Lissu: Dola za Kimarekani Milioni 42 (takribani Tsh. Bilioni 100) zilikutwa nyumbani kwa Magufuli baada ya kufariki

Lissu: Dola za Kimarekani Milioni 42 (takribani Tsh. Bilioni 100) zilikutwa nyumbani kwa Magufuli baada ya kufariki

Na mke wake akaamua kumuumbua mume wake. ??!!
Hii kitu haiingii akilini kwa watu wenye kufikiri vizuri !!

Au Mahakama ilitoa search warrant ndio baada ya upekuzi zikagundulika hizo pesa ??!!
Lazima ujiulize maswali mengi walishindwaje kuzificha hizo fedha familia yake ??!! Fake news !!!
Hujui wewe. Na hujui zilikuwa wapi. Baki na kutojua kwako.
 
Nachoona Lisu ana balance mambo,kamtukana sana Samia hadi kuitwa na DCI kuhojiwa. Lisu kagoma kwenda. Unafikir ni rahisi kugomea mamlaka na kuendelea kutamba?Lisu anajua Hasimu mkubwa wa namlaka ni Sukuma gang, ukiiponda Sukuma gang na jiwe unakua kwenye position nzuri ya kutoguswa.CCM hawasumbuliwi na CHADEMA wala ACT,CCM wanasumbuliwa na Sukuma gang, kama Lisu angeendelea Kumtukana Rais na akaside na Sukuma gang mamlaka zingekua zimemshughulikia kitambo sana. Ziara ya Lisu huko Chato ni faida ya CCM na sio LISU na CHADEMA coz mnufaika mkubwa wa SIASA za kumponda jiwe na sukuma gang ni CCM.Kuna Possibility ni maelezo ya CCM wenyewe kwa Lisu ili mambo yake yawe sawa aende chato akatoe makavu kwa Sukuma gang na jiwe wao.Toka mwanzo niliwahi sema CHADEMA hawako kuiondoa CCM madarakani, wako kuhakikisha CCM inadumu milele na ndio maana hata kwa hali iliyopo CHADEMA hawataki kuungana na kundi kubwa la sukuma gang kupambana na CCM.Watapambana na CCM lakini watakuja kubalance kwa kuishambulia sukuma gang, hapa mnufaika ni CCM.Lisu anajua ili upate kura nyingi kanda ya ziwa we msifie Jiwe,kwanini hafanyi hivyo?Ni mkakati wa CCM huo,wamewapa uhuru wa kufanya SIASA kila kona lakini sio kuungana na hili kundi.Wapige kelele watakavyo lakini wakumbuke pia sukuma gang inatakiwa kushambuliwa. Chadema haina tofaut na ACT, ukiwa smart utalitambua hili.

Ukisema Lisu sio mnafki utakua umeanza kumfuatilia Lisu leo.Huyu ndiye aliyemnadi Lowasa 2015.Huyu ndiye aliyekua anamsifia sana Samia na kumponda Magufuli.Saiz tena mara amponde Samia mara amsifie Magufuli mara amponde tena.So ni mtu wa kucheza na akili za wajinga wajinga na sio watu smart.Ukiona Kipa hayupo goloni na mfungaji kakosa goli katika mazingira ya wazi kabisa lazima ujiulize kuna nini?Mazingira ya CCM kutoka madarakani yako wazi kabisa. CHADEMA +SUKUMA GANG,CCM inatoka madarakani mapema sana ila sasa unakuta Lisu na CHADEMA wako busy kuishambulia Sukuma gang. CCM wanataka hali kama hii.Kulikua na mkutano wa kupinga bandari kuuzwa,ulimuona Lisu?Kuna kesi ya mwabukusi na wenzie,unawaona akina Lisu,Mbowe,Kibatala na wengine toka Chadema wakitoa msukumo?Ukifuatilia Lisu anasimama peke yake ndani ya Chadema kupambana na CCM,Mbowe naye anasimama peke yake kupambana na CCM na wengine wadogo wadogo ndio wanatumia chama kupambana na CCM, Sio Bahati mbaya. CCM inataka mfumo kama huu,ACT wako peke yao,Lisu yupo peke yake,Mbowe peke yake,Sukuma gang peke yao.

Niishie hapa
Dah!...
 
Kiasi chote hicho cha pesa kilikutwa nyumbani kwa Magufuli, ina maana alikiweka kwa siri hata mke wake na wengine wa familia yake hawakujua?

Ina maana baada ya msiba wa Magufuli kutokea, kuna watu waliokwenda nyumbani kwake, wasio wanafamilia waliopekuwa nyumba yake na kukuta kiasi hicho cha pesa?

Kama jibu ni ndio, kuna watu waliingia nyumbani kwa Magufuli na kupekuwa, tujiulize; hawa walifanya upekuzi kwa malengo yapi? walikuwa wanapekuwa nyumbani kwa Magufuli kutafuta nini? alikuwa mtuhumiwa? wanafamilia walikuwa na taarifa juu ya huo upekuzi?

Kama wanafamilia hawakuwa na taarifa juu ya huo upekuzi, kuna ubaya gani nikisema hao wapekuaji ndio waliokuwa na nia mbaya, kwa kuweka kiasi hicho cha pesa ili kumchafua marehemu Magufuli? [ hii ni tabia ya polisi wetu wengi].

Naandika hivyo hasa nikizingatia hali iliyojitokeza baada ya msiba wa marehemu Magufuli, wapo walioshangilia kwa namna tofauti, wengine wakadai nchi inapumua, mwingine akadai Mungu ameamua kesi, na mwingine akasema wazuri hawafi, je, hawa hawawezi kutengeneza tukio ili ku justify madai yao dhidi ya marehemu?

Sijui Lissu amezungumza hivyo kwa nia ipi, lakini nikizingatia heshima yake, nafasi yake, na chama anachotoka, siwezi kusema moja kwa moja Lissu anasema uongo, inawezekana ana taarifa za ndani zaidi ambazo wengi wetu hatuna, hasa nikizingatia informers waliokuwa wakimjuza juu ya unyama ambao angeweza kufanyiwa mpaka kukimbia nchi. Naona asibezwe, wala kuaminiwa 100% kwa hii taarifa yake.

N.B:
Lissu asisahau kuwauliza hao informers waliomwambia kuhusu uwepo wa kiasi hicho cha pesa nyumbani kwa Magufuli, je, wao baada ya kuzikuta hizo pesa walizipeleka wapi? isijekuwa nao wakagawana, halafu wanamnyooshea kidole Magufuli peke yake na kumuita mwizi wakitaka kuonekana wazalendo.
kitu ambacho huwezi kukielewa Mpaka sasa hata hao walinzi wake wanaweza kutoa siri za magufuri, kwa hiyo usi panic mkuu
 
Kwahiyo tukubaliane hoja ya Lissu kusema Rais samia kagawa bandari bure kwa waarabu ni ya uwongo?
Kwani huo ni mjadala wa Lissu..?mbona ye kaukuta..hujui kuna watu hadi wamefungua kesi?? Kuna watu wameshikiliwa hadi sasa kwa ajili ya hiyo ishu.

Lissu kadandia tu kutafuta political mileage.
 
Shida Lissu ukimbana kwa chochote kesho yake unasikia karudi Ubelgiji na stori nyingi za kuitwa na daktari wake au katishiwa kuawa
 
Somo ninalolipata kutokana na makala hii ni kwamba Tanzania haijawahi kuwa na chama cha upinzani,
bali kuna vyama vya upinzani pandikizi. Kwa kusema hivyo
nijitetee kwa kusema,Kitendo cha dokta sulaa alichotufanyia 2015 akisaidiana na porofesa wa buguruni
mimi kama mfuasi wa upinzani miaka hiyo kilinipa fundisho kwamba
viongozi wa upinzani ni mapandikizi wa chama kijani wanapoona dalili za upinzani kuingia ikulu,wanapiga hatua moja nyuma kwa kuanzisha mtafaruku baina yao ili wasishike dola.

Sasa hii hoja aliyoiibua TL kwangu naona ni mwendelezo huo huo,wa kutufanya wajinga.
Tujifanye anachokisema ni kweli,niulize swali,je huu ni wakati sahihi kuingiza hoja hiyo
kipindi hiki cha kukomboa bandari zetu na kupigania katiba mpya?

Ninachoshukuru,binafsi baada ya kuona ubabaishaji huu mkubwa
nimeamua kuisaka kadi ya chama tawala,ili mdogo mdogo
hata nigombee ujumbe wa shina,kwa kufanya hivyo nitawatendea haki
wanashina langu nitakalokuwa naongoza.
Hiki hakina tofauti na kile kisa cha mko vitani halafu askari mwenzenu anawasaliti alichosimulia Magu.

Huyu amekuwa msaliti siku zote..
 
Kwani huo ni mjadala wa Lissu..?mbona ye kaukuta..hujui kuna watu hadi wamefungua kesi?? Kuna watu wameshikiliwa hadi sasa kwa ajili ya hiyo ishu.

Lissu kadandia tu kutafuta political mileage.
Hujajibu swali Lissu anaaminika au haaminiki?
 
Radio mbao usema baada ya tangazo la msiba walinzi walijisevia mabunda.
Walibomoa wakachomoa wakajenga Tena.
Uenda zilizokutwa ni chache baada ya kuchotwa zingine na walinzi
 
Tupate mwingine Bhasi kama Yeye aisee ambae atakuwa hata Nusu ya Magufuliii... !! Maana nchi imeenda kombooo ni mwendo wa kulaliana tuuu.. huku bandari inauzwaa hukuu dola inapoteaa hatujakaa sawa mafuta beii Juu..!
 
Unajua Watanzania wengi wanajua Magufuli ni malaika na hakuwa na tamaa...
Ilipofika tarehe 6 March 2021 kulianza uvumi Magufuli mbona hajaonekana kanisani... Watu hawakufikiri kwa undani hii taarifa..
Wengi wanafikiri Mkuu aliondoka tarehe 17... Ila kabla ya hiyo tarehe yalifanyika mengi sana...

Kuhusu hela .. Ni hivi kulikuwa na hela kweli ndani ya nyumba ya Mkuu pale Chato kujua ni kiasi gani.. Ni siri ya wahusika.. (Lissu kusema ni 42 millions USD inawezekana ni kidogo au zilikuwa zaidi)

Lakini hela nyingi zilikuwa zinahusisha project za ujenzi na zilipitia kwa marafiki zake wa Tanroads..

Boss wa Tanroads alikuwa kwenye misukosuko na pressure kali sana ili kutoa ushirikiano kwa namna pesa ilivyokuwa inapitia kwao kwenda sehemu mbalimbali hasa kwa mambo ambayo hayahusu Tanroads

Wakandarasi waliofahamiana naye walijipendekeza kumpelekea rupia mkuu..
Pesa za wafanyabiashara wa beural de change nyingi hazikuingia BOT..
Na mbaya hazijulikaniki nyingi zimepotelea wapi... (Kwanini tusifikirie aliyewatuma na yeye hakujigawia?)

Mbaya zaidi waliotumwa task force wengine sasa hivi ni mamilionea.. Na bado kuna watu walikuwa wanasifia haya yatokee ili watu wawe maskini..
 
Njaaa kali inakus
Niliwahi kushauri, threads za tuhuma za kuchafua watu humu, kwa hearsay ziendane na uthibitisho usiotia shaka, usikute mtoa tuhuma anatafuta a honorary exit ili akitakiwa kuthibitisha, huyooo... anajitimkia zake kurejea kule kwake na kusingizia ametafutwa ili... Hongera JF kwa Whistleblow, JF tubadilike, tusichafue majina ya Watu kwa tuhuma za Hearsay zisizo na Uthibitisho, Ukituhumu, Weka Uthibitisho

Why umtuhumu tuhuma nzito hivi zisizo na uthibitisho al marhum asiyeweza kujitetea?

Kanuni ya tuhuma ni "he who alleges, must proves!".

Kwa msiojua Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani


P
[/QUOnjaaa Kali inakusukbua Sana mbaya Zaid ccm wamewafuta machawa wote kuanzia HV Sasa hawatakiwi nakuome huruma mno
 
Billioni 100 mtu unaweka chumbani?! Huu ni ulafi mkubwa!
Kweli ni ulafi mkubwa, je anaweza kujibu?
Btw, kuna watu walio hai wanaotuhumiwa kushirikiana na marehemu kutorosha mabilion mengine kupeleka nje ya nchi, serikali au hata upinzani wamewachukulia hatua gani?

Siku zote wanasiasa ni kuwa nao makini sana maana wanachosema mara nyingi 'sii hasa'.
 

Akiongea na wananchi wa Bugarama Halmashauri ya Geita Vijijini, Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Antipas Lissu leo Jumamosi ya Agosti 5, 2023 amesema kuwa, aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Magufuli baada ya kufariki kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 42 (zaidi ya Tsh. Bilioni 100), zilikutwa nyumbani kwake Chato.

Kiasi hicho cha fedha ni nyingi hasa ukilinganisha na mshahara wa Rais. Lissu aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, wakati akiwasilisha mada ya uuzwaji na uwekezaji wa bandari.

Lengo la kuweka habari hii hapa ni mshtuko nilioupata.
tundu lisu haekeweki huenda hata hoja za bandari ni zakufikrika! huyo jamaa kumbe akili haziko sawa unatoa tuhuma nzito kama hizo kama nyumba ya raisi ilipekuliwa tena chato duuh huyo jamaa haa!iniki kabisa
 
Back
Top Bottom