TUNDU LISSU ANAPIGANIA MAMBO YA MSINGI KULIKO HATA DUDU BAYA. LAKINI ANGALIA AKILI ZA WABONGO WENGI HOPELESSLY.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Ukitaka kujua akili za watu angalia yale wanayoyashabikia na kuyapigania. Hiyo itakupa picha upo na watu wa aina gani.
Tundu Lisu ni moja ya wapiganaji wa level za juu katika nchi hii ambapo mambo anayoyapigania yanagusa maisha ya watu moja kwa moja, kila familia, kila ukoo. Mtu yeyote.
Lisu anapigania haki mpaka za viongozi waliopo madarakani, usalama wa taifa, polisi, wanajeshi,magereza, watumishi wa umma na Watanzania wote.
Lisu anapigania HAKI, anataka jamii yehye kufuata sheria, yenye kutii sheria, yenye kuheshimu haki za binadamu.
Lisu hataki watu waonewe. Yeye huo ndio wimbo wake.
Kwa level ya elimu na kiwango cha maarifa alichonacho. Lisu angeweza kula na State, dola akakaa zake kimya maisha yakendelea. Na serikali ingemfaidi. Lakini yeye akachagua njia ngumu.
Dudu baya yeye kaja na Kupinga Ushoga. Kama nilivyosema yuko sawa.
Lakini mshtuko wangu upo hapa,
Uungwaji mkono kwa Dudu baya ni mkubwa sana.
Kila mtu YBWYB kila mtu Linda mgongo wako. Imefikia hatua watu wanachanga kwaajili ya Dudubaya.
Mpaka watu wanachapa Tsheti. Imagine.
Mpaka watu wanatukana basata.
Mpaka wasemaji wa timu za mipira nao. Wanamuunga mkono.
Yaani ni makundi mengi sana.
Lakini upande wa Lisu anayetetea Haki na mambo mengi na makubwa zaidi pamepoa.
Lisu anatetea haki sio tuu za wenye HAKI bali mpaka haki za waliokosea.
Kwamba huyu ni muuaji lakini naye anahaki zake. Yaani mnyonge mnyongeni lakini haki zake mpeni. Mnyongeni kwa kufuata taratibu.
Fikiria watu walivyokuwa wanatekwa alafu kila makundi ya watu wawe wanapiga kelele.
Embu angalia picha ikivuja ya uchi watu watakavyoishabikia. Wanajua kabisa ni uovu. Lakini wanashabikia.
Fikiria suala la Engonga yule aliyevujisha video za uchi. Angalia vijana wanavyompenda. Licha ya kuwa ule ulikuwa udhalilishaji. Unaweza ukaona upo kwenye jamii ya aina gani.
Fikiria ongezeko la single mothers ambapo ni matokeo ya ngono zembe na zinaa.
Unapinga Single mothers alafu upande wa pili wanaume wanajisifu kutia mimba wanawake hovyohovyo.
Jamii yetu inahitaji kubadilishwa kifikra ambapo ndio kazi kubwa kuliko kazi yoyote duniani.
Ni rahisi kubadilisha uchumi lakini ni ngumu sana kubadilisha fikra.
Kubadilisha mfumo wa utamaduni.
Watu kupambana na chanzo badala ya kupambana na matokeo.
Mimi nimemaliza.
TaikonMaster
Kwa sasa Kahama, Shinyanga