GE2025 Lissu hapiganii Watanzania anapigania maslahi yake

GE2025 Lissu hapiganii Watanzania anapigania maslahi yake

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Lissu[TAL] huyu sioni kama anapigania Watanzania bali namtazama kama mtu anaye pigania maslahi yake.

Maslahi yake ndio yanagonganisha interest zake na za watawala jambo linalo muweka matatizoni muda wote mpaka sasa.

Huwezi kuniambia kuwa Lissu anapigana Watanzania watu wasio na habari hata anachopigania, watu wasiojali yupo wapi ? anafanya nini ?anaishi mazingira gani ? anapitia shida au raha gani ?

Kwa ufupi ni kuwa sijaona mahali Watanzania wamemtuma Lissu awapiganie kuhusu shida zao hizi na hizi nachoona ni harakati zake binafsi zinagongesha maslahi yake na watawala sehemu moja.

Kumbuka hakuna mahali pagumu pa kufanya siasa za harakati kama Afrika tena katika nchi ya Tanzania.

Kama kuna watu wanafikiri kuwa Tundu Lissu anapigania Watanzania watu wasiotaka kupiganiwa na yoyote wao wapo busy na simba na yanga,diamond na zuchu watakuwa wanakosea sana.

Mdude katekwa hakuna anayejali kuhusu Mdude huku mkewe kaachiwa msimba mzito na mtoto mdogo asiyejua mahali Baba alipo Watanzania tupo busy na sajili za Simba na Yanga.
Kama sisiemu wangekua na maslahinna watu Huyo Mdude angetekwaje? Unadhani TAL akitaka kulamba asali kama wengine nani atakaeumia? Kuweni na heshima na watu waliochagua kutetea maslahi yenu mkiwa mitandaoni mmejificha nakutoa maoni huku hamna mchango wowote kwa Taifa zaidi yakuwa wapambe
 
Uraisi ni ajira, uwaziri ni ajira,ubunge pia ni ajira halikadhalika udiwani na mengineyo.
 
Kama maslahi yake si angemfuata Mbowe kuchukua pesa kwa Abdul
 
BAO lililokuzaa ww bora Mshua wako angepiga TONYE
 
Ndiyo mnavyodanganyana huko Lumumba, haya endeleni kushupata shingo - muwe tayari kuyanywa.
 
Back
Top Bottom