Uchaguzi 2020 Lissu, kuna kila dalili wenye CHADEMA yao hawakutaki ugombee urais, kama vipi twen'zetu ACT Wazalendo

Uchaguzi 2020 Lissu, kuna kila dalili wenye CHADEMA yao hawakutaki ugombee urais, kama vipi twen'zetu ACT Wazalendo

Yaani kama na hili unaliamzishia Uzi basi naanza kuwa na shaka na nyuzi zako. Jipe muda wa kupembua utaona kilicho mbele.
 
Kale kagenge ndani ya CHADEMA kanaendelea na kazi ya kumshughulikia Lissu. Msikilize Lema.

Maneno haya ndio wanayoambiwa wajumbe wa mkutano Mkuu wa Chama kwa sasa
View attachment 1480627

Lifanyikalo gizani linawekwa hadharani

Lissu akiisikia clip hii inabidi akae afikirie mara mbilimbili

Kama alidhani ana baraka za uongozi wa Chadema kupeperusha bendera ya chsma hicho kwenye uraisi basi ajipange upya. This is not the case!
 
Sisi sio Kama ccm hata angechukua fomu pekeake angepigiwa kura za Ndio/hapana Kama kwa Sumaye uchaguzi uliopita.

Vipi na Lowasa mlimpigia hizo kura za NDIYO/HAPANA 2015?
 
Kweli kabisa

Yani hata Lissu kichwa kinauma sana

Sio kwamba hayaoni, anayaona sana, hana namna
Hizo ndiyo mbinu zenu zilizobaki wanaccm.....

Mmekuwa wapiga ramli tu.......

Huko kwenu CCM ndiyo Jiwe pekee keshapitishwa......

Wapambe wanaendelea kumsifu na kumuabudu hadi wanakufuru na kumfananisha na Yesu Mwokozi!
 
Chadema hawawezi kumuweka mbele Lissu peke yake ikiwa kuna hatari akasumbuliwa kkurudi , muda ukifika watajitoa wengine na huenda mgombea akawa Lissu au Nyalandu
 
Wewe huoni kuwa badala ya sasa kumpa ushirikiano mtu anayeweza kumchallenge Magufuli wao wanaanza kujifanya wanachokua fomu na kuwachelewesha wananchi kuungana nyuma ya mtu anayeweza kumchallenge Magufuli?
Mbona unataka kushuka kabla ndege haijasimama.Yaani watu wako kwenye hatua za awali kabisa za watu kutangaza nia wewe umeshaanza kusema mambo yasiyoeleweka.Unataka ushirikiano gani sasa kwenye hatua hiyo.
 
Angalizo kwenye post yako namba moja ni zuri, ila umeongea maneno mengi mpaka hata kama ulikuwa na nia njema unaanza kutia shaka. Mimi binafsi sikutegemea kuwa Mbowe naye atatia nia ya kugombea urais. Ni kweli Mbowe anaweza kuwa na ushawishi mkubwa kwa baadhi ya watu ndani ya cdm. Lakini ni ukweli usioacha shaka, kuwa Lissu ndio mwenye mvuto wa kweli kwa wapiga kura wengi kuliko mgombea yoyote ndani ya cdm...

Kesi siyo kigezo cha kumzuia mgombea wa Chadema kugombea iwapo chama kitarally behind him.

Kitendo cha kuwapa CCM option kuwa Chadema ina wasiwasi na ugombea wa Lissu kitawafanya CCM wamshughulikie Lissu kweli kupitia mahakama. Lakini kama Chsdema itasema kuwa huyu ndo mgombea pekee tuliye naye hatuna mwingine, basi serikali ya CCM haitomshughulikia kwa sababu kufanya hivyo kutaondoa credibility ya zoezi zima la uchaguzi kitu ambacho Magufuli anakiogopa sana,

ili aweze kupata mikopo ma misaada nje ya nchi na kujaribu kujenga taswira kuwa alishinda kihalali na hivyo hatamshughulikia Lissu kumdiscredit kugombea.. Lakini hili linawezekana tu kama chama kitatuma meseji kuanzia sasa kuwa huyu ndo likely candidate wao!

Ila Chadema wakionyesha wasiwasi kwenye candidacy ya Lissu basi serikali ya CCM itacapitalize ktk hilo kumshughulikia kweli
 
Missile of the Nation CHADEMA imepita ktk mapito mengi mno, kwa wanazichanga karata zao kwa umakini mno. Sidhani kama Mwenyekiti na Makamu wake wanaweza kukosa umakini kwa wakati mmoja na kuingia kwenye kinyang'anyiro cha nafasi ya uraisi bila ya kushauriana pamoja.
 
Missile of the Nation,
LOooo, nimeshindwa kufika mwisho wa makala.

Hebu kwanza nikuulize, huko ACT-Wazalendo wewe ni nani?

Hilo swali ni pana sana, na ukitaka kulijibu jitahidi kulielewa vizuri.

Sitaki kukuchanganya kwa kuweka ufafanuzi juu ya hayo niliyosoma kwenye mada yako mwanzo hadi nilipoishia katikati.

Maadui wa ukombozi hujitokeza kwa njia mbalimbali, hata wakati wanapojinadi kuwa wapo pamoja na wapambanaji.
 
Wewe huoni kuwa badala ya sasa kumpa ushirikiano mtu anayeweza kumchallenge Magufuli wao wanaanza kujifanya wanachokua fomu na kuwachelewesha wananchi kuungana nyuma ya mtu anayeweza kumchallenge Magufuli?
Hayo ni mambo ya ndani ya chama. Atakayepita utaona chama chote kiko naye.
Mbona mnateseka hivi? Malizaneni na Membe kwanza huko kwenu tukutane kwenye kampeni.
Mwaka huu mtaruka samasoti hadi kuchama msamba!
 
Lissu alishasema chama wakinipa nafasi ya kupepeprusha bendera.Sisi sio Kama ccm hata angechukua fomu pekeake angepigiwa kura za Ndio/hapana Kama kwa Sumaye uchaguzi uliopita.Kwa hiyo wengi kuchukua fomu haimaanishi kwamba hawamtaki Lissu Wala Mwenyekiti kuchukua fomu haimaanishi Lissu hakubariki.Hii Ndio demokrasia nanhata nafasi za ubunge wa ndani Kuna wabunge ambao huwadhanii wanaweza kupigwa chini kutokana na Sina ya watu wakakao wachallenge kwenye majimbo.

ACT wazalendo pia Wana nafasi ya kusimamisha mgombea wakitaka Ila sio Lissu.Lissu hahami kwenda popote.Lissu anaweza kugombea Tena Cha CDM miaka mitano ijayo.Usitake kuleta siasa za uchonganishi hapa
Nazidi kukubaliana na maoninya mtoa mada.
 
Huwa na mashaka sana na wewe kama kweli unataka kuona upinzani nchi hii unaimarika.
Mbona huyo anaeleweka vizuri toka mwanzo wake humu JF.

Tatizo ni kwamba kumbukumbu kwa wengi, kama ilivyo 'usahaulifu' kwa waTanzania wengi ndio shida.
 
Wewe huoni kuwa badala ya sasa kumpa ushirikiano mtu anayeweza kumchallenge Magufuli wao wanaanza kujifanya wanachokua fomu na kuwachelewesha wananchi kuungana nyuma ya mtu anayeweza kumchallenge Magufuli?
Kwani kuchukua fomu ndio hatua ya mwisho?
 
Kila dalili ndani ya Chadema zinajionyesha, brother Lissu wenye Chadema yao hawakutaki ugombee urais kupitia chama hicho. Wangekutaka wangekupa hata signal ya kuwa wako nyuma yako katika kinyang'anyiro hiki.

Kuna sauti mitandaoni Godbless Lema anasema "umeanza kujiweka katika tune ya ugombea urais", yaani umeshaanza kujiaminisha kuwa wewe ni mgombea, hii ni dalili ya kwanza kwamba brother bado hauna baraka za wenye chama chao kugombea.

Pili, kitendo cha Mwenyekiti kuchukua fomu wakati tunajua by all means hana nia ya urais, sisi tunajua na yeye anajua, inalenga kufanya mahesabu yako ndani ya Chadema kupata hiyo nafasi kuwa ngumu, maana kiukweli mwenyekiti anaungwa mkono kuliko wewe ndani ya Chama, na there is no way unaweza kumshinda mbele ya wajumbe kwenye mkutano mkuu.

Kitendo cha Msingwa naye kuchukua fomu wakati naye tunafahamu fika hawezi kumchallenge Magufuli head on ni dhahiri umewekwa mtu kati, chance zako za kuwa mgombea zimeminywa kutokana na move hizi tunazoziona.

Nguvu zilezie zilizoamua Dr Slaa asiwe mgombea mwaka 2015 unfortunately ndiyo hizo hizo it seems zinataka usigombee this time.

Wewe Lissu, watu wana biashara zao, wana mipango yao ya hela pembeni, wengine siasa ni mtaji, unadhani wakipewa dili wakuzuie usigombee wanaumia chochote?

Aisee utakatwa kupitia mchakato feki ndani ya chama utakaopewa jina la demokrasia na wewe utashangaa!

Sisi wananchi tunajua wewe na Membe ndiyo mlioutaka Urais mapema kabisa na tunawajua na tunaamini. mmoja kati yenu ndo angeweza kumchallenge jiwe, Yaani Membe ndani ya CCM na wewe nje ya CCM.

Karata ya Membe huko CCM imeshatolewa mchezoni kimafia, umebaki wewe nje ya CCM. na lazima uchezewe mchezo uleule lakini hukohuko ndani ya upinzani! Kuna kitu kigumu mbele ya Fedha?

Sasa jiandae, kama unautaka Urais uwe tayari kushusha Tanga na kupandisha Tanga kwa kwenda ACT.

Kuna kila dalili ya wenye Chadema yao kwenye chama chako hawajawa na msimamo kuwa wewe uwe mgombea!

Endelea kujipanga na ujiandae kisaikolojia. Wewe unaweza kuwa real, lakini kuna baadhi ya watu uchaguzi ni dili.
Hiyo ACT unayomshauri TL kuhamia, mbona imo kundi moja na TLP, CUF, na vile vingine vinavyomilikiwa na sisiemu??
 
Back
Top Bottom