Lissu apunguze hasira na malipizi, atapendwa na wengi

Lakini pia hasira na mihemko kwenye kauli zake apunguze na atangulize uzalendo, hekima na busara

Tundu Lissu anawakilisha sauti za watanzania ambao kwa muda mrefu wa miaka 60 chini ya utawala wa chama kongwe dola CCM wamekuwa wakipuuzwa, kuonewa, kunyanyaswa kunyimwa haki zao za kikatiba .


Mpaka lini watanzania wakatazwe kuonesha hasira na kupaza sauti dhidi ya utawala huu mkongwe baada ya uhuru ambao umerithi haiba zote za mkoloni kabla ya uhuru na kuendelea kukandamiza raia

Mikutano ya CHADEMA inaonesha wazi watanzania wamechoka utawala huu mkongwe kandamizi na ndiyo maana watawala wa CCM wameingia hofu na kutaka kuweka picha potovu kuwa hadhira yote inayotokea ktk mikutano ya CHADEMA na maelfu wanaoifutilia mikutano hiyo yenye views nyingi YouTube n.k hawapo pamoja na CHADEMA kuonesha wamekerwa na yote yabayoendelea chini ya utawala gadamizi usiojali hali za kiuchumi, ajiri, demokrasia na haki za raia.
 
Hakuna machafuko yatakayotokezea.
Mungu ibariki Tanzania.
wewe utakua si mtanzania unaombea machafuko. utakua raia wa sudani au haiti
ccmu ndo wanaipeleka Tz huko , wewe unaeza omba uwezavyo lkn ukilala mlango waz utaibiwa tu
 
hakuna Tanganyika kuna Tanzania
 
anazidi kuthibitisha kuwa hafai kuwa kiongozi zaidi ya kuwa mlopokaji.

anajazwa misifa ya kejeli naye anavimba kichwa na kujiona yeye ndiye jasiri na bingwa kuliko mtu yeyote.
 
hakuna Tanganyika kuna Tanzania
Ila kuna Zanzibar ndani ya Tanzania.
anazidi kuthibitisha kuwa hafai kuwa kiongozi zaidi ya kuwa mlopokaji.

anajazwa misifa ya kejeli naye anavimba kichwa na kujiona yeye ndiye jasiri na bingwa kuliko mtu yeyote.
Tulieni dawa iwaingie mmezoea vya kunyonga sasa Lisu anawaumbua
 
10 May 2024

Sheikh Ponda Ahoji Namna ya Kero za Muungano Zinavyoshughulikiwa 'Tanganyika Haipo'


View: https://m.youtube.com/watch?v=iUdTVaGrm-c
Amesema hayo Sheikh Ponda kwenye Mkutano wa Kitaifa kutafakari na kujenga uelewa wa pamoja juu ya sheria za Uchaguzi zilizopitishwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa wa Mwaka 2024 na uchaguzi mkuu wa Mwaka 2025 ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania tarehe 9 Mei 2024
 
Tundu ana hoja ajibiwe kwa hoja ... tuache vijembe na ngonjera
 
Jibu hoja current za Lissu mkuu acha kujificha kwenye kivuli cha ubwana mdogo na ubwana mkubwa.

Licha ya wewe kuwa mkubwa kuliko Lissu kwenye rekodi za uwakili hujawahi kuwakilisha hata mtu mmoja mahakamani hata kwenye kesi ya wizi wa kuku.


Kiufupi wewe kwenye rekodi ya kesi ulizoshinda ni 0 , huku Lissu ameigaragaza serikali yako ya CCM kwenye kesi kibao kuanzia zama za Mkapa kwenye kesi za wachimbaji wa madini 1997 kule Tarime aliendelea kuwagagaraza hadi enzi za Kikwete na Dikteta mhutu kutoka Chato mlipompa kesi kibao za uchochezi.

Come again Pascal.
 
Baada ya Covid 19 sasa umeingia uhonjwa mwingine hatari "Lisu fever" yaani tayari umekumba 50% ya wa-TZ.
 
Acha ujinga fara
 
Mh Lissu amekuzidi kila kitu ,mifano; hajawahi kutakwa na wajumbe Kawe, amewahi kuwa President wa TZ law bar association, amewahi kushinda uchaguzi kama Rais wa TZ kwa huru na haki ....wewe ni opposite yote hapo juu ... wewe labda umemshinda umri na kujipendekeza tuu...ila samahani Kada.
 
Mkuu Matrix19 , naomba nikusaidie kuhusu wanasheria/mawakili, mtu kuwa wakili sio lazima ufanye litigations!. Law has so many field, na kwa taarifa yako, mawakili wa litigations are the poorest!. Sijawahi kwenda mahakamani hata siku moja!.

NB. Kwa wakili kwenda mahakama na kushinda kesi, hakumfanyi kuwa wakili bora, na wakili kutokwenda mahakamani, hakumfanyi kuwa sio wakili bora!. Umewahi kuwasikia mawakili madada wawili, Dr. Hawa Sinare na Mwanaidi Maajar? na Law firm yao ya Epitome?. Umewahi kuwasikia wakienda mahakamani kutetea kesi yoyote ya litigations?, they are among the richest!.

Kwa umri na kwa shule, mimi nimemtangulia TL, ila kwenye uwakili amenitangulia more than 10 ahead, na he is good kwenye kazi yake ya uwakili, na mimi ni mwandishi tuu wa habari na niko good kwenye kazi yangu. Naomba tembelea hapa, Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!
uone kuna a silly mistake Chadema walifanya, angalia aliyefanya kosa hilo ni nani?.

Japo ki umri nimemtangulia TL, lakini mimi kwake ni kama sisimizi mbele yake, wala sistahili hata kufunga gidamu ya kiatu chake!.
P
 
Naomba usinilinganishe na TL, kwasababu hatufanani, kuwa president wa bar, hata mimi naweza kuja kuwa!. Kule kugombea urais mimi ni miongoni mwa tuliomchagiza!, Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli! na kuna vitu vingi tuu tunamsaidia Nyaraka za Muungano: Tundu Lissu kutoishukuru JF na Pasco maana yake nini?

TL is good, but not in everything, and I'm bad, but not in everything!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…