Lissu haelewi maana ya ‘Jeshi la Akiba’?

Unazungumzia Sungusungu kuwa jeshi la akiba ?

Kama hujui uliza usaidiwe.
 
Jeshini kuna Active Force Na Reserve force Na maana Ya Reserve Force ni Jeshi la Akiba ambalo hapo nyuma liliitwa Mgambo ila kwa sasa ni Jeshi la akiba Na lina MKUU wao kabisa so hapo Lissu kajichanganya sana
Tusaidie ndg, ni kwa kifungu gani cha Sheria/Katiba. Maana mgambo bado wapo
 

Wako watu ambao na sema ni wajinga wanao mpa Lissu sifa asizokuwa nazo. Haiwezekani kawa bungeni miaka ya kutosha. Hajui kwa nini wako makamanda wa mgambo Mkoa na Wilaya tena Wanajeshi wa jeshi letu la kizalendo JWTZ. Hajui wala kuelewa Kwa nini polisi kuna dawati la ulinzi shirikishi na polisi kata. Eti, eti, eti...eti! ndio huyu huyu anataka awe rais. Aende akagombee urais wa kile chama chao duniani na yule seneta wa USA.

Lissu kanifanya niamue Rasmi kuanzia hivi ninavyo andika hapa, ni kiwa mzima wa afya kama Mungu atavyo nijalia mwaka 2030 nitagombea urais wa JMT na nitashinda.
 
Kwa kuongezea hata Askari wastaafu wa Jwtz ni part ya Jeshi la akiba
Kwahiyo askari wastaafu wa JWTZ wana mandate ya kwenda kulinda mikutano ya siasa?

Hiki mnachokitetea ni hatari sana kwa nchi ila kwa sababu wenzetu nchi ndiyo ccm fanyeni ila kama mnataka taifa hili liangamie ni kukalia kimya huu uhuni anaofanya Siro sijui kwa kutumwa na nani
 
Jeshi la mgambo siyo jeshi la akiba.

Kuna tofauti kati ya auxiliary police na Reserve Army.
Go and read bro...usiwe unabisha tu bila kua na facts....using English key words wont change the fact kua Jeshi la Akiba na Jeshi la Mgambo are one in the same.
View attachment 1557261
 
Lisu ndio maana anajifichia nyuma ya hoja yake ya Risasi tofauti na hapo ni empty set.

Hoja ya kitoto sana hii, yaani mijadala kama hii ndio ile mtu mkiwa kijiweni unaitoa ili kupotezea muda,

Stori za vijiweni ndio hoja anazokuja nazo mgombea Urais wa Chadema,

Inasikitisha sana.
 
Hebu tupe kifungu kinachotambua hili jeshi la akiba la hao watoto wadogo.?
 

Acha upotashaji wewe, hii haiko kwenye matakwa ya kisheria ya hiyo ajira ya JWTZ. Lakini kwa migambo na JKT wakati wa vita wanaweza kupekekwa mstari wa mbele kama chambo, kusaidia logistics zingine za kivita nk.
 
Jeshini kuna Active Force Na Reserve force Na maana Ya Reserve Force ni Jeshi la Akiba ambalo hapo nyuma liliitwa Mgambo ila kwa sasa ni Jeshi la akiba Na lina MKUU wao kabisa so hapo Lissu kajichanganya sana
UMETOA DOZI KUBWA KWA MWANAFUNZI WA CHEKECHEA LABDA MWONGEZEE KWAMBA MKUU WA JESHI LA AKIBA ANA CHEO CHA MAJOR GENERAL KUTOKA JWTZ LABDA YEYE NA WAPAMBE WAKE WATAELEWA
 
Hebu tupe kifungu kinachotambua hili jeshi la akiba la hao watoto wadogo.?

Soma michango hapa, yuko mchangiaji kesha weka screen short yake kutoka kwenye katiba ya lugha ya Kisukuma. Kama wewe ni Msukuma ama ulishawahi kuishi Usukumani.
 
Tunahoji uhalali wao kisheria ni sheria ipi imeunda hilo jeshi la akiba ?

Je lini mikutano ya kisiasa imeanza kulindwa sungusungu ?
 
Na wewe ni empty set kabisa, tuna jeshi moja tu???

Wewe unalenga Jwtz tu, lakini haujui kuwa Kuna Jeshi la Polisi, Jeshi la magereza,Jeshi la zimamoto, Jeshi la kujenga taifa,hayo yote kwako sio majeshi???
 
Hii sheria ya JWTZ haiwapi mamlaka reserve Army wa huko kufanya kazi kwenye mikutano ya kisiasa.

Ndiyo maana nchi haiendelei hii wengi wenu mnaopata nafasi za kuongoza watanzania hamna akili na maarifa ya kutosha kuongoza nchi.
Acha ujinga reserve forces (Mgambo) wakati wa amani wanatumika kama Police auxiliary au police wasaidizi na wanawajibika moja kwa moja kwa polisi na ndiyo maana sehemu nyingi wanamgambo wanalinda pasipokuwepo polisi na wanafanya vizuri sana kwakuwa nguvu kazi hii inapatikana kila mahali kuliko polisi ambao ni wachache kufika kila eneo ila wakati wa vita majeshi yote active na reserve forces huungana pamoja chini ya JWTZ kupambana na adui rejea vita vya Kagera kama ulikuwepo kama hukuwepo kaa kimya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…