Pre GE2025 Lissu ataka Ukomo wa Madaraka kwenye nafasi za uongozi CHADEMA. Asema itapunguza 'Uchawa'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wewe mzee wa kyela ni noma sana , itabidi uchukue jimbo umeiva mkuu
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Tundu Lissu, akizungumza na wanahabari Alhamisi, Desemba 12, 2024, Mlimani City, Dar es Salaam, amesema kwamba ukomo wa madaraka utapunguza upambe na uchawa unaojitokeza pale viongozi wanaposhikilia madaraka kwa muda mrefu katika mazingira yasiyokuwa na ukomo wa madaraka.

Lissu alikumbuka kauli ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyowahi kusema: “Kila nilipokuwa nikitaka kung’atuka walikuwa wakiniambia: ‘Mwalimu endelea tu, hii nchi ni changa na umeitoa mbali. Nchi hii haitaendelea bila wewe.’ Nami niliendelea hadi pale nilipokuja kugundua kumbe nchi changa waliyoiongelea ni familia zao, na hazitaendelea bila mimi kuwepo madarakani, maana walikuwa hawana uhakika kama Rais ajaye atawaacha katika nafasi walizokuwa nazo.”

Lissu pia alieleza azma yake ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa, akisema uamuzi huu ulitokana na hali ya kisiasa ya sasa na kuhitaji uongozi mpya ndani ya chama hicho.
Your browser is not able to display this video.
 
Afadhali leo ndio TL amelizungumzia hili, anashangiliwa, kama hakuna ukomo, then hakuna kung'ang'ania madaraka,hili neno kung'ang'ania madaraka ni kumsema mtu kwa mlango wa nyuma!。

Msikilize TL hapa Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA

Siku nilipoibua hii issue ya ukomo wa madaraka, KM wa wakati huo, Dr Slaa, aliruka kimanga na kuniparua Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Haya sasa leo TL kayasema, nasubiria kama ataparuliwa!。
P
 
Msigwa atajuta kusaliti Chadema!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…