Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Kuongoza chama kikuu cha Upinzani Nchini kama CHADEMA inahitaji moyo,inahitaji ujasiri,inahitaji kujitoa na kujitolea muda na rasilimali zako kwa ajili ya kukijenga chama wakati na muda wote.inahitaji uvumilivu wa hali ya juu sana.
Chama kinahitaji Kiongozi na viongozi wakuu wake kuwepo Nchini muda wote ili kuweza kushuka chini huko kukijenga na kukiimarisha chama.kuwepo na uwepo wao katika Operation mbalimbali inaleta morali, Ushawishi,nguvu na matumaini kwa viongozi wa chini pamoja na wanachama.inasaidia sana kukiamsha chama kilipolala na kukipa uhai.
Sasa huyu lissu anayetaka uenyekiti wa CHADEMA Taifa nafasi ambayo kiuhalisia haiwezi kuimudu ni vipi ataiongoza CHADEMA? Ni vipi ataijenga CHADEMA? Ni vipi atashirikiana na viongozi na wanachama kukisimika chama mioyoni mwa watu?
Ikumbukwe ya Kuwa lissu amekuwa akitumia muda mwingi kuzunguka ulaya na Marekani kuchafua na kuongea maneno yenye kuchafua taswira ya nchi yetu,kujijenga yeye binafsi,kutangaza nia zake za kugombea Urais na kutanua tu Maisha .
Akija Nchini anakuwa amekuja kwa maslahi yake binafsi au kutimiza matakwa ya wanaomtumia kwa mlango wa nyuma kutoa matamko yenye kuchochea chuki,ubaguzi na kuchafua watu. Akija Nchini ni kuomba michango binafsi kwa ajili yake mwenyewe.baada ya hapo huondoka kimya kimya na kwenda zake ulaya kuendelea na Maisha yake.
Sasa mtu wa namna hii chama kitapata wapi msaada wake wakati muda mwingi yupo angani na ulaya?atakitumikia chama muda gani? Atajua vipi uhai wa chama na maendeleo yake? Atakiandaa chama muda gani kushiriki uchaguzi na chaguzi mbalimbali? Si mliona hapo majuzi tu ameshindwa hata kujiandikisha kupiga kura? Sasa mnafikiri kwa sasa ndio atapata muda wa kuitumikia CHADEMA?
Anachotaka na atakachokifanya lissu ni kuitumia CHADEMA kwa maslahi yake binafsi na kujineemesha yeye binafsi.ataitumia CHADEMA kutolea matamko yake ya kichochezi na kibaguzi kuligawa Taifa letu na watanzania kwa ujumla wake.ataitumia CHADEMA kuchochea machafuko na na vurugu tu hapa Nchini.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.