Lissu: Dola za Kimarekani Milioni 42 (takribani Tsh. Bilioni 100) zilikutwa nyumbani kwa Magufuli baada ya kufariki

Lissu: Dola za Kimarekani Milioni 42 (takribani Tsh. Bilioni 100) zilikutwa nyumbani kwa Magufuli baada ya kufariki

Ajabu sana, maswali yangu niliyouliza yanayohusu mada iliyoko mezani unayaita ya kitoto, huku wewe uliyeuliza maswali yaliyopo nje ya mada kuhusu kifo cha Magufuli ndio unajiona mjanja, Ok.
Hata niliyokuandikia yanahusu mada pia na sijaribu kujifanya najua bali nimekuambia ninayojua...

Nilikuwa najaribu kukuambia, ujaribu tu kufikiri kwa frequency za masafa marefu zaidi badala ya kujiuliza maswali madogo, rahisi na ya kiwango cha chini kama hayo ya "wamejuaje kuwa ana pesa hizo? au waliingiaje ndani mwake? na mengine yanayofanana haya..

Kama hujanielewa, basi hiyo ni shida yako lakini nakuhakikishia ukijaribu kunisoma tena kwa upya na umakini, utanielewa..
 
Hii kitu ya kuambiwa halafu anatangaza kisha anaonekana mpinzani jasiri naona ilianzia kwa Dr. Slaa, nae alikuwa akipenyezewa taarifa na TISS na kuzitangaza, lakini mwisho wa siku akaja kufanya alichofanya 2015 nikiamini kabisa, maamuzi yake yaliingiliwa na ushauri wa TISS.
Mfano na mlinganisho sahihi kabisa.

Hofu kubwa sasa ni kwa Lissu kutumiwa kama kifaa. Ni lazima awe mwangalifu sana.
 
Kwani Magufuli hakuwa na miradi yake ya kumuingizia pesa⁉️ zingine ni propaganda tu
 

Akiongea na wananchi wa Bugarama Halmashauri ya Geita Vijijini, Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Antipas Lissu leo Jumamosi ya Agosti 5, 2023 amesema kuwa, aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Magufuli baada ya kufariki kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 42 (zaidi ya Tsh. Bilioni 100), zilikutwa nyumbani kwake Chato.

Kiasi hicho cha fedha ni nyingi hasa ukilinganisha na mshahara wa Rais. Lissu aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, wakati akiwasilisha mada ya uuzwaji na uwekezaji wa bandari.

Lengo la kuweka habari hii hapa ni mshtuko nilioupata.
Magufuli alikuwa jizi hilo halina ubishi
 
Vita kambi Sukuma Gang vs Chawa Mama ....
Kazi ipo sanaa
 
Kiasi chote hicho cha pesa kilikutwa nyumbani kwa Magufuli, ina maana alikiweka kwa siri hata mke wake na wengine wa familia yake hawakujua?

Ina maana baada ya msiba wa Magufuli kutokea, kuna watu waliokwenda nyumbani kwake, wasio wanafamilia waliopekuwa nyumba yake na kukuta kiasi hicho cha pesa?

Kama jibu ni ndio, kuna watu waliingia nyumbani kwa Magufuli na kupekuwa, tujiulize; hawa walifanya upekuzi kwa malengo yapi? walikuwa wanapekuwa nyumbani kwa Magufuli kutafuta nini? alikuwa mtuhumiwa? wanafamilia walikuwa na taarifa juu ya huo upekuzi?

Kama wanafamilia hawakuwa na taarifa juu ya huo upekuzi, kuna ubaya gani nikisema hao wapekuaji ndio waliokuwa na nia mbaya, kwa kuweka kiasi hicho cha pesa ili kumchafua marehemu Magufuli? [ hii ni tabia ya polisi wetu wengi].

Naandika hivyo hasa nikizingatia hali iliyojitokeza baada ya msiba wa marehemu Magufuli, wapo walioshangilia kwa namna tofauti, wengine wakadai nchi inapumua, mwingine akadai Mungu ameamua kesi, na mwingine akasema wazuri hawafi, je, hawa hawawezi kutengeneza tukio ili ku justify madai yao dhidi ya marehemu?

Sijui Lissu amezungumza hivyo kwa nia ipi, lakini nikizingatia heshima yake, nafasi yake, na chama anachotoka, siwezi kusema moja kwa moja Lissu anasema uongo, inawezekana ana taarifa za ndani zaidi ambazo wengi wetu hatuna, hasa nikizingatia informers waliokuwa wakimjuza juu ya unyama ambao angeweza kufanyiwa mpaka kukimbia nchi. Naona asibezwe, wala kuaminiwa 100% kwa hii taarifa yake.

N.B:
Lissu asisahau kuwauliza hao informers waliomwambia kuhusu uwepo wa kiasi hicho cha pesa nyumbani kwa Magufuli, je, wao baada ya kuzikuta hizo pesa walizipeleka wapi? isijekuwa nao wakagawana, halafu wanamnyooshea kidole Magufuli peke yake na kumuita mwizi wakitaka kuonekana wazalendo.
Hayo maswali kawaulize ndugu zake Magufuli, kilicho dhahiri Magufuli alikuwa mwizi, jambazi, mwuaji, period!
 
Niliwahi kushauri, threads za tuhuma za kuchafua watu humu, kwa hearsay ziendane na uthibitisho usiotia shaka, usikute mtoa tuhuma anatafuta a honorary exit ili akitakiwa kuthibitisha, huyooo... anajitimkia zake kurejea kule kwake na kusingizia ametafutwa ili... Hongera JF kwa Whistleblow, JF tubadilike, tusichafue majina ya Watu kwa tuhuma za Hearsay zisizo na Uthibitisho, Ukituhumu, Weka Uthibitisho

Why umtuhumu tuhuma nzito hivi zisizo na uthibitisho al marhum asiyeweza kujitetea?

Kanuni ya tuhuma ni "he who alleges, must proves!".

Kwa msiojua Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

P
Magufuli alikuwa mwizi mzee, wewe mwenyewe si alikunyoosha kwa kumwuliza tu swali?
 
Yuko sahihi kabisa
Huyu amefariki natamani wakampekue na Kikwete kwake watuambie watamkuta na ngapi ili atueleze akiwa hai tusisubiri mtu afe nafikiri itafaa zaidi.
 

Akiongea na wananchi wa Bugarama Halmashauri ya Geita Vijijini, Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Antipas Lissu leo Jumamosi ya Agosti 5, 2023 amesema kuwa, aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Magufuli baada ya kufariki kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 42 (zaidi ya Tsh. Bilioni 100), zilikutwa nyumbani kwake Chato.

Kiasi hicho cha fedha ni nyingi hasa ukilinganisha na mshahara wa Rais. Lissu aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, wakati akiwasilisha mada ya uuzwaji na uwekezaji wa bandari.

Lengo la kuweka habari hii hapa ni mshtuko nilioupata.
Tafuteni kiki nyingine
 
Kuna siku moja niliandika kuwa mtu yeyote wa Upinzani anaweza kuwa Rais mzuri isipokuwa Lissu. Ni mtu mtu mropokaji sana anayetoa tuhuma bila ushahidi. Zilikutwa dola kiasi hicho na hajasema zilikuwa na nani na zilipelekwa wapi, naa yeye alijuaje kama kweli zilikutwa ilhali hakuwapo. Hata kama aliambiwa, basi ni kiongozi anayetaka kusikia anayotaka tu, yaani ukimwambia analotaka kusikia hata kama ni ya uwongo basi yeye atayachukuwa kuwa ni ya kweli bila hata kuyahoji. Ukimwambia ukweli ambao hataku kusikia atasema huo ni uwongo.
 
Mkuu wewe huwa ni mtu unayejinasibu kama mtu with "an ear to the ground".
No sijinasibu, ila both parents walikuwa huko, hivyo unajikuta umezaliwa with an average intel lakini sio mtu wa kule!.
Usitutapeli kuwa hili uikuwa hulijui.
By nature ya professional yangu, kuna mengi tunasikia, but sio kila unachosikia ni kweli!, vitu vingine ni too much exaggerated, hivyo you have to use your natural intel to make sense of it!. $ 42 m, is not a joke!, it just doesn't make sense!.
Kwamba a large amount of solid, hard cash, zilikutwa nyumbani wa Magufuli, that is common knowledge.
Tunafunika kombe ili wanaharamu gani wapite?
Duh...!
Otherwise hata Magufuli aliwahi kusema msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
Kiukweli kabisa JPM alikuwa mkweli daima and sometimes mkweli too much!.
Ile issue nilioitiwa Bungeni, ni yeye aliisema!.
Hata zile pyu pyu alizisema!.

Hii issue ya mimi kuwa na sniffing nose kuhusu baadhi ya watu or issues ni kweli niko vizuri, na sio najisifu!.

Kuhusu hili la kupoteza watu, ... angalia tarehe ya bandiko hili Nimetishwa, kushitushwa na kuogopeshwa na kauli hii ya Rais Magufuli. Alimaanisha nini?
P
 
Mkuu, sasa hapa unatetea nini!? Kwamba JPM hakuwa fisadi au hizo USD 40 million hazikuwepo!?
Kuna wengi tuu hawajui the volume of US $ 42m!. It doesn't make sense mtu awenazo cash, nyumbani!.
Hata kama ni kickbacks za grand corruption, inamaana hizo fedha zimeletwa nchini in cash!. Who would bring such bulk undetected?, inamaanisha zimeletwa kwa diplomatic bag!, ukifikiria hayo yote!, it really doesn't make sense!.

Acheni kusingizia marehemu vitu vya ajabu! Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani
P
 

Akiongea na wananchi wa Bugarama Halmashauri ya Geita Vijijini, Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Antipas Lissu leo Jumamosi ya Agosti 5, 2023 amesema kuwa, aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Magufuli baada ya kufariki kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 42 (zaidi ya Tsh. Bilioni 100), zilikutwa nyumbani kwake Chato.

Kiasi hicho cha fedha ni nyingi hasa ukilinganisha na mshahara wa Rais. Lissu aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, wakati akiwasilisha mada ya uuzwaji na uwekezaji wa bandari.

Lengo la kuweka habari hii hapa ni mshtuko nilioupata.
I can't belive this lie without reliable evidence.
 
Back
Top Bottom