governments. Linahitaji kusimamia mifumo iliyopo kwa bidii na weledi basi.

Tabia ya quick gratification ndiyo inayotufikisha hapa. Watanzania wanapenda kupewa. Tulifanya audit humu wangapi wamefanya initiative yoyote kuleta maendeleo kijijini kwake au hata usafi mtaani kwake!? Wengi tunaolalamika tunataka wengine wafanye..

Na ukweli ni kuwa hata tungekuwa na serikali za kila kitongoji kama watanzania sisi hatujitoi kwenda kufanya kazi na kuboresha mifumo hatuwezi kamwe kwenda kokote.

Ujerumani haikuja Afrika kutafuta makoloni ni Kampuni zilizokuja na kufanya makoloni kwa ajili ya nchi zao, makampuni mengi makubwa ya ulaya huja baada ya makampuni madogo kutoa jasho na damu kutafuta masoko na kuyasecure... Sisi tutaka tupelekwe tuoneshwe haya pale kaa ule.

Na hata tukipelekwa katika maeneo hayo (mfano kuajiriwa serikalini) kazi hatufanyi tunanenepeana na kuning'iniza funguo za magari kwenda kulewa weekend hakuna value tunayoleta katika meza.. sasa haya sio matatizo ya serikali moja na wala hayaletewi suluhu na federation.. ni matatizo ya makuzi watanzania tumedekezana sana.

Ukibahatika kufanya kazi katika taasisi za kimataifa utaelewa kwann sisi tuko hapa.. ni uvivu ndio unaotutafuna. Na zao lake ni Choyo, Umimi, Kijicho na roho mbaya... Kuwa watu wa kusingizia na kutokukubali responsibility.

Tukipata wasaa tujadili kwa kina how states will work... Kama tulivyo sisi na Zanzibar!? Au itakuwa mikoa tu mikubwa!?

Maana ikiwa kama tulivyo na Zanzibar yako mengi ambayo nayaona ambayo yanaweza yasifanikiwe.. mgawanyo wa mali utakuwaje!? Tuanzie hapo. Mf. Kwa mbuga zinazotoka mkoa mmoja mwenda mwingine (Serengeti) nani atahakikisha mtalii aliyelipia kanda ya kaskazini hapiti kanda ya ziwa na ikiwa atapita atakuwa amelipa huko pia!? Je kutakuwa na jeshi kila state!? Au kukata majimbo haya kutazingatia vivutio kama hivi vinakuwa ndani ya jimbo moja tuu!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
..kinachokwenda kufanyika ni kuwapa mamlaka zaidi ya waliyonayo sasa hivi.

..Jpm amenyang'anya halmashauri mapato yote na kuyapeleka kwa serikali kuu.

..matokeo yake ndiyo tunamuona anatembea na majunia ya fedha akizigawa anavyojisikia.

..mfumo wa majimbo unakwenda kuwalinda wananchi na viongozi wa hovyo-hovyo kama Jpm.

..Tunakwenda kuzi-empower mamlaka za majimbo, halmashauri, wabunge, madiwani, ili waweze kuwatumikia kwa wakati wananchi.
Mamlaka za miji zilikuwa empowered kwa miaka mingi tu kabla ya Magufuli haja ingia ikulu na kilichokuwa kikifanyika ni ufisadi wa kiwango cha juu.

Hizo halmashauri zilipokuwa na uhuru wa matumizi ya pesa hakuna cha maana kilichofanyika zaidi ya upigaji wa madiwani.

Awamu hii miradi mikubwa inafanyika na tija inaonekana, kubana matumizi ya pesa kuna faida zake tena nyingi tu, hizo meli zinazojengwa na zahanati mamia kwa mamia ni nidhamu nzuri ya matumizi.

Na ikiwepo nidhamu mabadiliko ni lazima yawepo.

Rais wa Tanzania anayo pesa ya matumizi shilingi milioni mia kwa mwezi. JK alinunulia masuti, Mkapa akanunulia mikufu ya dhahabu na huyu anachangia ujenzi wa shule na kuwapa kina Peter Tino wakialikwa pale ikulu.
 
Kuhusu federation naona kuna ushabiki mkubwa wa kinadharia kuliko ukweli. Federation kwa watanzania hawa haiwezekani.. hatujajiandaa kiakili na kiutamaduni kuelekea huko.

Shida hizo ziko kila mahali, nchini lakini zinachagizwa na umasikini uliokithiri.. ambao ukiutazama ni swala la kimfumo ambalo halihitaji federal government na state governments. Linahitaji kusimamia mifumo iliyopo kwa bidii na weledi basi.

Tabia ya quick gratification ndiyo inayotufikisha hapa. Watanzania wanapenda kupewa. Tulifanya audit humu wangapi wamefanya initiative yoyote kuleta maendeleo kijijini kwake au hata usafi mtaani kwake!? Wengi tunaolalamika tunataka wengine wafanye..

Na ukweli ni kuwa hata tungekuwa na serikali za kila kitongoji kama watanzania sisi hatujitoi kwenda kufanya kazi na kuboresha mifumo hatuwezi kamwe kwenda kokote.

Ukibahatika kufanya kazi katika taasisi za kimataifa utaelewa kwann sisi tuko hapa.. ni uvivu ndio unaotutafuna. Na zao lake ni Choyo, Umimi, Kijicho na roho mbaya... Kuwa watu wa kusingizia na kutokukubali responsibility.

Tukipata wasaa tujadili kwa kina how states will work... Kama tulivyo sisi na Zanzibar!? Au itakuwa mikoa tu mikubwa!?

Maana ikiwa kama tulivyo na Zanzibar yako mengi ambayo nayaona ambayo yanaweza yasifanikiwe.. mgawanyo wa mali utakuwaje!? Tuanzie hapo. Mf. Kwa mbuga zinazotoka mkoa mmoja mwenda mwingine (Serengeti) nani atahakikisha mtalii aliyelipia kanda ya kaskazini hapiti kanda ya ziwa na ikiwa atapita atakuwa amelipa huko pia!? Je kutakuwa na jeshi kila state!? Au kukata majimbo haya kutazingatia vivutio kama hivi vinakuwa ndani ya jimbo moja tuu!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app

..Wewe ni mjenga hoja mzuri. Heshima kwako.

..Naomba nijibu baadhi ya hoja zako harakaharaka kwasababu ya muda.

1. Kweli mfumo wa majimbo bado ni nadharia. Unaweza ukafaulu, au unaweza ukafeli. Jambo la msingi ni kuutengeneza kwa namna ambayo utatuletea matokeo mazuri tunayoyataka.

2. Mfumo huu wa utawala tulionao umeishafeli. Ungekuwa haujafeli hoja ya majimbo isingekuwepo mezani. Tunaweza kujaribu kuurekebisha, lakini umesharekebishwa mara kadhaa na umeendelea kufeli. Nyerere aliwahi kuurekebisha kwa mpango wa madaraka mikoani. Pia aliwahi kukiri kufanya makosa kuvunja serikali za mitaa.

3. Utamaduni wa kupenda kupewa umetoka na mfumo huu wa serikali kuu. Wananchi waliaminishwa kwamba serikali kuu na Raisi ndiyo walezi wao hivyo wasubiri kila kitu wataletewa. Nadhani kauli kwamba Raisi ni sawasawa na "BABA" siyo ngeni kwako. Tatizo la Watanzania kuwa wategemezi linatokana na mfumo wetu wa utawala.

4. Tunatakiwa tutengeneze a taxable society. Tuwe na watu wanaolipa kodi, hata kama wanalipa kodi kidogo, na wanaona matumizi ya kodi zao. Wananchi wawe na mamlaka ya kuhoji kodi yao inatumika vipi. Na vilevile tuwe na viongozi waliochaguliwa na wananchi, na wanaowajibika kwa wananchi.

5. Sitegemei kwamba kutakuwa na majimbo yenye hadhi sawa na Zanzibar. Yakiletwa majimbo ya namna hiyo nitayapinga. Vilevile Tanganyika ktk historia yake haijapata kuwa na majimbo yenye hadhi sawa na Zanzibar ya leo.

6. Swali lako kuhusu rasilimali kama mbuga ya Serengeti ambayo upo uwezekano wa ku-cross majimbo zaidi ya moja ni zuri sana. Mimi kwa mtizamo wangu rasilimali za namna hiyo zinatakiwa kuwa chini ya Serikali kuu ambayo ndiyo itayapa majimbo husika mgao wao, na itaweka sheria na miongozi kuhusu matumizi yake.
 
Mamlaka za miji zilikuwa empowered kwa miaka mingi tu kabla ya Magufuli haja ingia ikulu na kilichokuwa kikifanyika ni ufisadi wa kiwango cha juu.

Hizo halmashauri zilipokuwa na uhuru wa matumizi ya pesa hakuna cha maana kilichofanyika zaidi ya upigaji wa madiwani.

Awamu hii miradi mikubwa inafanyika na tija inaonekana, kubana matumizi ya pesa kuna faida zake tena nyingi tu, hizo meli zinazojengwa na zahanati mamia kwa mamia ni nidhamu nzuri ya matumizi.

Na ikiwepo nidhamu mabadiliko ni lazima yawepo.

Rais wa Tanzania anayo pesa ya matumizi shilingi milioni mia kwa mwezi. JK alinunulia masuti, Mkapa akanunulia mikufu ya dhahabu na huyu anachangia ujenzi wa shule na kuwapa kina Peter Tino wakialikwa pale ikulu.

..sasa hivi upigaji umehamia Ikulu.

..hizo milioni 100 kwa mwezi kwa ajili ya Raisi zilitakiwa kuundiwa sheria ya matumizi yake kama ilivyofanyika kwa mfuko wa fedha za maendeleo ya jimbo.
 
..Wewe ni mjenga hoja mzuri. Heshima kwako.

..Naomba nijibu baadhi ya hoja zako harakaharaka kwasababu ya muda.

1. Kweli mfumo wa majimbo bado ni nadharia. Unaweza ukafaulu, au unaweza ukafeli. Jambo la msingi ni kuutengeneza kwa namna ambayo utatuletea matokeo mazuri tunayoyataka.

2. Mfumo huu wa utawala tulionao umeishafeli. Ungekuwa haujafeli hoja ya majimbo isingekuwepo mezani. Tunaweza kujaribu kuurekebisha, lakini umesharekebishwa mara kadhaa na umeendelea kufeli. Nyerere aliwahi kuurekebisha kwa mpango wa madaraka mikoani. Pia aliwahi kukiri kufanya makosa kuvunja serikali za mitaa.

3. Utamaduni wa kupenda kupewa umetoka na mfumo huu wa serikali kuu. Wananchi waliaminishwa kwamba serikali kuu na Raisi ndiyo walezi wao hivyo wasubiri kila kitu wataletewa. Nadhani kauli kwamba Raisi ni sawasawa na "BABA" siyo ngeni kwako. Tatizo la Watanzania kuwa wategemezi linatokana na mfumo wetu wa utawala.

4. Tunatakiwa tutengeneze a taxable society. Tuwe na watu wanaolipa kodi, hata kama wanalipa kodi kidogo, na wanaona matumizi ya kodi zao. Wananchi wawe na mamlaka ya kuhoji kodi yao inatumika vipi. Na vilevile tuwe na viongozi waliochaguliwa na wananchi, na wanaowajibika kwa wananchi.

5. Sitegemei kwamba kutakuwa na majimbo yenye hadhi sawa na Zanzibar. Yakiletwa majimbo ya namna hiyo nitayapinga. Vilevile Tanganyika ktk historia yake haijapata kuwa na majimbo yenye hadhi sawa na Zanzibar ya leo.

6. Swali lako kuhusu rasilimali kama mbuga ya Serengeti ambayo upo uwezekano wa ku-cross majimbo zaidi ya moja ni zuri sana. Mimi kwa mtizamo wangu rasilimali za namna hiyo zinatakiwa kuwa chini ya Serikali kuu ambayo ndiyo itayapa majimbo husika mgao wao, na itaweka sheria na miongozi kuhusu matumizi yake.
Bwana Jiwe mie nikushukuru.. Sana na ninatamani kuona siku moja unajiunga na chama chetu cha Mapinduzi... Wewe ni mtu sahihi... Na naona mawazo yako ni mema.

Labda niongezee kidogo kwenye hoja hii ya majimbo. Mie ninadhani kama hatuwezi kwenda all the way in na majimbo ni bora tubakie njia kuu.. kwanini.

1) Huu ni mfumo ambao tumeuwekeza kwa miaka 50+.. unayo madhaifu..Ndiyo. lakini tusiutupe kwa msala upitao. Maeneo yote uliyoyaandazia ninadhani yanaweza kujibika.

Kuna kitu kinaitwa "Master plan" au interim land use plans na strategic plans.. moja ya components za vitu hivi ni clear road map kuelekea magoli tuliyojiwekea.

Hivi ni vitu vilivyosahaulika na vimetufanya tuwe wazee wa free style... Wananchi hawajui wanakwenda wapi, viongozi (wasimamizi wa halmashauri) ambao ndio watendaji pia hawajui a wala ba.

Kwanza kabisa ningeshauri hapa hapa tulipo tujiwekeze kwenye kuandaa mipango kabambe(master plans) ili tuzitumie kuwapima viongozi wetu namna wanavyojizatiti katika kututumikia.

Master plans zinacapture community desires, scientifically zinaquantify desires into scientific bits na Kisha zinatengeneza road map kufikia desires zetu zikiainisha timeframe, landmarks, actors and other resources needed na mwisho namna ya kuzimobilize resources.

Nchi za wenzetu ndivyo zinavyoendeshwa. Na hilo halihitaji federation linahitaji unified community ambayo iko socially engaged Kutatua issues zake.

2) Kupanua Tax base tunahitaji Country planning na Regional planning. Hii inasaidia kuharmonise all individual city and town master plans kuelekea mahala pamoja. Ukiisoma vizuri Ilani ya Chama Cha Mapinduzi utagundua imejengwa juu ya msingi huu.. sasa inachokosa ni scientific inputs kuifanya iwe bora zaidi..

Lakini at least sio ya kufikirika au kinadharia tu. Ina mrengo wa kufanikisha Country plan. Tangu Uhuru hatuna sensa ya makazi na hatujawahi kuwa na malengo mahususi ya kuboresha makazi... Hatujafanya comprehensive country planning tangu Malkia aondoke.. yote haya yana mchango mkubwa kufanikisha namna bora ya kutawala.

Ila ni wazi kabisa hayahitaji serikali ya mtindo tofauti yanahitaji commitment ya watanzania wote, na yanahitaji viongozi focused na wenye Ajenda ya kitaifa.

Bwana JokaKuu napata raha kuona vijana tunajadili kwa namna kama hii.. ni swala jema kwa mustakabali wa taifa letu..

Saa kuhusu kuongeza Tax base.. lazima tuongeze kipato na kuandaa mfumo ambao kila mtanzania ataunganishwa kwenye mnyororo wa thamani..

Fikiria mto Nile ndio mnyororo wa thamani na wote walio pembezoni mwake kuanzia vijiji vidogo Uganda mpaka majiji makubwa kama Cairo wanafaidika ila kila mtu kwa bidii yake, wengine sana na wengine kidogo kulingana na namna kila mmoja anavyohitaji.

Sasa kwetu sisi ardhi ndio sehemu pekee ambayo inatu unify. Tajiri mpaka kapuku sote ardhi yetu inatuleta pamoja. Ni mpango wa serikali kuona ardhi inampa kila mmoja nafasi ya kufurahia maisha. Sasa hili si rahisi.. ni kati ya vitu complex sana.. lakini ni sisi watanzania tunaohitaji kuboresha kwa manufaa yetu na vizazi vya baadae.

Chief, Serikali ni coordinator tu. Tukilijua hilo sidhani mjadala wa Serikali Tatu unakuwa na mashiko.. ambacho ningeshauri na kukubaliana na wewe na kuboresha usimamizi wa kitaasisi na kimfumo ili kuruhusu "ubunifu na uvumbuzi" kuchukua hatamu.. na haya ni sehemu ya machache yanajibika katika ilani yetu mwaka huu.

Bwana JokaKuu ahsante sana mkuu..

Kwa hoja namba sita.. hebu tupate wasaa tuutazame upya maana inaweza kuwa tafrani zaidi.

Ubarikiwe

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Majimbo madhara yake ni makubwa na ya muda mrefu.

Kodi anayolipa mtu wa Mtwara ndivyo inayojenga meli ziwa Victoria.

Kodi anayolipa mkulima wa Kahama Kagera ndio inapanua bandari ya Tanga.

Kodi anayolipa mkulima wa mahindi Ruvuma ndio imejenga kilio kikubwa cha mabasi Dodoma.

Hiyo ndio maana ya umoja wa nchi na ndio kusudio la waasisi wa taifa.

Tukipata tunatumia kwa faida ya wote na tukikosa tunalala njaa wote.

Kauli ya rais lengo lake ni kuwafanya wanasiasa wakukumbuka jukumu lao la msingi kwamba ni kushughulika na shida za watu kuliko kuzama kwenye siasa za kususa na kutoka nje ya jengo la bunge.

Duh! Mkuu Philipo hii kitu ya “ from each according to his ability and to each according to his needs” imeshindwa duniani kote.

Naamini kwa dhati kwamba msingi wa mifumo ya namna hii ni woga na tamaa ya madaraka ya waasisi wake na wala sio upendo au ukarimu kwa wananchi.

Tukubali tu kuwa si vizuri kurudia majaribio kama hayo yatakayozidi kuumiza vizazi vilivyopo na vijavyo.

Na kwa vyovyote vile vizazi vipya havitakubali mifumo ya aina hii itakayoendelea kuvidumaza.
 
Bwana Jiwe mie nikushukuru.. Sana na ninatamani kuona siku moja unajiunga na chama chetu cha Mapinduzi... Wewe ni mtu sahihi... Na naona mawazo yako ni mema.

Labda niongezee kidogo kwenye hoja hii ya majimbo. Mie ninadhani kama hatuwezi kwenda all the way in na majimbo ni bora tubakie njia kuu.. kwanini.

1) Huu ni mfumo ambao tumeuwekeza kwa miaka 50+.. unayo madhaifu..Ndiyo. lakini tusiutupe kwa msala upitao. Maeneo yote uliyoyaandazia ninadhani yanaweza kujibika.

Kuna kitu kinaitwa "Master plan" au interim land use plans na strategic plans.. moja ya components za vitu hivi ni clear road map kuelekea magoli tuliyojiwekea.

Hivi ni vitu vilivyosahaulika na vimetufanya tuwe wazee wa free style... Wananchi hawajui wanakwenda wapi, viongozi (wasimamizi wa halmashauri) ambao ndio watendaji pia hawajui a wala ba.

Kwanza kabisa ningeshauri hapa hapa tulipo tujiwekeze kwenye kuandaa mipango kabambe(master plans) ili tuzitumie kuwapima viongozi wetu namna wanavyojizatiti katika kututumikia.

Master plans zinacapture community desires, scientifically zinaquantify desires into scientific bits na Kisha zinatengeneza road map kufikia desires zetu zikiainisha timeframe, landmarks, actors and other resources needed na mwisho namna ya kuzimobilize resources.

Nchi za wenzetu ndivyo zinavyoendeshwa. Na hilo halihitaji federation linahitaji unified community ambayo iko socially engaged Kutatua issues zake.

2) Kupanua Tax base tunahitaji Country planning na Regional planning. Hii inasaidia kuharmonise all individual city and town master plans kuelekea mahala pamoja. Ukiisoma vizuri Ilani ya Chama Cha Mapinduzi utagundua imejengwa juu ya msingi huu.. sasa inachokosa ni scientific inputs kuifanya iwe bora zaidi..

Lakini at least sio ya kufikirika au kinadharia tu. Ina mrengo wa kufanikisha Country plan. Tangu Uhuru hatuna sensa ya makazi na hatujawahi kuwa na malengo mahususi ya kuboresha makazi... Hatujafanya comprehensive country planning tangu Malkia aondoke.. yote haya yana mchango mkubwa kufanikisha namna bora ya kutawala.

Ila ni wazi kabisa hayahitaji serikali ya mtindo tofauti yanahitaji commitment ya watanzania wote, na yanahitaji viongozi focused na wenye Ajenda ya kitaifa.

Bwana JokaKuu napata raha kuona vijana tunajadili kwa namna kama hii.. ni swala jema kwa mustakabali wa taifa letu..

Saa kuhusu kuongeza Tax base.. lazima tuongeze kipato na kuandaa mfumo ambao kila mtanzania ataunganishwa kwenye mnyororo wa thamani..

Fikiria mto Nile ndio mnyororo wa thamani na wote walio pembezoni mwake kuanzia vijiji vidogo Uganda mpaka majiji makubwa kama Cairo wanafaidika ila kila mtu kwa bidii yake, wengine sana na wengine kidogo kulingana na namna kila mmoja anavyohitaji.

Sasa kwetu sisi ardhi ndio sehemu pekee ambayo inatu unify. Tajiri mpaka kapuku sote ardhi yetu inatuleta pamoja. Ni mpango wa serikali kuona ardhi inampa kila mmoja nafasi ya kufurahia maisha. Sasa hili si rahisi.. ni kati ya vitu complex sana.. lakini ni sisi watanzania tunaohitaji kuboresha kwa manufaa yetu na vizazi vya baadae.

Chief, Serikali ni coordinator tu. Tukilijua hilo sidhani mjadala wa Serikali Tatu unakuwa na mashiko.. ambacho ningeshauri na kukubaliana na wewe na kuboresha usimamizi wa kitaasisi na kimfumo ili kuruhusu "ubunifu na uvumbuzi" kuchukua hatamu.. na haya ni sehemu ya machache yanajibika katika ilani yetu mwaka huu.

Bwana JokaKuu ahsante sana mkuu..

Kwa hoja namba sita.. hebu tupate wasaa tuutazame upya maana inaweza kuwa tafrani zaidi.

Ubarikiwe

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app

..asante.

..lakini pia siyo lazima tuwe na mfumo wa majimbo 100% kama wanavyouelezea CDM.

..vilevile siyo lazima tuwe na mfumo centralized 100% kama huu waliotuletea CCM.

..mimi kuna details ambazo zisipendi ktk mfumo uliopendekezwa na CDM, lakini nakubaliana na malengo makuu na vision ya mfumo huo.

..kwa upande wa CCM naona huu mfumo umepitwa na wakati, ni very un-democratic, na umelenga kukitumia chama tawala kuliko wananchi.

..actually, sipendi kuwaona CDM wakiingia madarakani na kuutumia mfumo huu dhidi ya CCM na vyama vingine.

..tuchukue mazuri yaliyoko ktk mfumo wa sasa, tuchanganye na mazuri yaliyoko ktk mfumo unaopendekezwa, ndipo tupate mfumo utakaotufaa sisi na vizazi vijavyo.
 
Back
Top Bottom