Wasalaam wana jamvi
Leo Lissu kaendelea na kampeni lakini jambo la kushtua zaidi ni mpango wa CHADEMA wa kuigawa Tanzania kwa majimbo kwa kisingizio kuwa majimbo ndio chanzo cha maendeleo
Lissu ameendelea kusema kuwa nchi ikagawiwa kwa majimbo ndio watu watapata maendeleo na kila mtanzania atakula kwa urefu wa kamba zake.
Wasalaam wana jamvi
Akili ndogo ya MATAGA katika kuelewa mambo, wanafikiri sera ya kuigawa nchi katika utawala wa majimbo wandhani ni haya majimbo ya uchaguzi, majibo ya wabunge.
Ndio maana wengi wanadai ooh anataka kuigawa nchi vipande vipande, wanashindwa kuelewa kwamba mfumo tulionao sasa ndio imeigawa zaidi nchi kwenye vipande vidogovidogo.
Majimbo tunayozungumzia yanakuwa na eneo kubwa la utawala, kati ya mikoa 3 mpaka 4 hilo ni jimbo moja. Na zaidi sana lengo ni kugatua madaraka kwa kuwapa wananchi mamlaka zaidi juu ya utawala na maendeleo yao.
Tofauti na ilivyo sasa maendeleo ya Katavi eti yanapangwa na kuamuliwa Dodoma, halafu yanasimamiwa na watu kutoka Mtwara, Morogoro, au Tanga ambao hata hawaijui vizuri jiografia na utamaduni wa wana Katavi.
Mbaya zaidi hao wasimamizi hata wakifanya ufisadi wanakatavi hawana mamlaka ya kuwawajibisha, mpaka aliyewateua apende.
Mara ooh majimbo mengine hayana raslimali hivyo yatabaki kuwa masikini, huo ni uongo, maana kila sehemu kuna raslimali. Na hata kama hazitoshi, hapo ndipo Serikali kuu inakuwa na wajibu wa kusaidia hizo sehemu ziweze kupiga hatua ya kimaendeleo.
Ukiona watu wanapinga sera hii, ujue hofu yao imejengwa kwenye madaraka na si vinginevyo, na ni dhahiri madaraka ya kiutawala yanaenda kupungua, sasa wale tunaopenda madaraka makubwa hatuwezi kukubali kupunguziwa madaraka.
Vile vile kuna wale wanaovizia teuzi hawawezi kukubaliana na hii sera maana nafasi za uteuzi zinakuwa finyu kwenye mfumo huu.
Tusichoke tuendelee kuwaelimsha hawa ndugu zetu.