sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 3,344
- 9,066
Uongozi ni kalama na zawadi hii anaigawa mwenyezi Mungu pekee.
Lissu alitumia nguvu, matusi, kejeli, dhiaka na kila aina ya uchafu ili awe mwenyekiti wa Chadema.
Alipata alichokitaka.
Amekuwa mwenyekiti ila hakuna jipya analofanya. Tuliambiwa tumpe muda anaenda chimbo akirudi nchi itasimama.
Naomba niongelee press yake ya jana ambayo matarajio yalikuwa makubwa sana kwa wafuasi wake lakini amewaangusha mno hawakupata walichotegemea.
Jana ilikuwa iwe siku ya kimkakati ya kuonesha uelekeo wa uongozi wa Lissu katika miaka yake mitano, alitakiwa aoneshe energy, aoneshe dira na mikakati inayoeleweka kwa wafuasi wake.
Matokeo yake.
Mwenyekiti anafanya exclusive press conference na makamu mwenyekiti nae anafanya exclusive yake mkoani. Watu hawajui wamsikilize nani. Press ikakosa mvuto hakuna anaeangaika kuijadili.
Ujumbe waliokuwa wanauleta kwa watanzania haieleweki wanachotaka ni nini.
No reform no election ni kama fumbo la imani. Uku wanasema hakutakuwa na uchaguzi kama hakuna reform hapo hapo wanasema hawajasusia uchaguzi. Wao wenyewe hawajui nini haswa wanataka kukifanya. Na wafuasi wao kila mtu ana tafsiri yake ya no reform no election. Sijawai kuona duniani slogan ya kisiasa inabidi ukae chini ueleweshwe ndio uielewe.
Kitengo cha communication kina mengi ya kujifunza bado, Lissu alitakiwa akutane na wanahabari awape nguvu ya kuchukua matangazo wenyewe ili wayaweke kwenye media zao lakini mfumo uliotumika ni kama wanatoa habari za msiba wa kitaifa.
Mapema tu mmeanza habari za kutembeza bakuli, labda kama amuwajui watanzania kwenye michango 😂😂
Ni wazi Chadema is too big for Lissu and Heche. Wakae chini na watu wenye hekma za uongozi na uzoefu wafundishwe kuongoza. Watanzania wanawatazama if mnaweza kuongoza au ni wapiga kelele wazuri. Na wameanza kuwapuuza sababu hawaelewi nini mnachofanya.