Tetesi: Lissu kukutana na viongozi waandamizi wa Ulaya

Tetesi: Lissu kukutana na viongozi waandamizi wa Ulaya

Mhe. Tundu Lissu anatarajia kukutana na viongozi waandamizi wa ulaya siku tatu zijazo, viongozi hao ni Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Katibu Mkuu wa umoja wa ulaya pamoja na Spika wa bunge la ulaya.. NTAENDELEA KUWAJUZA
Kwa kweli nilikuwa najiuliza kwa nini lissu apelekwe ubelgiji badala ya nchi nyingine mahiri kwa utabibu wa binadamu, kumbe ni mbinu nyingine ya kwenda jumuia ya ulaya kwa mgongo wa matibabu?
Hao wabelgiji si ndio walimuua Patrice Lumumba wa Congo kwa kumyeyusha na acid au?
Poor politics za cdm hadi mnatukera wapiga kura.
 
sizonje na bashite matumbo joto. unyama wao wote hadharani
 
Tanzania sio salama kuishi ukilinganisha na nchi gani? Mwanzo nilijisikia vibaya kwa uhuni alio fanyiwa na attempt ya kumuua iliyo shindwa, lakini huku anapo elekea siko. Huwezi kuwa unawaza kuisema nchi tena ugenini. Huko Ulaya au nchi zingine si kwamba hakuna madhaifu, lakini wakienda nje wanaeleza mazuri, madhaifu wanabanana humo kuyashughulikia. Hakuna nchi inaongoza kupigwa watu risasi hovyo kama US , lakini hutasikia CNN au vyombo vyao vingine vikitangaza hayo!!!! Tundu lissu ni janga, kama vipi aishie huko huko ahamie, huu ni uhaini, akirudi hapa atubu au amalizwe!!! Shabaash
Vipi ungelikuwa ni wewe umemiminiwa risasi zile,alafu ukawa unaishuku serikali kama alivyoeleza,alafu ukakutana na viongozi tunaoelezwa hapa kuwa atakutana nao,ungewaeleza nini?ungeliwambia Tanzania ni nchi safi kabisa?.
 
Kwa hiyo siasa za ndani zimewashinda mnategemea wazungu waiwekee vikwazo Tz na ninyi ndo mtokee hapo? Poor you..!Wazungu ni werevu na wana maslahi endelevu kwa nchi zao.Wale wanawasiliana na serikali kwa jambo lolote na usifikiri atakachotapila Lissu ndiyo kitakuwa final..thubutu..fanyeni kazi za kujiletea maendeleo na si kama fisi kusubiri mkono wa binadamu udondoke..

Sijui ulikuwa na umri gani wakati tulipokuwa tunashupalia akina John Foster (Balthazaar Johannes Vorster in Afrikaans) na Botha wawekewe vikwazo na mataifa hayohayo? Kwa kiasi fulani tulifanikiwa na South Africa ya leo sio ile ya Foster!
 
Alianza kuisema Tanzania akiwa Kenya. Anaona hajatosheka anatutangazishia ubaya mpaka huko alipo. Lengo lake liko kwenye jumuia ya kimataifa itutenge. Mwisho wa siku yy ndiye atakayeonekana mchawi
Nadhani yeye anahubiri alichotendewa.
 
Sijasema Mimi nitakua hai, Mimi na wewe tutakufa , Tanzania itabaki. Huyu mpuuzi anaidhalilisha Tz nje ya mipaka yake, aondolewe tu
Kwa hiyo mlipotaka kumtoa uhai mlidhani si binadamu kama nyinyi. Aliwasema mjirekebishe akiwa ndani mkaona mmtoe huai lakini Mungu akamlinda sasa mnaona aibu gani kusemwa nje kama ndani mmerekebishwa mkashindikana. Acha kutoa uahi wa watu jengeni nchi kwa mashirikiano siyo kujitenga na kila mkikosorewa mnatumia mtutu au mnapoteza watu au kama si hivyo mnaua na kutupa bahari kwenye mifuko. Tafuteni suruhu watu wote tukae na kujenga nchi, siyo badala ya kujenga viwanda mmekalia kununua wabunge na madiwani. Tangulizeni uzalendo acha kuweweseka
 
Alianza kuisema Tanzania akiwa Kenya. Anaona hajatosheka anatutangazishia ubaya mpaka huko alipo. Lengo lake liko kwenye jumuia ya kimataifa itutenge. Mwisho wa siku yy ndiye atakayeonekana mchawi
Kwa hiyo mlipotaka kumtoa uhai mlidhani si binadamu kama nyinyi. Aliwasema mjirekebishe akiwa ndani mkaona mmtoe huai lakini Mungu akamlinda sasa mnaona aibu gani kusemwa nje kama ndani mmerekebishwa mkashindikana. Acha kutoa uahi wa watu jengeni nchi kwa mashirikiano siyo kujitenga na kila mkikosorewa mnatumia mtutu au mnapoteza watu au kama si hivyo mnaua na kutupa bahari kwenye mifuko. Tafuteni suruhu watu wote tukae na kujenga nchi, siyo badala ya kujenga viwanda mmekalia kununua wabunge na madiwani. Tangulizeni uzalendo acha kuweweseka
 
Kwa kweli nilikuwa najiuliza kwa nini lissu apelekwe ubelgiji badala ya nchi nyingine mahiri kwa utabibu wa binadamu, kumbe ni mbinu nyingine ya kwenda jumuia ya ulaya kwa mgongo wa matibabu?
Hao wabelgiji si ndio walimuua Patrice Lumumba wa Congo kwa kumyeyusha na acid au?
Poor politics za cdm hadi mnatukera wapiga kura.
Wapigakura wapi?hawa waliogoma kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa marudio baada ya CHADEMA kujitoa?.
 
Hivi jamani, ni mimi tu sielewi au?! Maana mimi naona hii ni tetesi tu kuwa Lissu atakutana na hao viongozi....ajabu kuna watu wanalaani na lawama kibao! Kwani kuna mpiga ramli amewaambieni kuwa watajadili nini?! Na kuna jamaa hapo juu kauliza kuwa Lissu anakutana nao kama nani! Kweli?! Hata tukiacha mengine yote, si ana uhuru wa kukutana nao kama mwanadamu aliyeshambuliwa kwa risasi zote hizo lakini Mungu akamponya?
 
Mhe. Tundu Lissu anatarajia kukutana na viongozi waandamizi wa ulaya siku tatu zijazo, viongozi hao ni Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Katibu Mkuu wa umoja wa ulaya pamoja na Spika wa bunge la ulaya.. NTAENDELEA KUWAJUZA
Kama alishindwa wakati yupo mzima alipopiga kambi bunge la ulaya kwa wiki mbili,kwa sasa ni kama wanaenda kumuona mgonjwa na kumpa pole tu
 
Back
Top Bottom