..nadhani mnajichanganya mnapoyazungumzia majimbo ya Marekani ktk hoja hii.
..Marekani wao walianza na majimbo ambayo yalikwenda kuunda/kuzaa nchi.
..Tanzania tunaanza na nchi na tunakwenda kuunda majimbo. Kumbuka kwamba tayari tuna mikoa ambayo chimbuko lake ni majimbo.
..Sina uhakika kama Raisi wa Marekani anaweza kuigawa nchi yake na kuunda majimbo mapya.
..Raisi wa Tanzania atakuwa na uwezo wa kuunda majimbo, kama anavyofanya sasa hivi ktk mikoa.
..Pia sitegemei majimbo yatakayoundwa hapa Tanzania yatakuwa na mamlaka mapana kama yaliyonayo majimbo ya mataifa mengine kama Marekani, Nigeria, au Afrika Kusini.
..Mwisho, sote tunakubaliana kwamba serikali yetu ina madaraka makubwa mno. Sasa tuangalie ni madaraka yapi yanaweza kuondolewa toka serikali kuu na kupelekwa kwenye mamlaka nyingine kama majimbo[kama tutaamua kuyaunda], mikoa, majiji, au halmashauri.
From the outset that was what I have been implying kulikuwa na colonial states zikaamua kuungana kupambana na colonial master, huo muungano ukaleta nchi na hatimae federal constitution.
Kuhusu Tanzania hoja ya CDM ni kuunda majimbo ili local resources ziwasaidie zaidi wazawa wa maeneo.
Kama issue ni effectiveness ya serikali decentralisation iliyopo inatosha hata under a unitary state.
Tatizo la Tanzania lina sehemu mbili wanasiasa tia maji tia maji na kugeuza techinical position nafasi za kichama, especially under Magufuli it must be said. Lakini mfumo auna tatizo.
Kwanini wanasiasa tia maji tia maji ni tatizo. Ni vigumu kwa serikali kuu kujua local issues na priorities za mahitaji ya kila sehemu. Kupunguza central decision making kuna mfuko wa jimbo na baraza la madiwani. Hawa wana majukumu ya kutatua matatizo madogo madogo ya maeneo yao kutokana na local knowledge waliyonayo, wanapata hela kutoka kwenye vyanzo vyao, serikali kuu na mfuko wa jimbo. Sasa badala ya kushirikiana kutwa wanazozana kisiasa.
Pili technical position kupewa wanasiasa ukisikiliza malalamiko ya Jaffo kwenye ziara zake una pata picha watu wanaotakiwa ku manage strategies za central government ni wakuu wa wilaya na strategist wao ni wakurugenzi. Sasa katika hao unakuta mkuu wa wilaya hana system ya kujua nini kinafanyika kimefikia hatua gani na kwa kiwango kipi, mkurugenzi nae sijui katoa tender kwa kampuni gani ambao mradi sio value for money, au mkandarasi sijui aendi sambasamba na time ya mradi na hakuna penalties mkandarasi anazopewa. Ukisikiliza kwanini mradi umechelewa unakuta huyo mtu aliepewa tender hana resources za kufanya kazi aliyoomba, either capital au machinery etc with Tanzania nonsense.
Tatu wizarani hakuna system of performance bench marks (Quality Systems), periodic performance appraisal za kila wilaya kwa ujumla wake na individuals wanao ziongoza kutokana na majukumu waliyopewa and that is also the case kwenye serikali ya mkoa.
Wao huko juu wanachoangalia ni target za makusanyo tu kama wamevuka na kushangiliwa.
Otherwise the system is there tatizo ni watu wanaoendesha na kusimamia most are unqualified for the position nor having the experience to work at those positions.