Pre GE2025 Lissu athibitisha kuandika barua ya kugombea Urais, asema CCM wameweka fedha katika Akaunti yake, tatizo liko wapi?

Pre GE2025 Lissu athibitisha kuandika barua ya kugombea Urais, asema CCM wameweka fedha katika Akaunti yake, tatizo liko wapi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hitaji la sasa ni Katiba mpya na kufanya kura ya maamuzi kuhusu muundo wa Muungano. Lissu kujinadi sasa kugombea kiti cha urais ni uthibitisho wa uchu wa madaraka ya kushika Dola wakati akijua kuwa nchi imejengwa kwenye misingi mibovu ambayo tiba yake ni kuwa na Katiba mpya.

Nawashauri wapinzani wote wasikubali kushiriki uchaguzi mkuu wa 2025 bila kuwa na Katiba mpya maana hata akishinda yeye Lissu bado tutamdai Katiba mpya.
Huu uchaguzi wa Serikali za mitaa wanaweza kushiriki ili kupata watendaji lakini uchaguzi mkuu hapana!.

Samia na chama chake cha CCM aendelee hadi 2030 wakati tukishughulikia Katiba mpya na referendum.... Hiyo ndio njia sahihi ya kufuata.
Unataka Tumsusie mlevi gongo???
 
Nafikiri Bw. Tundu Lissu, CHADEMA, pamoja na wanachama wengine wa vyama vya Siasa hususani wapinzani kwa sasa hivi wajikite zaidi Kupigania upatikanaji wa Katiba Mpya itakayokuwa nzuri. Waachane na haya mambo ya kutaka kugombea vyeo, wafikirie suala la kubadilishwa kwa Katiba ya nchi kwanza ndipo masuala mengine yafuatie.

Tundu Lissu anataka kugombea Urais kwa kupitia kwenye Katiba ipi ambayo anafikiri kwamba atatangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi endapo kama atapata kura nyingi zaidi? Kwa sababu Katiba iliyopo hivi sasa hairuhusu jambo hili kufanyika. TAL Atakuwa anajisumbua nafsi yake bure na kupoteza wakati wake na rasilimali zake bure kabisa. Kwa Katiba hii iliyopo hapa Tanzania hata kama atapata Kura kwa Asilimia 99 ya Kura zote kabisa za Wagombea wa Kiti Cha Urais, KAMWE hataweza kutangazwa kuwa ni Mshindi wa Uchaguzi kwa kiti Cha Urais. Badala yake Mgombea wa CCM ndiye atakayetangazwa kuwa ni Mshindi.
Wewe unafikiri CCM itakubali mchakato wa Katiba mpya? Kwamba CCM wakubali mabadiliko?
Issue ni kwamba kama WaTz hamtaki kujiletea mabadiliko basi msihangaike kujisemesha katiba mpya wala nini.
 
Tundu Lissu will die one day a frustrated man but not as a former president of Tanzania.

Nahakikisha Tundu hawezi kuwa Rais. Wanaopata uRais wa Tanzania siyo wa haiba kama ya kwake au wanaopania kwa udi na uvumba kuwa maRais wa Tz.

Yeye amepewa nafasi ya pili ya kuishi baada ya Magufuli na Makinda kutaka kumuua, amshukuru Mungu tu. Ila Urais kwake ni maji marefu
Noted!; Nitakukumbusha a day Tundu Lisu AKIWA Rais!
 
Wewe unafikiri CCM itakubali mchakato wa Katiba mpya? Kwamba CCM wakubali mabadiliko?
"The right cannot be given as a gift by the oppressor, it must be demanded by the oppressed."

By Martin Luther King Jr.


Aidha, "Njia pekee ambayo Wananchi wataitumia katika kuzungumza au kujadiliana na Watawala wao ambao ni madikteta ili kufikia muafaka wenye maslahi kwa pande zote mbili ni kwa kupitia Mtutu wa Bunduki."

Jeff's O'Brien.
 
Lissu anataka kugombea ili ashindane kwenye Urais, au kiu yake ni kugombea pekee?
 
Noted!; Nitakukumbusha a day Tundu Lisu AKIWA Rais!
Haiwezi kutokea, niko hapa hapa toka Serikali ya Nyerere na sasa ni mstaafu. Ukisemwa sana, ukiutaka sana urais wa Tz huwezi kuupata. Anaupata usiyemtarajia
 
Wana haki ya kumlipa maana wai ndio waliharibu gari
 
Sijaona kosa la Lissu! Alichofanya ni kutangaza nia ya kugombea Urais.
Yuko sahihi kabisa! Na sidhani kama kuna kipengele cha Katiba hii mbovu tuliyonayo kama inamkataza raia wa Tanzania kutangaza nia ya kugombea Urais.
 
Back
Top Bottom