Mbali na sifa zote alizo nazo Tundu Lissu, tukubaliane kwamba, kuna kitu mhimu kinapungua kwake, na kwa hicho, ndicho kinachosumbua vichwa vya wasomi wenzake wanaoona mbali kumwamini kupewa nafasi mhimu kama hiyo
Nimepitia maoni mbali mbali ya wachambuzi mahiri wa siasa katika nchi yetu na waandishi manguli katika nchi yetu, baada tu ya Makamo Mwenyeki wa chama kikuu cha upinzani nchini (CHADEMA) kutangaza hadharani na mbele ya makamera na waandishi wa habari wa ndani na nje kwamba, anahitaji kugombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa katika chama alichopo
Baada ya kupitia maoni mbalimbali kumhusu yeye, nahitimisha kusema kwamba, Mh Tundu lissu, hafai kuaminiwa na wanachi katika nafasi ya Urais
Nafasi ambayo, inahitaji watu watulivu, waliojaa hekima na maamzi yasiyo ya kukurupuka, nafasi ambayo kwa neno moja tu la mkuu wa nchi, linaweeza kuhatarisha usalama wa nchi na wananchi
Kama yeye Mh Tundu lissu, hapati kuaminiwa kwenye nafasi ndogo tu ya kuongoza chama chenye wanachama wanaosadikiwa kufika 12M, tumwamini vipi katika nafasi ya kuongoza taifa lenye zaidi ya watu milion 70?
Nashauri, ili Mh Lissu aaminiwe katika nafasi ya Urais, ni bora aaminiwe kwanza kwenye chama chake!
Mh Tundu lisu ni JPM aliyechangamka aishie kwenye nafasi aliyopo na akienda sana, aishie kwenye kuongoza Wizara tu