Blackcornshman
JF-Expert Member
- Aug 25, 2016
- 6,514
- 15,701
Hasa yale mabulungutu ya madafu hata wobongoflava wanagawaga...biashara yake ilikuwa Uraisi wa Tz.
..hivi mmesahau mabulungutu ya pesa aliyokuwa akitembea nayo na kuyagawa alivyokuwa akijisikia?
..sasa kuna ajabu gani mtu wa aina hiyo kukutwa amejaza mapesa nyumbani kwake?
..wasiwasi wangu uko ktk kiwango cha fedha inachodaiwa zilikuwa nyumbani.
..lakini sishangazwi na madai kwamba kuna fedha, tena nyingi, zilikutwa nyumbani kwa Magufuli, IKULU.
Kama wana guts wapeleke kesi mahakamani😅😅Kusema ukweli kuhusu mtu ndo kum attack character yake?
Tundu Lissu alidanganya kuhusu huyo mlinzi wa Magufuli. Nimeweka ushahidi wa video na picha.
Unasema nimemu attack character badala ya kuchambua kesi aliyoileta.
Seriously?? Tundu Lissu hapa kaleta kesi gani zaidi ya hearsay?
Sikliza/ angalia tena hiyo clip. Lissu mwenyewe anasema kwamba “Naambiwa amekutwa na pesa za kigeni dola za Kimarekani milioni 42 nyumbani kwake baada ya kufa”
Hiyo ni nukuu.
Umezungumzia textbook definition, siyo? Basi hicho alichokidai Tundu Lissu hapo ni hearsay.
Hajatoa ushahidi wowote ile. Kasema kaambiwa kuwa Magufuli alikutwa na hizo hela.
Kama kuna mtu anayechafua character ya mwenzake hapa basi ni Tundu Lissu anayedai Magufuli alikuwa ameiba dola milioni 42, bila ushahidi wowote ule.
Mimi kuutaja uongo wa Lissu ambao uko documented si character assasination.
Tundu Lissu lied then and he might be lying now as well.
Yeye kaambiwa tu halafu anapanda jukwaani anasema Magufuli alikutwa na mahela nyumbani kwake.
Ushahidi wake uko wapi?
Wezi watupuUnajua JPM alitaka viongozi imara, kulinganisha na huyu mama ni mbingu na ardhi.
Bashiru, Polepile, Kalemani, Lukuvi, Kabudi, Hussein Mwinyi
Magufuli kusachiwa siyo ajabu hakuwa mtanzania wa kawaida kama unavosema alikuwa Rais wa nchi hivyo serikali inaamini alikuwa ana mambo mengi anayajua hivyo kusachiwa nyumbani kwake siyo ajabu. Na je tunajuaje labda mama janeth ndio alisema huko serikalini kwamba njoeni kuna hela nyingi zipo chumba fulani na marehemu hakuwa mfanyabiashara You never know. LISSU ASIPUUZWE ANA HOJA NA ASIKILIZWE.Kwamba Tundu Antipas Lisu anatuambia baada ya kufa Nyumba ya Shujaa Magufuli ikasachiwa na fedha hizo zikakutwa?
Kwanini alisachiwa kama ndivyo?
Tundu Antipas Lisu ana habari gani kwa Watanzania ambazo hawazijui? Tamaduni za misiba ya kitanzania zinajulikana mambo ya kusachiana hayapo
Niishie hapo
Mlale Unono [emoji3]
Haya kachukueni mle.Hizo pesa ninaweza kula Mimi na familia yangu yote mpaka tunakufa bila kufanya kazi yeyote ....
Ina maana baada ya magu kufariki,kuna walioenda nyumbani kwake kupekua?
Akiongea na wananchi wa Bugarama Halmashauri ya Geita Vijijini, Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Antipas Lissu leo Jumamosi ya Agosti 5, 2023 amesema kuwa, aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Magufuli baada ya kufariki kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 42 (zaidi ya Tsh. Bilioni 100), zilikutwa nyumbani kwake Chato.
Kiasi hicho cha fedha ni nyingi hasa ukilinganisha na mshahara wa Rais. Lissu aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, wakati akiwasilisha mada ya uuzwaji na uwekezaji wa bandari.
Lengo la kuweka habari hii hapa ni mshtuko nilioupata.
Lissu siyo wa kumuamini anazunguka kuwadanganya wananchi kuwa Rais samia kauza bandari kwa waarabu kumbe uwongo mtupu. Lissu anawapeleka watanzania mputamputa.huyu ndo aliyetaka kwenda kumuamsha magufuli?sijawah kumuamini lisu
Nilimshuhudia Lissu anapelekewa moto...unahitaji ushahidi wa namna gani kuamini hilo.Ushahidi wa aina gani unautaka?
Si mlishawawekea Kinga wasishitakiwe wakiwa hai na wakifa.
Hata wengine walisema china, wengine canada, wengine malaysia..na huyu kasema nyumbani..kwa hiyo yeyote anaweza sema awazavyo.Mwandishi Luqman Maloto alishawahi kuandika kuhusu hii ishu ila hakutaja kiasi.
Waliomuamini JPM hawawezi kumuamini Lissu..na waliomuamini Lissu hawawezi kumuamini JPM..ndio maana kila mtu alipata kura zake.Nadhani wengi walimwamini sana Jpm kumbe naye alikua mlaji mbinafsi
Kwani hizi anazotoa samia kwenye magoli ya simba na yanga mpaka tunaambiwa na msigwa mama kasema pesa zipo nyingi tu anazitoa wapi??..binafsi najiuliza mabulungutu ya pesa aliyokuwa akitembea nayo Magufuli yalikwenda wapi baada ya kufa? Nani aliyachukua? Alikuwa anayaweka wapi?
Kwahiyo tukubaliane hoja ya Lissu kusema Rais samia kagawa bandari bure kwa waarabu ni ya uwongo?Waliomuamini JPM hawawezi kumuamini Lissu..na waliomuamini Lissu hawawezi kumuamini JPM..ndio maana kila mtu alipata kura zake.
Mmoja ni kiongozi aliyetenda kwa vitendo, mwingine ni kiongozi wa maneno..pia usisahau hata watangazaji wana mashabiki na wachezaji wana mashabiki..ila utajua yupi ana mashabiki zaidi.
Sio wavuvi tu..kama eneo serikali imezuua kuingia na wewe ukaingia basi unachukuliwa kama jangili..nenda kawinde kwenye hifadhi za taifa uone kama utachekewa na askari wa game.Raia wengi (wavuvi) walipoteza maisha yao huko, JPM alikua MHALIFU sana
Wavuvi(majangili) wazidi kuuawa hifadhi ya kisiwa cha Rubondo
Hili si jambo la kuficha. Yapata aidha kipindi cha miezi minne sasa wavuvi wanaoingia kwenye hifadhi ya Rubondo kwa kujipatia kitoweo wanapigwa risasi na kupoteza maisha kila kukicha. Sehemu hizi zinazokizunguka kisiwa hiki cha Rubondo ambazo ni: Izumacheli, Maisome, Ikuza na Mganza, Sasa...www.jamiiforums.com
Somo ninalolipata kutokana na makala hii ni kwamba Tanzania haijawahi kuwa na chama cha upinzani,
Akiongea na wananchi wa Bugarama Halmashauri ya Geita Vijijini, Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Antipas Lissu leo Jumamosi ya Agosti 5, 2023 amesema kuwa, aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Magufuli baada ya kufariki kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 42 (zaidi ya Tsh. Bilioni 100), zilikutwa nyumbani kwake Chato.
Kiasi hicho cha fedha ni nyingi hasa ukilinganisha na mshahara wa Rais. Lissu aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, wakati akiwasilisha mada ya uuzwaji na uwekezaji wa bandari.
Lengo la kuweka habari hii hapa ni mshtuko nilioupata.
Tundu Lissu haaminiki anatangaza kuwa Rais Samia anagawa bandari bure kwa waarabu kumbe uwongo mtupu. Lissu anawapeleka watanzania mputamputa.Somo ninalolipata kutokana na makala hii ni kwamba Tanzania haijawahi kuwa na chama cha upinzani,
bali kuna vyama vya upinzani pandikizi. Kwa kusema hivyo
nijitetee kwa kusema,Kitendo cha dokta sulaa alichotufanyia 2015 akisaidiana na porofesa wa buguruni
mimi kama mfuasi wa upinzani miaka hiyo kilinipa fundisho kwamba
viongozi wa upinzani ni mapandikizi wa chama kijani wanapoona dalili za upinzani kuingia ikulu,wanapiga hatua moja nyuma kwa kuanzisha mtafaruku baina yao ili wasishike dola.
Sasa hii hoja aliyoiibua TL kwangu naona ni mwendelezo huo huo,wa kutufanya wajinga.
Tujifanye anachokisema ni kweli,niulize swali,je huu ni wakati sahihi kuingiza hoja hiyo
kipindi hiki cha kukomboa bandari zetu na kupigania katiba mpya?
Ninachoshukuru,binafsi baada ya kuona ubabaishaji huu mkubwa
nimeamua kuisaka kadi ya chama tawala,ili mdogo mdogo
hata nigombee ujumbe wa shina,kwa kufanya hivyo nitawatendea haki
wanashina langu nitakalokuwa naongoza.
Kwani hizi anazotoa samia kwenye magoli ya simba na yanga mpaka tunaambiwa na msigwa mama kasema pesa zipo nyingi tu anazitoa wapi??
Hasa yale mabulungutu ya madafu hata wobongoflava wanagawaga.
Ukiwa Rais unakua Mali ya state, ndio maana mjane wake anaendelea kulipwa 80% ya salary ya sitting president, anapewa magari, wapishi, wasaidizi na atajengewa nyumba. Hata kaburi lake linalindwa na askari wetu. Baada ya kifo lazima vijana wapite kukusanya documents za office zikahifadhiwe.Kiasi chote hicho cha pesa kilikutwa nyumbani kwa Magufuli, ina maana alikiweka kwa siri hata mke wake na wengine wa familia yake hawakujua?
Ina maana baada ya msiba wa Magufuli kutokea, kuna watu waliokwenda nyumbani kwake, wasio wanafamilia waliopekuwa nyumba yake na kukuta kiasi hicho cha pesa?
Kama jibu ni ndio, kuna watu waliingia nyumbani kwa Magufuli na kupekuwa, tujiulize; hawa walifanya upekuzi kwa malengo yapi? walikuwa wanapekuwa nyumbani kwa Magufuli kutafuta nini? alikuwa mtuhumiwa? wanafamilia walikuwa na taarifa juu ya huo upekuzi?
Kama wanafamilia hawakuwa na taarifa juu ya huo upekuzi, kuna ubaya gani nikisema hao wapekuaji ndio waliokuwa na nia mbaya, kwa kuweka kiasi hicho cha pesa ili kumchafua marehemu Magufuli? [ hii ni tabia ya polisi wetu wengi].
Naandika hivyo hasa nikizingatia hali iliyojitokeza baada ya msiba wa marehemu Magufuli, wapo walioshangilia kwa namna tofauti, wengine wakadai nchi inapumua, mwingine akadai Mungu ameamua kesi, na mwingine akasema wazuri hawafi, je, hawa hawawezi kutengeneza tukio ili ku justify madai yao dhidi ya marehemu?
Sijui Lissu amezungumza hivyo kwa nia ipi, lakini nikizingatia heshima yake, nafasi yake, na chama anachotoka, siwezi kusema moja kwa moja Lissu anasema uongo, inawezekana ana taarifa za ndani zaidi ambazo wengi wetu hatuna, hasa nikizingatia informers waliokuwa wakimjuza juu ya unyama ambao angeweza kufanyiwa mpaka kukimbia nchi. Naona asibezwe, wala kuaminiwa 100% kwa hii taarifa yake.