Lissu: Dola za Kimarekani Milioni 42 (takribani Tsh. Bilioni 100) zilikutwa nyumbani kwa Magufuli baada ya kufariki

Lissu: Dola za Kimarekani Milioni 42 (takribani Tsh. Bilioni 100) zilikutwa nyumbani kwa Magufuli baada ya kufariki

Chadema mtu pekee aliewahi kusimama na kuhubiri siasa mpka nikaogopa nikahisi atakua RAIS ni MBOWE.

Waliobaki wengine na wajao nisio wajua Hamna na hatokaa awepo.

Nina sababu zaidi ya 1000 za kuiona CCM ikitawala mpka Unyakuo unafika.
 
Niliwahi kushauri, threads za tuhuma za kuchafua watu humu, kwa hearsay ziendane na uthibitisho usiotia shaka, usikute mtoa tuhuma anatafuta a honorary exit ili akiitwa kuthibitisha, huyooo... kurejea kwake na kusingizia anatafutwa!. Hongera JF kwa Whistleblow, JF tubadilike, tusichafue majina ya Watu kwa tuhuma za Hearsay zisizo na Uthibitisho, Ukituhumu, Weka Uthibitisho

Why umtuhumu tuhuma nzito hivi zisizo na uthibitisho al marhum asiyeweza kujitetea?

Kanuni ya tuhuma ni he who alleges, must proves!.

Kwa msiojua Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

P
Mbingu ipi unayoongelea yupo Kwa baba yake... Hata wauaji na watesi baba yao shetani kwao ni mbingu yao pia Mkuu....
 
Kiasi chote hicho cha pesa kilikutwa nyumbani kwa Magufuli, ina maana alikiweka kwa siri hata mke wake na wengine wa familia yake hawakujua?

Ina maana baada ya msiba wa Magufuli kutokea, kuna watu waliokwenda nyumbani kwake, wasio wanafamilia waliopekuwa nyumba yake na kukuta kiasi hicho cha pesa?

Kama jibu ni ndio, kuna watu waliingia nyumbani kwa Magufuli na kupekuwa, tujiulize, hawa walifanya upekuzi kwa malengo yapi? walikuwa wanapekuwa nyumbani kwa Magufuli kutafuta nini? alikuwa mtuhumiwa? wanafamilia walikuwa na taarifa ya huo upekuzi?

Kama wanafamilia hawakuwa na taarifa juu ya huo upekuzi, kuna ubaya gani nikisema hao wapekuaji ndio waliokuwa na nia mbaya, kwa kuweka kiasi hicho cha pesa ili kumchafua marehemu Magufuli? [ hii ni tabia ya polisi wetu wengi].

Naandika hivyo hasa nikizingatia hali iliyojitokeza baada ya msiba wa marehemu Magufuli, wapo walioshangilia kwa namna tofauti, wengine wakadai nchi inapumua, mwingine akadai Mungu ameamua kesi, na mwingine akasema wazuri hawafi, je, hawa hawawezi kutengeneza tukio ili ku justify madai yao dhidi ya marehemu?

Sijui Lissu amezungumza hivyo kwa nia ipi, lakini nikizingatia heshima yake, nafasi yake, na chama anachotoka, siwezi kusema moja kwa moja Lissu anasema uongo, inawezekana ana taarifa za ndani zaidi ambazo wengi wetu hatuna, hasa nikizingatia informers waliokuwa wakimjuza juu ya unyama ambao angeweza kufanyiwa mpaka kukimbia nchi. Naona asibezwe, wala kuaminiwa 100% kwa hii taarifa yake.
Kwani walikuwa wanazipeleka hawawezi kutoa SIRI? SIO LAZIMA UPEKUZI
 
Unahitaji uthibitisho ?
Kinachoweza kushangaza tu hapa, ni kwa nini habari kama hii ililala usingizi wa pono ikimsubiri Tundu Lissu aitangazie dunia, licha ya kujua lile kundi lililomo ndani ya CCM ambalo hii taarifa ingetangazwa mapema sana kuonyesha alivyokuwa mbaya!
Hili kundi lililokuwa likiwaita wenzao "Sukumagang" hii taarifa haikuwafikia?

Lakini binafsi nauliza tu hapa: Lissu kaiokota hii taarifa na kuiweka mbele ya wanachi kwa mara ya kwanza, kwa lengo gani hasa?

Na ikitokea kuwa ni mtego uliowekwa kumnasa yeye na chama chake, hapo sasa itakuwaje?

Inanishawishi niamini kwamba, hadi Lissu aichukue hii taarifa, hana mashaka yoyote juu ya usahihi wake, vinginevyo ni kujitafutia migogoro isiyokuwa ya lazima, hasa wakati huu mambo yakielekea pazuri.
 
Lissu ni muongo, shida zaidi ni wafuasi wa huyu ropo-ropo ambae hajui anafanya nini kwenye siasa zaidi ya kutupigia kelele zisizo na kichwa wala miguu; halafu kuna watu wanachukua kauli zake at face value.

Baada ya kutunga uongo wake wa DPW sasa kahamia kwa Magufuli; yote hayo yanaisaidia vipi CDM kwenye political mileage za uchaguzi wa 2025.

Wananchi wengi hawana interest na habari za bandari, kwenye mikutano yao CDM ni nadra sana kuzungumzia changamoto za maeneo enyeji wanayozunguka wao ni ropo ropo tu.



$42 million dollars in 100 bills stacks urefu wake ni feet 143, ni sawa na ‘Antony Davies’ kama 21 uwalaze kwenye chumba, hizo hela hata kwenye transit van zinaweza zisitoshe. Huyo Magufuli ni mjinga kiasi gani asijue offshore accounts aweke hizo hela nyumbani kwake.

Ujinga mtupu
Zina uzito wa kilo 400, Kwa noti za 100$, ila kama ni madafu contena inajaa
 
Chadema mtu pekee aliewahi kusimama na kuhubiri siasa mpka nikaogopa nikahisi atakua RAIS ni MBOWE.

Waliobaki wengine na wajao nisio wajua Hamna na hatokaa awepo.

Nina sababu zaidi ya 1000 za kuiona CCM ikitawala mpka Unyakuo unafika.
Labda unyauko wa familia yako, siyo ya watanzania
 
Hicho kizee ninge mwona live ningempa makofi mfululizo tundu ni mpuuzi
 
Uzito wa kiasi hiko Cha Fedha Kwa noti za dola mia ni kilo 400, au gunia 4 za mahindi au mcheke
 
Kiasi chote hicho cha pesa kilikutwa nyumbani kwa Magufuli, ina maana alikiweka kwa siri hata mke wake na wengine wa familia yake hawakujua?...

Amekosea, ushahidi uko wapi hata wa picha tu?

Mbona hakumpa mke wake ubunge, mtoto wake uwaziri, RC,DC, Kurugenzi, Vitengo, kata, CCM? washikaji wake wote wizara nyeti kama Kikwete anavyofanya sasa hivi chini ya SSH.

Wengi hatuna vyama ila ukilinganisha Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Samia. JPM alikuwa na uzalendo.

Uwajibikaji, umeme, maji, nidhamu serikalini hadi mtaani ilionekana. Watu kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uaminifu kwa nafasi zao.

Lissu namuunga mkono kwa asilimia 80 y%, kazi, harakati zake.
Ilitakiwa na inachokiwa akifanye ni kuunganisha nchi, kanda, dini, makabila, vyama vyote, wasio na vyama kupigania Tanzania.

Of course natambua alipigwa risasi wakati wa JPM, lakini kama yupo serious, Watanzania wote tumuunge mkono 100%, Itabidi tu aache kumnanga JPM.
 
Sasa billion 9 za kitanzania ndiyo ushangae kwa mtu mkubwa na nyadhifa kubwa kwa miaka yote hiyo aliyohudumu katika uwaziri na urais?

Aliyezikuta keshi billion 9+ na kuzihesabu ni nani?

Watu akili zinashikwa kwa uongo wa hovyo kabisa[emoji1]
Dola 42m ni zaidi ya bilioni 9,Dola milionii moja ni sawa na bilioni 2.5
 
Wavujisha habari watakuwa ni ndumila kuwili wa CCM waliosemwa na Magufuli kuwa mchana wanamuunga mkono usiku wanampinga hasa kundi la watu wasiojulikana kwa kuwa wao ndio wanaonyosha mapito ya viongozi.
 
Kwani walikuwa wanazipeleka hawawezi kutoa SIRI? SIO LAZIMA UPEKUZI
Wakatoa "SIRI", na serkali ikachukua jukumu la kwenda nyumbani kuzichukua kimya kimya hadi leo hii alipolizungumzia hili Lissu kwa mara ya kwanza?

Tulishawahi kusikia zile pesa za 'pre-bargain', kwamba zilipelekwa China, na hizi je, wakaamua wazinyamazie?
 
Back
Top Bottom