Lissu asema CHADEMA itaigawa Tanzania kwa Majimbo. Kila jimbo litakula kwa urefu wa kamba yake

Lissu asema CHADEMA itaigawa Tanzania kwa Majimbo. Kila jimbo litakula kwa urefu wa kamba yake

Selfish oriented policy...maana baada ya hapo kila mtu ataenda kwenye Kanda yke kufanya maendeleo..mwisho utaskia wachaga wote,mwanza, kahama ,dar na other places warudi kwao..wakinga nao the like.

Kutakuwa na wasomi nao watataka wafanye kazi kwenye Kanda/Jimbo lao and the story goes on..
Hauna uelewa wowote kuhusu mambo ya mifumo ya kiutawala. Huu mfumo wa Federation unatumika katika nchi nyingine bila matatizo yoyote.

Wewe inaonekana ukifundishwa unaweza ukaelewa huu mfumo unavyofanya kazi sambamba na faida zake kwa nchi.

Swala la ukabila halihusiani na na mfumo wa kiutawala. Nakumbuka Nigeria wakati ikiwa Unitary State ie kabla ya vita vya Biafra kulikuwa na ukabila wa kufa mtu na ndio hata ikapelekea wanapigana vita vya wenyewe kwa wenyewe, lakini walipoanzisha mfumo wa Federation hilo tatizo lilipungua mno.

Mataifa mengi yaliyopiga hatua kubwa kimaendeleo yanatumia mfumo huu pia inasaidia sana kudhibiti kiongozi kuwa dikteta.
 
Lissu ameendelea kusema kuwa nchi ikagawiwa kwa majimbo ndio watu watapata maendeleo na kila mtanzania atakula kwa urefu wa kamba zake.
Rudia tena. Mna masikio lakini hamsikii kinachozungumzwa. OMG
 
Mwenzenu Leo kule chato alikuwa hapigi kampeni alikuwa anafoka tu. Mwambieni asitufokee
IMG-20200915-WA0045.jpg
 
Kila mkoa uwe jimbo.. zanzibar majimbo mawili.. pemba na unguja..

Mkuu akisikia hii utashngaa anatangaza chato kuwa mkoa[emoji1][emoji1][emoji1]
Tunaunga mkono majimbo, mbona Kenya wameanzisha
 
Itasaidia kuwajibisha watendaji wabovu.. leo Rais anajadili ujenzi wa vyoo vya zahanati nyaishozi vijijiji.
Wazo zuri sana hili. Hakuna jimbo masikini kila mtu akijiamulia mambo yake ndipo tutaweza kuendelea.

Sio leo mtu kakurupuka tu huko anachukua hela za gas Mtwara anaenda kujenga International Airpot Kijijini kwake Chato ilihali huko kwa wenye gas hakuna hata barabara la lami.

Safi sana CHADEMA TUMAINI LA PEKEE LA WATANGANYIKA NA WAZANZIBAR
 
Kagera kama Paris
~naiona Arusha kama Carlifornia
~Mtwara kama Texas
~Kilimanjaro kama New York
~Dar kama Chicago
~na Zanzibar kama Jimbo la Hawaii kama laiti Lissu akishinda
~Tabora kama jimbo la Nevada
 
Eti sileti taa za barabarani kwa sababu hamjanichagua.. ujinga..
Labda mtashinda chato!! Serikali za majimbo ndo suluhisho la kweli la maendeleo ya uhakika. Sio sasaivi mnanyanyasa watu Eti hampeleki maendeleo sehemu za wapinzani wajinga nyie. Mmekaa kibaguzi tu!!
 
Ungeisikiliza hotuba yake yote huko Mufindi ungeelewa kwani alikuwa akihutubia anawauliza anaowahutubia kisha anatoa mifano, hakuwa anafoka kama bwana yule.
JF ni wazi kuna great thinkers wachache sana wengi wetu ni great sinkers, tunakosa critical thinking. Tunachukua pande kwanza halafu tunajifanya kufikiri. Kwa mtindo huu ndio maana tunaona International Airport Chato ni sawa (kwa uchumi gani basi) na serikali za Majimbo ni utopolo tunajifanya hatujui kuwa serikali za majimbo zinaendana na serikali kuu. Kwa akili hizi bado tunatetea serikali mbili badala ya serikali tatu.
 
Ndio hivyo mkuu hii ni sera ya chadema since day one Kama tu unavyoona muundo wa kiungozi wake uko kikanda,hata sasa huwa Kuna kanda ya ziwa,Kusini,kadiazini,nyanda za juu nk
Hii ni best system inatumiwa duniani kote ili kuleta ufanisi wa kiutendaji na kuondoka hodhi ya serikali kwenye baadhi ya mambo...
Hii staili itakomesha wale wanaotumia madaraka vibaya kwa kujipendelea kwao na kuwanyima wengine kwa kisingizio Cha kuchagua upinzani wakati kodi tunalipa wote tena ukute yetu ni nyingi.Raha ya hii system mkichagua kiongozi kiazi na mbulula Kama walivyo wale mbogamboga mtakula viazi.
 
..Mikoa tuliyonayo sasa hivi chimbuko lake ni Majimbo.

..Tuliachana na mfumo wa majimbo mwaka 1966.

..hapa chini ni jedwali la muundo wa majimbo na mikoa iliyotokana na majimbo hayo.

source: Wikizero - Mikoa ya Tanzania



Na.JimboIdadi ya WakaziEneo (km²)Makao makuuMikoa ya baadaye
1.Kati886,96294,301DodomaDodoma, Singida
2.Mashariki955,828107,630Dar es SalaamPwani (kisehemu), Morogoro
3.Dar es Salaam128,7421,393Dar es SalaamPwani (kisehemu)
4.Ziwani1,731,794107,711MwanzaMara, Mwanza, Shinyanga (kisehemu)
5.Ziwa Magharibi514,43128,388BukobaZiwa Magharibi
6.Kaskazini772,43485,374ArushaArusha, Kilimanjaro (kisehemu)
7.Kusini1,014,265143,027MtwaraMtwara, Ruvuma
8.Nyanda za Juu za Kusini1,030,269119,253MbeyaIringa, Mbeya (kisehemu)
9.Tanga688,29035,750TangaKilimanjaro (kisehemu), Tanga
10.Magharibi1,062,598203,068TaboraKigoma, Mbeya (kisehemu), Shinyanga (kisehemu), Tabora
11.Zanzibar165,2531,658ZanzibarZanzibar Shambani, Zanzibar Magharibi
12.Pemba133,858984Chake ChakePemba
Majimbo yote9,084,724928,537
 
Mwenye ilani ya uchaguzi ya chadema naomba anisaidie nipate kuipitia
 
Kwanza hata ulivyoandika tu, imeonyesha umerukia hoja kwa mihemko na hivyo huwezi kuielewa wala kuwaelewesha wengine! Kwa kifupi anachoongelea Lissu sio kitu kigeni katika muundo wa serikali, Bali ni kitu kinaitwa POWER DELEGATION, kwa lugha nyepesi ni ugatuaji wa madaraka wenye lengo kusogeza maamuzi karibu zaidi na wananchi wa eneo husika! Ikumbukwe hata wakati wa serikali ya awamu ya kwanza chini ya Baba wa Taifa Mwl. Nyerere, serikali ilikusanya wananchi na kuwatenga katika vijiji vya ujamaa ambapo kila eneo kulikuwa na uongozi na walifikishiwa huduma kulingana na mahitaji.

Pia mikoa, wilaya, kata na mitaa yote tunamoishi sasa ni matokeo ya mgawanyo kama huo.
Hivyo kuigawa TZ katika majimbo hakuna shida ni kurahisisha tu uharakishaji wa maendeleo ya eneo husika pamoja na kunufaika vema na rasilimali zinazowazunguka! Sio unakusanya kodi za majengo kule Tandahimba au Katavi alafu unapeleka kwenda kujenga Flyover Dar es salaam!

Kuna halmashauri nyingi tu zinakusanya pesa za kutosha kabisa lakini zinapelekwa mfuko mkuu wakati wananchi wa halmashauri hizo wanataabika, hawana huduma za maji, barabara ni mbovu, huduma za afya ni duni! Wanasikia tu viongozi wakishindana kupeleka miradi Chato, Huyu leo anasema atajenga hospitali kubwa ya rufaa ya kanda Chato, Mwingine hapohapo anaahidi kujenga uwanja wa kisasa wa mpira, huku majuzi tu pamejengwa uwanja wa ndege wa kimataifa, pamejengwa soko la la kisasa la madini, pamelekwa hifadhi ya taifa ! Je huku kwingine hakuna watanzania??

Infact Lissu yupo sahihi kabisa kuanzisha utaratibu wa majimbo! Huu ndio utaratibu unaotumiwa hata nchi zilizoendelea kama Marekani.

..umeielezea hii concept vizuri sana.

..binafsi napendelea tuwe na mfumo utakaowawezesha wananchi kuwa na maamuzi zaidi ktk mambo ya kiutawala.

..mfumo wetu wa utawala uko too centralized / top-down, ningependa halmashauri na wabunge wawe na sauti zaidi ktk maamuzi.

..siungi mkono serikali za majimbo, na siungi mkono mfumo wa sasa hivi. wasiwasi wangu ni kwamba serikali za majimbo zinaweza kuongeza gharama ktk uendeshaji wake.

..Mfumo ulioko sasa hivi una wakuu wa wilaya ambao naamini hawahitajiki. kwa hiyo niko interested na mfumo ambao ni "hybrid" ya majimbo, na mfumo tulionao sasa hivi.
 
Kazi ya serikali kuu imesha isha.. turudi kwenye majimbo/ mikoa..


Kwanza kutakua na ushindani mkubwa sana kimaendeleo.
..wakati wa utawala wa Muingereza Tanganyika ilikuwa imegawanywa ktk majimbo.

..baada ya Uhuru, nadhani mwaka 1962, majimbo yaligawanywa zaidi na kuunda mikoa.

..hata wakati tuna majimbo wananchi walikuwa wanaweza kwenda maeneo mbalimbali na kufanya kazi au kujitafutia riziki.

..au kama tunaogopa nchi kugawanyika mbona sasa hivi kuna mikoa?
 
Magufuli kaharibu sana nchi.
Kama yalivyotaka kujitenga majimbo ya nchi gani kwa sababu yaliona yanachangia sana?!

Hata usipoweka sera za majimbo, usipojenga haki miongoni mwa maeneo mbalimbali, bado watu watakuwa na hisia za kujitenga!!

Miaka kadhaa iliyopita, kulikuwa na mbunge mmoja Kusini mwa Tanzania ambae alizoelea umaarufu kwa kuitetea Kusini hadi akafikia kusema haya mambo yakiendelea "Mikoa ya Kusini Tutajitenga na mpaka utakuwa Mto Rufiji"!

Alisema hayo si kwa sababu aliamini kusini inazalisha sana bali kwa sababu aliamini kusini inatengwa sana kwenye mipango ya serikali!
 
Kuna revenue share kati ya majimbo na serikali kuu.

Mfano kama revenue ya singida ni tr 100 basi tr 60 zinabaki singida na tr 40 serikali kuu.
Na jeshi lako uliandika utali fund vipi?
Maswala ya National security kama TISS na tactical infrastructure nani alipie cost zake?
Who’s to be in control of the banking sector, monetary and fiscal policies, role of central bank?

Ebu tuelezee hiyo paper yako inasemaje kuhusu maeneo hayo? Uchumi wa jimbo uki collapse what your bailout plan and who’s to fund that.
 
Naona shule ya sheria imeanza kutukolea..[emoji1][emoji1]
Acha kukariri!

Unazungumzia Federal Law ipi wakati Tanzanai ni unitary government?!

Tangu kuanzishwa kwao CHADEMA wana sera ya majimbo! Which means, wakiingia madarakani wanaweza ku-opt sera ya majimbo na hatimae kuwa na federal government!

Wakifanya hivyo ina maana kutakuwa na federal constitution in place of unitary constitution!

So, it's all about Federal Constitution itasema nini about various issues including taxes, and tax income allocations, resource distribution, etc.
 
[emoji111]
Ukisikia Sera ya majimbo wenzako wanakwambia nchi wanaigawa alafu wewe unakubali tu kwa sababu wewe ni zuri. Katika dunia ya sasa hakuna sera makini katika kuchochea maendeleo ya kweli ya watu kama sera za majimbo kwa sababu inachchea maendeleo kila sehemu sio kama sasa nyie mnakusanya kodi kutoka kwa watanzania wote alafu mnagawa maendeleo kibaguzi hasa mkinyima maendeleo sehemu za wapinzani
 
Kenya tuu hapo wamesha fanikiwa na sasa mjadala mkubwa ni revenue share kati ya majimbo na serikali kuu
Kama unataka kusikia utekelezaji wake andaeni mdahalo mumuulize Lissu hayo maswali atakujibu. Unataka akwambie utekelezaji wale kwenye kampeni?

kwani kuna shida gani kwenye money supply tukitekeleza mfumo wa majimbo???? Kama sehemu zingine wamefanikiwa Kwa nini Tanzania tushindwe?

Kwani mfumo wa majimbo umefanikiwa Marekani tu? Mbona nchi nyingi duniani zinafanya huu mfumo na zinaendelea?
 
Hilo swali ilibidi ujiulize mwenyewe kwa sababu inaelekea kwamba umekariri a particular federal system na kisha kuona kwa CHADEMA haiwezekani kwa sababu unaangalia hiyo federal system unayoijua wewe!!

And you expected yote hayo hayaongee kwenye mikutano?!

Na nilishakuambia kabla kwamba endapo Lissu ataingia madarakani, na CHADEMA waka-opt kuendelea na lengo lao la Serikali za Majimbo, kuanzia hapo itabidi wabadili katiba itakayoendana na mfumo mpya wa utawala! It's not Tundu Lissu issue bali itakuwa suala la kitaifa!

Huwezi kuamka tu kivipi wakati tangu kuanzishwa kwake CHADEMA wanayo hiyo sera?!
Duh! We jamaa bhana!! Hivi hapa napo inabidi ukumbushwe kwamba hilo ni suala la kikatiba?!

Hivi suala la kikatiba ni suala mtu mmoja hadi useme nimekubali kwamba hayupo clear na itabidi asaidiwe?! Man, kwenye siasa unatoa chambo, ngoma ikikubali ndo mnakaa kuangalia mtafanya fanya vipi!
Kumbe nilikuwa right niliposema unavyofanya mambo kuwa magumu ni kama unachanganya kati ya Federation na Confederation!

Man, unachanganya madesa!!!

Serikali ya "US" ambayo ilipigana na British ni Confederation Government... anyway, kabla ya kuunda Confederation Govt through Articles of Confederation hizo states were just colonies!

Hadi US inapata uhuru through American Revolution War, bado walikuwa confederacy.

Lakini kama nilivyosema awali ku-run confederacy ni pasua kichwa, ndipo yakajitokeza yale unayohoji wewe... gharama ya hiki na kile, kile ata-fund nani, deni lile lilipwe na nani, and so on.

Hayo yalitokea wakati wa confederacy ambayo wewe unataka kuyafanya ni issue ya federal state!

Kufuatia huo ugumu, ndipo wakakutana tena wakati vita vimeshaisha kitambo... wakakutana through what's known Philadelphia Convention.

Lengo kuu la Philadelphia Convention ilikuwa ni kupitia Articles of Confederation kutokana na ugumu uliokuwa umejitokeza! Kwa bahati mzuri, wakapiga hatua kubwa zaidi na hatimae kuzalisha US Constitution under the federal government.
Hayo yalifanyika wakati wa transformation from Confederacy... kuna states zingine, hususani zile ndogo, zilitaka ziachiwe baadhi ya mamlaka!

Kama kumbukumbu zangu zipo sawa, walishindwa kwenye kura!!

Nani alikudanganya federal government inazuia civil war?! You seriously believe KE waliingia kwenye machafuko kwa sababu walikuwa na unitary system?

Au hapa tena ukumbushwe kwamba pamoja na back in 1789 (or close to that) US kuwa federal state lakini hiyo haikuzuia kutokea kwa Civil War in 1861 huku Lower Southern States zikitaka kurudisha confederation?! And if that's case, how come uamini KE wali-adapt Federal Governance kwa sababu ya machafuko yaliyokuwa yametokea?

All in all, ni kwamba yamenipita yanayoendelea East Africa, au? Ni lini Kenya imeachana na unitary system?! Au kwavile unaona US kuna Maseneta na Magavana, na Kenya hivi sasa kuna Maseneta na Magavana, ndo tayari unataka ku-conclude kwamba KE ni federal state?

Anyway, labda hili la Kenya limenipita, kwahiyo nimuombe ndugu yangu MK254 aje anitoe matongotongo!!

Why UK na Scotland ni KAMA federal tu?! Are they federal or not?!
Lakini bado unahoji hoja ya Tundu Lissu na kuona ni kitu ambacho ni KIGUMU KWELI KWELI na wakati huo huo unadai "...unachohitaju ku investigate what remains in the central control" You're very funny! Hivi unavyosema haiwezekani jambo la uchumi kuwa a state issue unamaanisha nini hasa?!
The problem ukiulizwa maswali huwa hujibu na badala yake unaleta hoja zingine! Kwa mfano nilikuuliza kuhusu nchi za Austria, Malaysia, UAE na zingine, wewe ukaniletea habari za Kenya!!!
Duh we jamaa inabidi ukasome upya vitabu vya US history. Ndugu in short kuna mambo mengi yalitokea leading to American revolution main instigators of the states rebellion were taxes put upon them from UK parliament which were deemed unreasonable.

Kama umesoma historia vizuri utaona kabla ya states kuungana ilikuwa moja iki rebel waingereza wanaenda kutembeza kichapo jamaa wanatia adabu na kurudi kwenye mstari. Ili kukabiliana na colonial master ikabidi waungane unofficially na baadae kuungana rasmi kwa katiba 1787 baada ya kushinda vita.

Huo muungano wa states wa awali ulikuwa wa kimaslahi dhidi ya colonial masters. Kwa ivyo kuna baadhi ya states walitaka some aspects of their autonomy kutokana na jinsi walivyokuwa wanafanya mambo kwao and that remains the foundation of US federal union to date.

Kuna muungano wa states halafu kuna muungano wa wafanyabiashara na wenyewe ulikuwa na watu kama kina Rockefeller, Rothschild, J.P Morgan na wengineo walioudhuria mkutano wa ‘Jekyll Island’ (ukitaka full story soma kitabu kinachoitwa ‘the creature from Jekyll Island’) matter of fact every economist should read that book and those people were unscrupulous characters; ndio waliotengeneza US capitalist system.

Kwa ivyo how US federal government operates is based on early reasons of uniting na uchumi wao upo based na misingi ya early entrepreneurs na hizo ndio siasa za US mpaka leo.

Ni hivi nchi zilizotawalia nyingi mpaka 20th century katiba zake zipo based on their colonial government. Wakati wao colonial masters katiba zao zina misingi yake na sababu zao maalum.

Ndio maana mnaulizwa mnalilia federal system how exactly would it work? Hamna majibu rasmi na kuanza kuleta hadithi za sijui nani na nani wanafanya nini, mara sijui porojo watu wataiba ideas zenu kha, etc with nonsense.

Ni hivi the whole idea from CDM/Lissu and yourself is based na kuona mambo yanavyofanyika nchi zingine bila ya kuelewa sababu zao.
 
Back
Top Bottom