Lissu hajawahi kutamka neno Rais apinduliwe

Lissu hajawahi kutamka neno Rais apinduliwe

Kweli kabisa mkuu, wangejua jinsi jeshi likipindua nchi wananchi tutawaunga mkono wangekaa kimya tu. Tumechoka kutawaliwa na hiki chama kwa shuruti, kinachokaa madarakani kwa mbeleko ya vyombo vya dola.
Umechoka we na nani?? Jisemee nafsi yako ukichoka lala!!
 
Hakuna mwanadamu anayestahili kumuua mwanadamu mwingine...

Umenukuu maneno ambayo, Mungu alitamka ya kwamba Adam na Hawa watakufa, na wala hakusema kwamba atawaua...
Kwani mtu hata akifa kalala,huwa kauawa na nani Kama siyo Mungu!?..mwanadam aliyeua mwenzie anapaswa kuuawa ili wengine wahofu kuua wenzao,siyo unajua halafu unaendelea kuning'iniza kengele na mtindi duniani
 
Aliposema" Sijawahi kuona raisi wa ajabu kiasi hiki, " na lugha ya matope, Ni sawa tu na kutangaza mapinduzi.
 
Kwanini aangushwe
Kwanini apinduliwe.. Kuna shida gani kwani?
Hivi mtu anayetaka kufanya hivyo anatangaza hadharani kweli? Kama kuna kosa limefanyika basi ni kuwakamata wakosoaji na kuwasweka ndani huku mkiwabambikia makosa makubwa ya uongo yalioongozwa na hisia zaidi..

Wale jamaa labda wafie huko waliko.. Maana wakitoka....

Sent using Jamii Forums mobile app
Wale hawafi na watatoka mapema sana kabla 2025 ila Tanzia kubwa itakuwepo Mungu amechukia dhuluma
 
Weka ushahidi hapa, kama yeyote kati ya Adv. Mwabukusi, Mdude, au Dr. Slaa akitamka hayo maneno Rais apinduliwe, usilete porojo za kitoto hapa..
Ushahidi kwa Dr Slaa huu hapa
 
Kwanini aangushwe
Kwanini apinduliwe.. Kuna shida gani kwani?
Hivi mtu anayetaka kufanya hivyo anatangaza hadharani kweli? Kama kuna kosa limefanyika basi ni kuwakamata wakosoaji na kuwasweka ndani huku mkiwabambikia makosa makubwa ya uongo yalioongozwa na hisia zaidi..

Wale jamaa labda wafie huko waliko.. Maana wakitoka....

Sent using Jamii Forums mobile app
"Ukicheka na nyani utavuna mabuwa". Hawa mapimbi walikuwa wanahamasisha civil unrest. Labda Mshana Jr hujawahi kuwasikia kule Club house na Mariaspsce.

Waliiuwa wanapnga kwananunukia vipazia sauti hadi vijana wa kwenye vijiweni ili wasikikize na wahamasike na harakati zao za kutaka kuipindua serikali.

Serikali imechelewa sana ku DEAL na wahuni hawa
 
Na ushahidi wa uhaini sio kutamka tu. Kupindua hadi kuprove dhamira lazima uwepo ushahidi. Kuwepo mipango maandalizi silaha etc. Kesi dhidi ya dr slaa inaweza sanasana kua uchochezi ambayo angeshinda kirahisi. Mwenyewe nilisikia amesema serikali isiyo sikivu hatua extreme ni kuipindua.
Binafsi nilisema waarabu watatuchochea kutengana. Watapandikiza udini ubara na uzanzibari maana ni hodari kuhonga. Wao mradi wapate wanachotaka. Samia ashauriwe aachane na hii mambo ya bandari. Sijui hizi sera anatoa wapi maana ccm bado rasmi ni chama cha kulinda maslahi ya umma.
Kama neno kupindua wanaikubali pia wakubali neno serikali isiyosikivu
 
Namkosoaga sana Tundu Antipas Lissu ila kwenye eneo ambalo nakiri na nasema ukweli ni kwamba Tundu Antipas Lissu ni mwanasheria smart sana.

Tundu Lissu anajua sheria hasa, kwenye maneno yake anapima kila kitu anachoongea kwenye mizani ya sheria ndo mana hata kumkamata kisheria ni ngumu sana.

Uhaini ni shtaka zito sana. Ndo shtaka lenye adhabu ya kifo tangu dunia iumbwe.

Walianza Adamu na Hawa ambapo Mungu aliwaambia mtakufa hakika maana waliamini wakila tunda la mti wa kati watakuwa kama Mungu.

Kwa maneno wanayosema Slaa, Mdude na Mwabukusi eti tutaiangusha Serikali ya Samia , eti tutaipindua kamwe huwezi kusikia hayo maneno akiyatamka mwanasheria makini Tundu Antipas Lissu.

Ushauri wangu kwa ufipa. Kamwe wenye akili hawasemagi tutapindua Serikali.

Kulitamka hilo neno tu ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 39 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.
Watapinduliwa tu. Ipo siku yao.
 
Back
Top Bottom