Lissu: Dola za Kimarekani Milioni 42 (takribani Tsh. Bilioni 100) zilikutwa nyumbani kwa Magufuli baada ya kufariki

Lissu: Dola za Kimarekani Milioni 42 (takribani Tsh. Bilioni 100) zilikutwa nyumbani kwa Magufuli baada ya kufariki


Akiongea na wananchi wa Bugarama Halmashauri ya Geita Vijijini, Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Antipas Lissu leo Jumamosi ya Agosti 5, 2023 amesema kuwa, aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Magufuli baada ya kufariki kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 42 (zaidi ya Tsh. Bilioni 100), zilikutwa nyumbani kwake Chato.

Kiasi hicho cha fedha ni nyingi hasa ukilinganisha na mshahara wa Rais. Lissu aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, wakati akiwasilisha mada ya uuzwaji na uwekezaji wa bandari.

Lengo la kuweka habari hii hapa ni mshtuko nilioupata.
Harafu Serikali ikazichukua au mataga wakagawana? Simon
 

Akiongea na wananchi wa Bugarama Halmashauri ya Geita Vijijini, Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Antipas Lissu leo Jumamosi ya Agosti 5, 2023 amesema kuwa, aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Magufuli baada ya kufariki kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 42 (zaidi ya Tsh. Bilioni 100), zilikutwa nyumbani kwake Chato.

Kiasi hicho cha fedha ni nyingi hasa ukilinganisha na mshahara wa Rais. Lissu aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, wakati akiwasilisha mada ya uuzwaji na uwekezaji wa bandari.

Lengo la kuweka habari hii hapa ni mshtuko nilioupata.
Nani na Nani walioziona hizo pesa ??!!
 
Hivi wewe ndiyo unasikia leo hili?

Hili lilisemwa semwa siku chake tu baada ya kifo chake lakini ghafla taarifa zikazimwa. Nadhani, Pandora box inaanza kufunguliwa mdogo mdogo na mwisho wa siku hakuna kitu chochote kilichofanyika sirini hakitatokelezea katika Nuru..!!

After all unajiuliza maswali ya kitoto sana ndugu yangu denooJ..

Kwa sababu kama unashangaa na kujiuliza maswali rahisi kuhusu huyu bwana kukutwa na pesa tu nyumbani kwake, kwanini usishangae na kujiuliza maswali magumu zaidi kama vile; hivi iweje Rais wa nchi augue ktk muda usiozidi wiki tu na taarifa za kuugua kwake zikifichwa fichwa na baada muda tunataarifiwa kuwa kafia kwenye kituo cha afya kiitwacho "Mzena??"

Hujiulizi maswali haya??

Majibu yake ni rahisi mno. Na ni kuwa, it's obviously kifo chake si cha asili (not a natural death) bali ni cha kutengenezwa na tena na watu wake mwenyewe na ni wenzake aliowaamini humo humo ndani ya serikali..

Kama wali plan na kutekeleza mpango wa kifo chake, washindwe nini ku - expose na Kila Siri na uchafu wake..?

Hupaswi kushangaa hili. Hata Rais wa Sudan, Hayati Omar Al Bashir mara baada ya kifo chake, nyumbani kwake kulikutwa chumba kmoja kimesheheni maboksi na maboksi ya million of dollars...

Hiyo ndiyo tabia ya viongozi dictators wote duniani, kuiba na kuficha fedha kwa sababu wanaamini ndiyo ulinzi na usalama yao badala ya Mungu aliyewaumba..!!!
Ajabu sana, maswali yangu niliyouliza yanayohusu mada iliyoko mezani unayaita ya kitoto, huku wewe uliyeuliza maswali yaliyopo nje ya mada kuhusu kifo cha Magufuli ndio unajiona mjanja, Ok.
 
Hili lilisemwa sana wakati Magufuli amezikwa. Watanzania ni ama wasahaulifu sana au hawataki kufuatilia mambo. Kwa kifupi Magufuli alikuwa na fedha nyingi ameziweka nyumbani na hii habari ilizungumzwa sana.
Na mke wake akaamua kumuumbua mume wake. ??!!
Hii kitu haiingii akilini kwa watu wenye kufikiri vizuri !!

Au Mahakama ilitoa search warrant ndio baada ya upekuzi zikagundulika hizo pesa ??!!
Lazima ujiulize maswali mengi walishindwaje kuzificha hizo fedha familia yake ??!! Fake news !!!
 
Moja ya sifa kubwa ya Lissu ni kusema ukweli. Hana tabia ya kusingizia uongo mtu hata kama ni mbaya wake.
Lakini hili jambo nilisikia likisemwa na watu wenye dhamana wa ndani zaidi.
Kusikia peke yake hakutoshi kuthibitisha..
 
N.B:
Lissu asisahau kuwauliza hao informers waliomwambia kuhusu uwepo wa kiasi hicho cha pesa nyumbani kwa Magufuli, je, wao baada ya kuzikuta hizo pesa walizipeleka wapi? isijekuwa nao wakagawana, halafu wanamnyooshea kidole Magufuli peke yake na kumuita mwizi wakitaka kuonekana wazalendo.
The main contention hapa ni kuwa magufuli 42,000,000 US$ zilikutwa kwake na alizitoa wapi! That is what was pleaded by Lisu, we should stick to our pleadings! Zilikwenda wapi that is another independent inquiry!
 
Hii mistari..., kuna jibu humo.

Itakuwa nijambo la kushangaza sana Lissu kuyasema hayo aliyosema, tena mahali alipoyasemea na ikawa ni kelele za kupayuka tu.

Nia ya kuyasema haya katika hadhara hiyo hasa ililenga kitu gani?

Lissu ana tabia moja ambayo sasa inajulikana. Hana tabia ya kinafiki, kulembalemba juu ya jambo lolote analolijua yeye.
Shida pekee ninayomtahadharisha juu yake, ni kuwa na uhakika juu ya usahihi anayoambiwa, na yeye kuyatangaza.

Kutokana na tabia aliyokuwa nayo Magufuli, siwezi kamwe kwa sasa hivi kutetea kwamba asemayo Lissu ni uongo.

Ila, kama ulivyoeleza, huo msako nyumbani kwa Magufuli ulifanywa na nani na kwa sababu zipi hasa?
Hii kitu ya kuambiwa halafu anatangaza kisha anaonekana mpinzani jasiri naona ilianzia kwa Dr. Slaa, nae alikuwa akipenyezewa taarifa na TISS na kuzitangaza, lakini mwisho wa siku akaja kufanya alichofanya 2015 nikiamini kabisa, maamuzi yake yaliingiliwa na ushauri wa TISS.
 
Hivi bilioni 100 zinafanya nn nyumbani kwa mtu? Tutumie akili basi😂😂
Halafu jumba lote lile pakosekane mahali salama pa kuziweka hizo pesa ili watu wengine wasiohusika wasizione ??!! ??!!
Ndio maana tunauliza Ilitolewa search warrant ili nyumba ya Rais ipekuliwe 😅😅 !! Fake news !!
 
Mwizi mwizi tu hata akifa tutalisema jina na kabuli lake kwakua aliezikwa humo alikua muuaji pia mwizi magufuli alikua mwizi Huku akitangaza mtakatifu
 
Back
Top Bottom