Lissu: Dola za Kimarekani Milioni 42 (takribani Tsh. Bilioni 100) zilikutwa nyumbani kwa Magufuli baada ya kufariki

Lissu: Dola za Kimarekani Milioni 42 (takribani Tsh. Bilioni 100) zilikutwa nyumbani kwa Magufuli baada ya kufariki

we unafikiri ni nani mwingine anayeweza kuingia nyumbani kwake, vyombo vya serikali, na bado tutasikia mengi kuhusu huyo mtetezi wenu wa wanaoitwa wanyonge. Mtu mwenye afya njema utakubalije kuitwa mnyonge na we unakubali km zuzu, sema wapambanaji
Mbona wewe umekubali kubatizwa CHAWA!
 
Kiasi chote hicho cha pesa kilikutwa nyumbani kwa Magufuli, ina maana alikiweka kwa siri hata mke wake na wengine wa familia yake hawakujua?

Ina maana baada ya msiba wa Magufuli kutokea, kuna watu waliokwenda nyumbani kwake, wasio wanafamilia waliopekuwa nyumba yake na kukuta kiasi hicho cha pesa?

Kama jibu ni ndio, kuna watu waliingia nyumbani kwa Magufuli na kupekuwa, tujiulize; hawa walifanya upekuzi kwa malengo yapi? walikuwa wanapekuwa nyumbani kwa Magufuli kutafuta nini? alikuwa mtuhumiwa? wanafamilia walikuwa na taarifa juu ya huo upekuzi?

Kama wanafamilia hawakuwa na taarifa juu ya huo upekuzi, kuna ubaya gani nikisema hao wapekuaji ndio waliokuwa na nia mbaya, kwa kuweka kiasi hicho cha pesa ili kumchafua marehemu Magufuli? [ hii ni tabia ya polisi wetu wengi].

Naandika hivyo hasa nikizingatia hali iliyojitokeza baada ya msiba wa marehemu Magufuli, wapo walioshangilia kwa namna tofauti, wengine wakadai nchi inapumua, mwingine akadai Mungu ameamua kesi, na mwingine akasema wazuri hawafi, je, hawa hawawezi kutengeneza tukio ili ku justify madai yao dhidi ya marehemu?

Sijui Lissu amezungumza hivyo kwa nia ipi, lakini nikizingatia heshima yake, nafasi yake, na chama anachotoka, siwezi kusema moja kwa moja Lissu anasema uongo, inawezekana ana taarifa za ndani zaidi ambazo wengi wetu hatuna, hasa nikizingatia informers waliokuwa wakimjuza juu ya unyama ambao angeweza kufanyiwa mpaka kukimbia nchi. Naona asibezwe, wala kuaminiwa 100% kwa hii taarifa yake.

N.B:
Lissu asisahau kuwauliza hao informers waliomwambia kuhusu uwepo wa kiasi hicho cha pesa nyumbani kwa Magufuli, je, wao baada ya kuzikuta hizo pesa walizipeleka wapi? isijekuwa nao wakagawana, halafu wanamnyooshea kidole Magufuli peke yake na kumuita mwizi wakitaka kuonekana wazalendo.
Umeandika point kubwa mkuu
 
Kwamba kuna upekuzi ulianza mara moja nyumbani kwake baada ya kifo cha Magufuri?

Hapo ndiyo anaenda kuwakera wasukuma sasa! Anapambana na mfu anayependwa kwao.
Ajabu sana hii, so na wewe unaamini Jiwe alikuwa msukuma , [emoji848]
 
Hiyo bilion 100 Hata Diamond wa Wasafi anayo ndio ushangae kwa kidume Shujaa Magufuli Waziri miaka 20 Rais miaka 6?

Bavicha mnawaza kimaskini Sana[emoji23][emoji23]
Mkuu unajua zamani nilikuwa najua wewe ni me
 
Nikiwa rais kila Mtanzania lazima anilipe Tshs 300 kila mwezi tuko 60M X 300 = 18,000,000,000 kwa mwezi.
216,00,000,000 kwa mwaka.
1,080,000,000,000 Miaka mitano.
Kama ni 100B tu Magufuli alijimegea pesa kidogo sana,Unayo kinga ya kutoshtakiwa kwanini uogope kupiga pesa za Mafala.
 
Utasikia tozo, tozo.

Kumbe watu wanapiga.
 
Mkuu kumbe na wewe ni Sukuma gang?
Sipo huko kwenye mabishano yenu ya kisiasa wala sijawahi kuwepo,nimehoji tu kama mchangiaji huru,Kila kiumbe chenye uhai kitaonja umauti,sasa unapomuona mtu anayemdhihaki binadamu mwenzake aliyetangulia,linakua sio jambo la kawaida.
 
Akiongea na wananchi wa Bugarama Halmashauri ya Geita Vijijini, Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Antipas Lissu leo Jumamosi ya Agosti 5, 2023 amesema kuwa, aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Magufuli baada ya kufariki kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 42 (zaidi ya Tsh. Bilioni 100), zilikutwa nyumbani kwake Chato.

Kiasi hicho cha fedha ni nyingi hasa ukilinganisha na mshahara wa Rais. Lissu aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, wakati akiwasilisha mada ya uuzwaji na uwekezaji wa bandari.

Lengo la kuweka habari hii hapa ni mshtuko nilioupata.
Uyu mzee hakuuza bandari ila alikua mwizi
 
Niliwahi kushauri, threads za tuhuma za kuchafua watu humu, kwa hearsay ziendane na uthibitisho usiotia shaka, usikute mtoa tuhuma anatafuta a honorary exit ili akitakiwa kuthibitisha, huyooo... anajitimkia zake kurejea kule kwake na kusingizia ametafutwa ili... Hongera JF kwa Whistleblow, JF tubadilike, tusichafue majina ya Watu kwa tuhuma za Hearsay zisizo na Uthibitisho, Ukituhumu, Weka Uthibitisho

Why umtuhumu tuhuma nzito hivi zisizo na uthibitisho al marhum asiyeweza kujitetea?

Kanuni ya tuhuma ni "he who alleges, must proves!".

Kwa msiojua Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

P
Mkuu, sasa hapa unatetea nini!? Kwamba JPM hakuwa fisadi au hizo USD 40 million hazikuwepo!?

Anyway, kwenye ufisadi hilo halina ubishi. Viashiria vyote vinainyesha kuwa JPM alikuwa fisadi kama watangulizi wake..... Kuanzia Hekalu lake Chato, Tausi toka Ikulu. Hotel yake ya 4 Stars Chato, Uwanja wake wa ndege na Bageshi wake na zile Tshs 2.5 Trillion zilizomuondoa kazini Prof Assadi.
 
Kiasi chote hicho cha pesa kilikutwa nyumbani kwa Magufuli, ina maana alikiweka kwa siri hata mke wake na wengine wa familia yake hawakujua?

Ina maana baada ya msiba wa Magufuli kutokea, kuna watu waliokwenda nyumbani kwake, wasio wanafamilia waliopekuwa nyumba yake na kukuta kiasi hicho cha pesa?

Kama jibu ni ndio, kuna watu waliingia nyumbani kwa Magufuli na kupekuwa, tujiulize; hawa walifanya upekuzi kwa malengo yapi? walikuwa wanapekuwa nyumbani kwa Magufuli kutafuta nini? alikuwa mtuhumiwa? wanafamilia walikuwa na taarifa juu ya huo upekuzi?

Kama wanafamilia hawakuwa na taarifa juu ya huo upekuzi, kuna ubaya gani nikisema hao wapekuaji ndio waliokuwa na nia mbaya, kwa kuweka kiasi hicho cha pesa ili kumchafua marehemu Magufuli? [ hii ni tabia ya polisi wetu wengi].

Naandika hivyo hasa nikizingatia hali iliyojitokeza baada ya msiba wa marehemu Magufuli, wapo walioshangilia kwa namna tofauti, wengine wakadai nchi inapumua, mwingine akadai Mungu ameamua kesi, na mwingine akasema wazuri hawafi, je, hawa hawawezi kutengeneza tukio ili ku justify madai yao dhidi ya marehemu?

Sijui Lissu amezungumza hivyo kwa nia ipi, lakini nikizingatia heshima yake, nafasi yake, na chama anachotoka, siwezi kusema moja kwa moja Lissu anasema uongo, inawezekana ana taarifa za ndani zaidi ambazo wengi wetu hatuna, hasa nikizingatia informers waliokuwa wakimjuza juu ya unyama ambao angeweza kufanyiwa mpaka kukimbia nchi. Naona asibezwe, wala kuaminiwa 100% kwa hii taarifa yake.

N.B:
Lissu asisahau kuwauliza hao informers waliomwambia kuhusu uwepo wa kiasi hicho cha pesa nyumbani kwa Magufuli, je, wao baada ya kuzikuta hizo pesa walizipeleka wapi? isijekuwa nao wakagawana, halafu wanamnyooshea kidole Magufuli peke yake na kumuita mwizi wakitaka kuonekana wazalendo.
Mkuu ahsante sana kwa hoja fikirishi. Lakini kwa kuwa Chadema hakuna mwenye akili, hawatakuelewa!
 
Back
Top Bottom