Uchaguzi 2020 Lissu, kuna kila dalili wenye CHADEMA yao hawakutaki ugombee urais, kama vipi twen'zetu ACT Wazalendo

Uchaguzi 2020 Lissu, kuna kila dalili wenye CHADEMA yao hawakutaki ugombee urais, kama vipi twen'zetu ACT Wazalendo

Mimi ninafikiri wanachukua fomu ili kuleta taswira ya kuwa kuna ushindani ndani ya chama, Ila mgombea ni Lissu. Wana-prove siasa za ushindani & siasa safi.
Kwa mtazamo wangu pia umemaliza mkuuu
 
Lissu alishasema chama wakinipa nafasi ya kupepeprusha bendera.Sisi sio Kama ccm hata angechukua fomu pekeake angepigiwa kura za Ndio/hapana Kama kwa Sumaye uchaguzi uliopita.Kwa hiyo wengi kuchukua fomu haimaanishi kwamba hawamtaki Lissu Wala Mwenyekiti kuchukua fomu haimaanishi Lissu hakubariki.Hii Ndio demokrasia nanhata nafasi za ubunge wa ndani Kuna wabunge ambao huwadhanii wanaweza kupigwa chini kutokana na Sina ya watu wakakao wachallenge kwenye majimbo.

ACT wazalendo pia Wana nafasi ya kusimamisha mgombea wakitaka Ila sio Lissu.Lissu hahami kwenda popote.Lissu anaweza kugombea Tena Cha CDM miaka mitano ijayo.Usitake kuleta siasa za uchonganishi hapa
Lowasa alipigiwa kura mzee baba /mama?
 
Kila dalili ndani ya Chadema zinajionyesha, brother Lissu wenye Chadema yao hawakutaki ugombee urais kupitia chama hicho. Wangekutaka wangekupa hata signal ya kuwa wako nyuma yako katika kinyang'anyiro hiki.

Kuna sauti mitandaoni Godbless Lema anasema "umeanza kujiweka katika tune ya ugombea urais", yaani umeshaanza kujiaminisha kuwa wewe ni mgombea, hii ni dalili ya kwanza kwamba brother bado hauna baraka za wenye chama chao kugombea..
HUELEWI MCHEZO WANAOCHEZA CHADEMA , BAADAE NDIO UTAJUA KWA NINI WENGINE WALICHUKUA FORM ZA URAIS
 
Mimi nalitizama kwa jicho tofauti. Naona tu CDM wameamua kuwa prudent. CDM ikimsimamisha Lissu, kuna watu wanaumia sana...wanaogopa! Kwa hivyo upo uwezekano mkubwa wa kujaribu kumzuia Lissu asigombee.....wanaweza hata kumkamata na kumfungukia mashataka ya kutakatisha fedha au uhujumu uchumi (hata kama hakuna ushahidi kabisa) na kumnyima dhamana ili kumkwamisha. Kwa hivyo ni muhimu CDM ikawa na Plan B.

Nadharia nyingine ni kujaribu tu kujenga legitimacy kwa Lissu..... ..tuseme chama kinajua kitampitisha lakini kinataka kuonesha uwepo wa demokrasia lakini pia kumpa Lissu kujiamini zaidi.

Kuna vyama vingine ukionesha hata dalili tu ya kuwa unaweza kutia nia ya kugombea urais, wanakuvua uanachama!
 
Hayo ni mambo ya ndani ya chama. Atakayepita utaona chama chote kiko naye.
Mbona mnateseka hivi? Malizaneni na Membe kwanza huko kwenu tukutane kwenye kampeni.
Mwaka huu mtaruka samasoti hadi kuchama msamba!
Huku kufarijiana Mkuu,,, mimi MWANA Chadema Damu na Mifupa,,,,Picha lishaonekana Lissu hatakiwi CHADEMA,,ANATAKIWA NYALANDU AU MBOWE,,,,,,Ila wote hawauziki kama. TUNDU ANTIPAS LISSU,,,Tena NYALANDU ndo mweupee kabisa ,,,,
 
Wale watu waliotaka kumuua lissu sasa itakuwaje?hawatataka kumalizia " kazi "?,je amemalizana nao? Maana wana sababu zilizofanya wampige risasi.mnawaza asimame na magufuli kwenye uchaguzi badala ya kuwaza usalama wake,mmeshasahau kwamba lissu ana kimeo... shauri yenu...
 
yaani CHADEMA wasipompitisha Lisu kitakuwa chama cha ajabu kupata kutokea duniani. Zito atajiokotea embe dodo chini ya muarobaini.
 
yaani CHADEMA wasipompitisha Lisu kitakuwa chama cha ajabu kupata kutokea duniani. Zito atajiokotea embe dodo chini ya muarobaini.
Lisu hatapitishwa chadema wamemuomba arudi nchini ili ashiriki mchakato na awe karibu na Wana chadema kakataa anasema apewe uteuzi wa uraisi kwanza ndio atarudi !!! Akina Mbowe wamegoma kushinikizwa na kuburuzwa na Lisu ndio maana wamechukua fomu hawatanii na Wala hawafanyi usanii wako serious ambaye hayuko serious Ni mchungaji msigwa tu
 
Kesi siyo kigezo cha kumzuia mgombea wa Chadema kugombea iwapo chama kitarally behind him.

Kitendo cha kuwapa CCM option kuwa Chadema ina wasiwasi na ugombea wa Lissu kitawafanya CCM wamshughulikie Lissu kweli kupitia mahakama. Lakini kama Chsdema itasema kuwa huyu ndo mgombea pekee tuliye naye hatuna mwingine, basi serikali ya CCM haitomshughulikia kwa sababu kufanya hivyo kutaondoa credibility ya zoezi zima la uchaguzi kitu ambacho Magufuli anakiogopa sana, ili aweze kupata mikopo ma misaada nje ya nchi na kujaribu kujenga taswira kuwa alishinda kihalali na hivyo hatamshughulikia Lissu kumdiscredit kugombea.. Lakini hili linawezekana tu kama chama kitatuma meseji kuanzia sasa kuwa huyu ndo likely candidate wao!

Ila Chadema wakionyesha wasiwasi kwenye candidacy ya Lissu basi serikali ya CCM itacapitalize ktk hilo kumshughulikia kweli

Acha ushawishi wa bei rahisi ww. Kama mnataka Lissu aende ACT akawang'rishie nyota, tumia mbinu nyingine na sio hizo nyepesi. Huko Act unakotaka Lissu aje agombee mbona hata huko Zanzibar ambako ina nguvu, bado wapiga kura wenu hawaandikishwi na hamna lolote mmefanya?

Hapo hakuna cha option yoyote wanayopewa ccm, bali Magufuli ndio muamuzi wa kila kitu na haogopi chochote. Ni kweli kuna wanaccm kadhaa wanajua madhara ya kukosa support ya nje, je Magufuli anajali hayo? Hata kama atafanya atakalo na nchi kuchukuliwa hatua, ni kipi anajali yeye binafsi? Ni hasara ngapi amelitia taifa hili na wala hajali?

Ni lini umemuona akijali matatizo ya watu mpaka useme nchi ikinyimwa misaada atajali? Hukijifunza alichofanya kwenye tetemeko la Kagera, kwenye korosho ameogopa nini? Labda nchi hii ivamiwe na hayo mataifa ya nje kama Libya wangalau ndio atajali, au yeye binafsi akamatwe kwenda jela ndio ataogopa, ndio maana kajiwekea kinga.

Lakini kusema eti anaogopa kukosa misaada yeye sio wa hivyo. Mfano wa kwamba haogopi,na hayo mataifa ya nje hayachukui hatua kwa haraka hivyo, muulize Maalim Seif alipoenda kushitaki huko nje kuporwa ushindi wa Zanzibar, kama kuna lolote limetokea.

Tafadhali nukushauri acha ushawishi wa kijinga, jenga ACT yako mpambane na hali yenu, na sio kusaka mwanachama kwa kuchafua taswira ya chama kingine.
 
Acha ushawishi wa bei rahisi ww. Kama mnataka Lissu aende ACT akawang'rishie nyota, tumia mbinu nyingine na sio hizo nyepesi. Huko Act unakotaka Lissu aje agombee mbona hata huko Zanzibar ambako ina nguvu, bado wapiga kura wenu hawaandikishwi na hamna lolote mmefanya?
Lisu mwenyewe alishaongea na Zitto kuwa Chadema wasipomteua ataenda kugombea ACT wazalendo

Yupo anasubiria tu maamuzi ya Chadema wakimpiga chini atimkie ACT wazalendo
 
Lisu mwenyewe alishaongea na Zitto kuwa Chadema wasipomteua ataenda kugombea ACT wazalendo

Yupo anasubiria tu maamuzi ya Chadema wakimpiga chini atimkie ACT wazalendo

Ni haki yake kwenda chama chochote, ila cdm ndio yenye wapiga kura wengi wa upinzani. Kwangu ninaamini Lissu ndio mgombea urais wa upinzani mwenye mvuto mkubwa kwa wapiga kura wa upinzani, tena akiwaacha wengine wote kwa mbali. Hilo wala halihitaji mjadala. Hapo ni suala la kuangalia kisheria imekaaje ili asikose nafasi.

Lakini sio Mbowe, Nyalandu, Msigwa au yule unknown women, wanaweza kuvuta hisia za wapiga kura wa upinzani. Wangalau Zito ambaye sio cdm ana mvuto wa kuridhisha, kutokana na uwezo wake wa kujenga hoja.
 
Ni haki yake kwenda chama chochote, ila cdm ndio yenye wapiga kura wengi wa upinzani. Kwangu ninaamini Lissu ndio mgombea urais wa upinzani mwenye mvuto mkubwa kwa wapiga kura wa upinzani, tena akiwaacha wengine wote kwa mbali. Hilo wala halihitaji mjadala. Hapo ni suala la kuangalia kisheria imekaaje ili asikose nafasi. Lakini sio Mbowe, Nyalandu, Msigwa au yule unknown women, wanaweza kuvuta hisia za wapiga kura wa upinzani. Wangalau Zito ambaye sio cdm ana mvuto wa kuridhisha, kutokana na uwezo wake wa kujenga hoja.
Jiandae tu kisaikolojia Lisu hatateuliwa na chadema Kuna issues nyingi Lisu kachemka
 
Angalizo kwenye post yako namba moja ni zuri, ila umeongea maneno mengi mpaka hata kama ulikuwa na nia njema unaanza kutia shaka. Mimi binafsi sikutegemea kuwa Mbowe naye atatia nia ya kugombea urais. Ni kweli Mbowe anaweza kuwa na ushawishi mkubwa kwa baadhi ya watu ndani ya cdm. Lakini ni ukweli usioacha shaka, kuwa Lissu ndio mwenye mvuto wa kweli kwa wapiga kura wengi kuliko mgombea yoyote ndani ya cdm...
Mimi natamani aje wakati ameshateuliwa kugombea urais na kampeni zinaanza Kama kesho tuone wa kumkamta?hao CCM sometimes mnawapa sifa wasizostahili na ndo maana wanaharibu nchi yetu
 
Mleta mada siasa unaichukulia urahisi sana. Siasa ni propaganda, vp kama Lisu katangaza hiyo nia ili kupandisha pressure na kupima mapokeo kwa Ccm? .

Lissu kasema anajadiliana na wadau ili wamhakikishie usalama ndipo aje, vp kama hatoweza rejea sbb za kiusalama je cdm wasiwe na mgonbea? je vp kama chama kinataka kionyeshe kuwa kuna demokrasia?
 
Kila dalili ndani ya Chadema zinajionyesha, brother Lissu wenye Chadema yao hawakutaki ugombee urais kupitia chama hicho. Wangekutaka wangekupa hata signal ya kuwa wako nyuma yako katika kinyang'anyiro hiki.

Kuna sauti mitandaoni Godbless Lema anasema "umeanza kujiweka katika tune ya ugombea urais", yaani umeshaanza kujiaminisha kuwa wewe ni mgombea, hii ni dalili ya kwanza kwamba brother bado hauna baraka za wenye chama chao kugombea.

Pili, kitendo cha Mwenyekiti kuchukua fomu wakati tunajua by all means hana nia ya urais, sisi tunajua na yeye anajua, inalenga kufanya mahesabu yako ndani ya Chadema kupata hiyo nafasi kuwa ngumu, maana kiukweli mwenyekiti anaungwa mkono kuliko wewe ndani ya Chama, na there is no way unaweza kumshinda mbele ya wajumbe kwenye mkutano mkuu.

Kitendo cha Msingwa naye kuchukua fomu wakati naye tunafahamu fika hawezi kumchallenge Magufuli head on ni dhahiri umewekwa mtu kati, chance zako za kuwa mgombea zimeminywa kutokana na move hizi tunazoziona.

Nguvu zilezie zilizoamua Dr Slaa asiwe mgombea mwaka 2015 unfortunately ndiyo hizo hizo it seems zinataka usigombee this time.

Wewe Lissu, watu wana biashara zao, wana mipango yao ya hela pembeni, wengine siasa ni mtaji, unadhani wakipewa dili wakuzuie usigombee wanaumia chochote?

Aisee utakatwa kupitia mchakato feki ndani ya chama utakaopewa jina la demokrasia na wewe utashangaa!

Sisi wananchi tunajua wewe na Membe ndiyo mlioutaka Urais mapema kabisa na tunawajua na tunaamini. mmoja kati yenu ndo angeweza kumchallenge jiwe, Yaani Membe ndani ya CCM na wewe nje ya CCM.

Karata ya Membe huko CCM imeshatolewa mchezoni kimafia, umebaki wewe nje ya CCM. na lazima uchezewe mchezo uleule lakini hukohuko ndani ya upinzani! Kuna kitu kigumu mbele ya Fedha?

Sasa jiandae, kama unautaka Urais uwe tayari kushusha Tanga na kupandisha Tanga kwa kwenda ACT.

Kuna kila dalili ya wenye Chadema yao kwenye chama chako hawajawa na msimamo kuwa wewe uwe mgombea!

Endelea kujipanga na ujiandae kisaikolojia. Wewe unaweza kuwa real, lakini kuna baadhi ya watu uchaguzi ni dili.
Ukweli mchungu
 
Back
Top Bottom