What if mwandishi alitaka TL mwenyewe atamkie/awathibitishie Wakenya kuwa amevuliwa ubunge?
Everybody in the world knows Tundu Lissu sio mbunge tena, Wakenya sio wajinga. Kama ni lazima Tundu Lissu "... awatamkie mwenyewe... athibitishe" basi asingemu introduce kama mbunge aliyefukuzwa.
Total waste of time!
Ndio maana Benjamin Mkapa kasema wakienda BBC wanatemeshwa nyongo na "maswali ya kushambulia" !
There were a hundred million questions to bombard him with:
Unaongeleaje kugombea Urais unaishi ukimbizini?
Nani atakuhakikishia usalama wako, polisi na vyombo vilivyotaka kukuua au mashirika ya nje ya haki za binadamu?
Au tukuulize, nani unadhani alitaka kukuua, na nani atakulinda?
Unasema ubunge wa upinzani unapatikana kwa madhila, vipigo, jasho na damu, do you take responsibility kwa uzembe wa kutozingatia technical requirements za kumfahamisha speaker kwa maandishi kwa nini hurudi, hata kama ni figisu za dhuluma za CCM?
Magufuli anasema kajenga kilomita nyingi za lami in four years than four presidents in 50 years combined, unamkubali or why not?
Civic elections mlizosusia umesema ni uhuni wa CCM, kwa nini mnashindwa vijitu technical vidogo vidogo kama kufunzana paperwork requirements za kujaza fomu za uchaguzi mpaka 95% mnaenguliwa? Again, hata kama ni figisu za dhuluma za CCM. Mnajua CCM walifanya semina za kujaza fomu?
Ukiwa Washington DC umemshutumu Magufuli hajui Kiingereza, sisi ni Waingereza?
Mara ngapi unatuambia ukipona unarudi, ukipona unarudi, mpaka tarehe unapanga, nini kipya kimetokea ghafla kukufanya ujue usalama hakuna, vitisho vya Musiba?
Ukiwa Uingereza umeshutumiwa kwa kutetea haki za mashoga, toa ufafanuzi, ulitetea mashoga hukutetea mashoga, nyosha maelezo!
Incumbent president Magufuli anasema Nyerere, Mwinyi, JK na Mkapa wamejenga hospitali za wilaya 77 in 60 years, yeye peke yake kajenga 67 in four years, zitakuwa mbili kila wilaya, kwa nini humkubali???
Akijibu tatizo demokrasia unamwambia kwa nini hakuna demokrasia CHADEMA, uchaguzi especially wa mwenyekiti hakuna, mpaka Sumaye kasema demokrasia hakuna CHADEMA, mtabadilika lini?