Tetesi: Lissu kuongoza jopo la mawakili 29 kumtetea Bi. Fatuma Karume

Tetesi: Lissu kuongoza jopo la mawakili 29 kumtetea Bi. Fatuma Karume

Rais wa chama cha wanasheria nchini na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ataongoza jopo la mawakili 29 watakaomtetea Wakili Fatma Karume Katika Kesi Yake Ya Kushikwa Mwili Wake Bila Ya Ridhaa, Kuvutwa Kwa Nguvu Na Kusababishiwa Madhara Katika Bega Lake.
Katika Kesi Hiyo Iliyofunguliwa Mahakama Kuu Ya Tanzania, Bi.Fatma Anamdai Fidia Ya Shilingi Bilioni Moja, Inspekta Eugen Mwampondela Wa Kituo Kikuu Cha Polisi DSM.
Kesi Itakapoanza Kusikilizwa, Mtuhumiwa Atatakiwa Kuwepo Kizambani Kujieleza Na Kujibu Maswali.

My Take
Cross Examination za Tundu Lissu hazijawahi kumuacha askari salama
Unajua maana ya mtuhumiwa au unajiandikia tuu??
 
Huyo askari anatamani akafanye Plastic Surgery asijulikane.... Maana ni bonge la msiba
 
Abuse of proffession....Hivi polisi wakiamua kuwakamata ile kisawasawa watakuwa wazima kweli?

This is an abuse of Power not abuse of Poffession my friend!!
Polisi kwa kupewa kibri na Utawala hasa huu wa A5 wanatumia madaraka yao vibaya. Yaani Jeshi la Polisi wanafikiri kwa vile Magufuli wao yuko juu ya sheria basi na wao wanaweza kuwa juu ya sheria!!!Sasa ngoja ashikishwe adabu na itakuwa somo kwa Mapolisi wote wajingawajinga wanaofanya kazi zao bila kutumia weledi.
 
Abuse of proffession....Hivi polisi wakiamua kuwakamata ile kisawasawa watakuwa wazima kweli?
Kwani polisi wanaruhusuwa kuwakamata kwa nguvu? Amri toka juu ndizo huwafanya polisi kujiona wapo juu ya sheria, hii kesi itasaidia watanzania kutambua haki zao.
 
hao mawakili wapigane hii kesi irushwe live na sie ma bush lawyer tupate vi techniques vya kutambia mjini

maana tusha nyanyaswa sana, ni muda wa kutamba na sie
 
Rais wa chama cha wanasheria nchini na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ataongoza jopo la mawakili 29 watakaomtetea Wakili Fatma Karume Katika Kesi Yake Ya Kushikwa Mwili Wake Bila Ya Ridhaa, Kuvutwa Kwa Nguvu Na Kusababishiwa Madhara Katika Bega Lake.
Katika Kesi Hiyo Iliyofunguliwa Mahakama Kuu Ya Tanzania, Bi.Fatma Anamdai Fidia Ya Shilingi Bilioni Moja, Inspekta Eugen Mwampondela Wa Kituo Kikuu Cha Polisi DSM.
Kesi Itakapoanza Kusikilizwa, Mtuhumiwa Atatakiwa Kuwepo Kizambani Kujieleza Na Kujibu Maswali.

My Take
Cross Examination za Tundu Lissu hazijawahi kumuacha askari salama
nimeipenda sana hii

kula uliwe"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
aiseee.. hii haijawahi kutokea Tanzania, sasa wanaomtetea huyo mtesi ni wangapi?
 
Back
Top Bottom