Pre GE2025 Lissu jitokeze ukanushe habari za Msigwa kugharamia Press ya kutangaza nia, vinginevyo umekwisha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Atajitokeza mara ngapi kwa kila uzushi jaribu basi kutumia akili hata kisoda
 

View: https://www.instagram.com/reel/DDjJCL0twP-/?igsh=cXZrNDFldTA2MnRr
 
Lissu amesema kuwa mojawapo ya dosari kubwa katika CHADEMA ni kutokuwa wazi katika mapato na matumizi yake. Kwa sababu hiyo anapaswa kuweka wazi alichokusanya na nani aliyemchangia na ametumia vipi nchango huo huo. Hivyo hivyo kwenye mchango wa gari lake. Ama sivyo ataonekana kuwa ni wale wale wanaosema hili lakini wanatenda hivi. Kalizua hili mwenyewe na atakiwa kujibu.

Amandla...
 
Uko sahihi kabisa, nia ya thread ni kutaka hizo allegations zijibiwe na kufutika ili hisia chafu zisiwepo lakini humu ndani kwa vile idadi kubwa wanaendeshwa na mihemko badala ya akili wanadhani ametuhumiwa na mleta mada.
Kwa taarifa ni kuwa hapa anaungwa mkono Lissu kwa hatua yake na kinachofanyika ni kumlinda yeye.
Hoja ya kuwa Msingwa hana hela sio hoja, maana hata kama ametumwa kuratibu tuu ni kosa kubwa la kimkakati kwa timu ya Lissu.
 
Acha hizo

Mchungaji Msigwa ana madeni kibao ambayo analipiwa kidogo kidogo na ASAS Misasa

Kwa Sababu unaishi machame basi unadhani ukumbi wa Mlimani City ni wa gharama sana

Hapo tunafanyiaga sherehe za komunio ya kwanza 😀😀
Umepiga kwenye mshono
 
Ungekuja na uthibitisho wa miamala inayoonyesha lisu katumiwa fedha na msigwa na baada ya hapo ungetaka lisu ajibu

Huna ushahidi wowote ajibu nini ni kama unarusha jiwe gizani
 
Alichangiwa na Wadau SAUTi ya watanzania na watu wengine Baki ...sio msigwa
 
Sasa kila lisemwalo ajitokeze kukanusha ataweza kweli????
Ukiwa kiongozi huwezi ukawa unamjibu kila mtu alizike.
Huwezi kunfurahisha kila kiumbe.
#CRITICAL THINKER.
 
Ungekuja na uthibitisho wa miamala inayoonyesha lisu katumiwa fedha na msigwa na baada ya hapo ungetaka lisu ajibu

Huna ushahidi wowote ajibu nini ni kama unarusha jiwe gizani
Samahani nikisema huna akili ingawa ni kweli. Mimi ndiye nimesema? Nimemwambia awajibu wasemao hivyo ili uvumi huo usiendelee unaniuliza mie ushahidi? Usiukubali ukilaza ukakuzoea na kukuganda!
 
Miye nilivyoona Msigwa nikajua Msigwa msemajj wa Serikali kumbe Msigwa Pastor? Mwenyewe huko CCM tegemezi labda kama huyo ndugu yake Msigwa msemajj ndio kapenyeza huo msaada kupitia kwa Pastor
 
Lissu amekuwa mbunge na wakili Tanzania hii miaka kadhaa, hawezi kukosa pesa ya kukodi kijiukumbi mlimani city , Lissu ni wa kimataifa.

Mwambieni mbowe aachie uenyekiti, kila mwanachama wa chadema yuko na haki sawa na uwezo wa kuwa mwenye kiti, hilo la kusema ohh mbowe ndo anafaa sijui akitoka chama kitakuwa vile ni njaa za wapambe wake.

20yrs ni mingi sana, nini atafanya ambacho hajawahi fanya? Hana jipya zaidi ya kupiga pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…