Pre GE2025 Lissu ataka Ukomo wa Madaraka kwenye nafasi za uongozi CHADEMA. Asema itapunguza 'Uchawa'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Unaifadhili chadema kwenye nyanja gani kama ni pesa si wanapokea ruzuku za kutosha?
Ruzuku? Ungehoji ccm inayochukua fedha nyingi za ruzuku zaidi ya mara 10 mbona inasaidiwa na watu individual?
Kuendesha chama ni gharama sana na ndio maana wenye mapenzi mema wanavichangia
 
Ruzuku? Ungehoji ccm inayochukua fedha nyingi za ruzuku zaidi ya mara 10 mbona inasaidiwa na watu individual?
Kuendesha chama ni gharama sana na ndio maana wenye mapenzi mema wanavichangia
Mpaka umafia wa kusanehe kodi kwa wafanyabiashara unatumika ili ipate pesa kwa mlango wa nyuma.
 
Hapa lazima kuna vikao na mbuzi kachinjwa kujadili namna ya kuokoa chama unaachaje chama bwashee
 
Hii prediction nimeipata kwa kusoma kitabu

A Handbook of Cartomancy
Fortune - Telling and Occult Divination by

Grand Orient.( Of London)

George Redway 1891.

Hawa Grand Orient ndio muungano wa Freemasons na Illuminati na all Occult organizations uliofanyika London 300 years ago
 
Mbali na sifa zote alizo nazo Tundu Lissu, tukubaliane kwamba, kuna kitu mhimu kinapungua kwake, na kwa hicho, ndicho kinachosumbua vichwa vya wasomi wenzake wanaoona mbali kumwamini kupewa nafasi mhimu kama hiyo

Nimepitia maoni mbali mbali ya wachambuzi mahiri wa siasa katika nchi yetu na waandishi manguli katika nchi yetu, baada tu ya Makamo Mwenyeki wa chama kikuu cha upinzani nchini (CHADEMA) kutangaza hadharani na mbele ya makamera na waandishi wa habari wa ndani na nje kwamba, anahitaji kugombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa katika chama alichopo


Baada ya kupitia maoni mbalimbali kumhusu yeye, nahitimisha kusema kwamba, Mh Tundu lissu, hafai kuaminiwa na wanachi katika nafasi ya Urais

Nafasi ambayo, inahitaji watu watulivu, waliojaa hekima na maamzi yasiyo ya kukurupuka, nafasi ambayo kwa neno moja tu la mkuu wa nchi, linaweeza kuhatarisha usalama wa nchi na wananchi

Kama yeye Mh Tundu lissu, hapati kuaminiwa kwenye nafasi ndogo tu ya kuongoza chama chenye wanachama wanaosadikiwa kufika 12M, tumwamini vipi katika nafasi ya kuongoza taifa lenye zaidi ya watu milion 70?

Nashauri, ili Mh Lissu aaminiwe katika nafasi ya Urais, ni bora aaminiwe kwanza kwenye chama chake!

Mh Tundu lisu ni JPM aliyechangamka aishie kwenye nafasi aliyopo na akienda sana, aishie kwenye kuongoza Wizara tu
 
Kelele nyingi bila utulivu, ni kukosa sifa ya kuwa kiongozi bora
 
Lisu hafai kuwa kiongozi mkuu wa jumuiko lolote, iwe chama cha siasa, nchi, etc. Hana charisma wala hekima ya uongozi. Chadema wakimpa uenyekiti chama kitakufa.
 
Kuna shuuma nzito dhidi ya Lisu zimeandikwa na Yericko Nyerere ambazo Lisu anapaswa kutoka hadharani na kuzitolea ufafanuzi ama aombe radhi.
1. Kusema kuwa hajalipwa hela yake ya matibabu kumbe kalipwa.
2. Madai kuwa Abdul alienda nyumbani kwake kumhonga wakati kumbe alikuwa anamsaidia kufanikisha malipo ya matibabu yake.
3. Kupewa nafasi kubwa ktk chama lkn hazitendei haki

Lisu anapaswa kutoka hadharani na kujisafiaha ama kuomba radhi.
 
Ni mjanja mjanja sana Lissu
 
Mnahangaika sana..... Tundu Lissu ni next level.
Siasa za MBOWE zime prove failure, hazina matokeo chanya
 
Lisu hafai kuwa kiongozi mkuu wa jumuiko lolote, iwe chama cha siasa, nchi, etc. Hana charisma wala hekima ya uongozi. Chadema wakimpa uenyekiti chama kitakufa.
kweli dunia ina maajabu yake yaani TL asifae ila ....afae duuuh
 
Kwa hiyo hizi tuhuma chadema walikuwa wanazijua ila wakazimezea mpaka alipotangaza kugombea uenyekiti? Ama kweli hiyo nafaasi ina mengi.
 
kweli dunia ina maajabu yake yaani TL asifae ila ....afae duuuh
Mtu akitaka kugombea wenyekiti basi hapo kwao hafai tena, wataanza kumwita msaliti, anatumiwa, na shutuma nyingi wakati wamekuwa naye miaka yote hiyo.
Mtu ambaye atakuwa anacheka sana ni zitto. Maana wote waliokuwa mstali wa mbele kumsema nao sasa wameanza kuonja joto lile lile. Amini vijana wa chadema hapa watampa tundu lissu shutuma zile zile anazopewa zitto.
 
Wakifanya hivyo hakuna tena atakayewaamini Chadema.

Wataonekana wao na CCM ni walewale!
 
Ni mjanja mjanja sana Lissu
Lissu sio mjanja kivile ni Trump type politician.Anayetafuta sympathy.
Lakini Lissu amekuwa Mbunge,Amekuwa Mwenyekiti wa Tanganyika Lawyer's Society,Amegombea urais wa Tanzania na Magufuli.
Sijaona jambo alilofanya extraordinary. Nadhani ni illution ya MAKE TANZANIA GREAT AGAIN

No plans ni kelele tu.
 
Trump unamchukulia poa? Ndiyo hivyo wamarekani wanamwelewa sasa.
Haya mmeyajua baada ya kusema anagombea nafasi ya kuwa mwenyekiti au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…