Nafikiri Bw. Tundu Lissu, CHADEMA, pamoja na wanachama wengine wa vyama vya Siasa hususani wapinzani kwa sasa hivi wajikite zaidi Kupigania upatikanaji wa Katiba Mpya itakayokuwa nzuri. Waachane na haya mambo ya kutaka kugombea vyeo, wafikirie suala la kubadilishwa kwa Katiba ya nchi kwanza ndipo masuala mengine yafuatie.
Tundu Lissu anataka kugombea Urais kwa kupitia kwenye Katiba ipi ambayo anafikiri kwamba atatangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi endapo kama atapata kura nyingi zaidi? Kwa sababu Katiba iliyopo hivi sasa hairuhusu jambo hili kufanyika. TAL Atakuwa anajisumbua nafsi yake bure na kupoteza wakati wake na rasilimali zake bure kabisa. Kwa Katiba hii iliyopo hapa Tanzania hata kama atapata Kura kwa Asilimia 99 ya Kura zote kabisa za Wagombea wa Kiti Cha Urais, KAMWE hataweza kutangazwa kuwa ni Mshindi wa Uchaguzi kwa kiti Cha Urais. Badala yake Mgombea wa CCM ndiye atakayetangazwa kuwa ni Mshindi.