Lissu, Lema na Maria Sarungi wana agenda nyingine?

Lissu, Lema na Maria Sarungi wana agenda nyingine?

Wanzania wa leo hawazai watoto wengi kama zamani; hasa mijini wanazaa watoto kigogo sana kati ya 2 hadi 4 tu. Hivyo, kuruhusu mtoto wao mmoja kujeruhiwa au kufa ni jambo ambalo hawataki kulisikia kabisa kwao.

Lissu, Lema, na Maria Sarungi nao pia wana watoto wachache sana kila mmoja, na wangependa asipotee hata mmoja kizembe au kwa bahati mbaya. Hii imewafanya watoto wao kuwaondoa hapa Tanzania ile wawe na uhakika wa 100% ya usalama wao na maisha yao. Watoto wa Lissu wako marekani na watoto wa Lema wako Canada na wale wa Maria nadhani wako Kenya.

Kuzuia uchaguzi usifanyike sio jambo la kawaida sio tu Tanzania, bali hata Afrika, Ulaya, Asia, marekani na duniani kote; na kama likitokea tukio kama hilo nadhani haliwezi kusababishwa na mtu mmoja, kikundi au taasisi moja tu bila kusababisha vurugu za kufa mtu kati ya dola na mtu/kikundi au taasisi hiyo. Tuwaombe akina Lissu, Lema na Maria wazirejeshe familia zao Tz siku ya uchaguzi waje wapige kura au wazuie uchaguzi pamoja na watoto wa wanachadema wenzao.

Nijuavyo mimi watanzania wengi na dola hawawezi kushindanisha amani na utulivu na Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi; Kwao amani na utulivu ni zaidi ya katiba mpya na tume huru; maana Kenya, Marekani, Ulaya, Ukraine, Urusi wana katiba nzuri na tume huru za uchaguzi lakini nao wanalalamika kura kuibiwa, watu kupotea, na wagombea kuhujumiwa pia. Ni tatizo la dunia linalohitaji mbinu na mjadala wa kitaifa, kikanda na kidunia badala ya Lisu, Lema na Maria kushawishi watoto wa watu wengine wazuie uchaguzi. Bila shaka ni mkakati ambao utazalisha majeruhi wengi sana wasiokuwa na idadi kamili itakayojulikana.

Wote tunajuwa kuwa Katiba yetu, Tume ya uchaguzi na chaguzi zetu bado sio za viwango vikubwa, lakini pia lazima tukubali pia hata vyama vyetu vya siasa bado havitoshi kwenda Ikulu kwa sasa; bado sanaaa. Tuendelee kujadiliana kama taifa kuwa na katiba mpya, tume huru na chaguzi huru kwa njia jumuishi na sio kiharakati zai kufungua njia, milango na madirisha ya watu kwenda Ikulu bila vikwazo.
Mwaka huu mtahara damu!! mamaye! yaani mnajamba jamba wakati ndiyo shughuli inaanza? Ni hivi hatuhitaji kutekwa tena kwa ajili uchafuzi wenu nyoko nyie!!
 
Yaani watoto wao wanakula pizza huko Marekani na Kanada, wanataka wa kwetu wadhurike?
kwani watoto wa mwigulu wanasoma kayumba? watoto wako wewe wanasoma wapi? kama kuishi nchini ndiyo kuwqa na uchungu au uzalendo kwa nchi vipi kuhusu ABDUL mbona anaishi DUBAI na siyo KIZIMKAZI?
Siasa za ki propaganda hizo
 
Watanzania wanajitambua hizo blah blah za amani zimepitwa na wakati by the way Tz hakuna amani Kuna uvumilivu na utulivu tu na wananchi wamechoka kuvumilia uozo.
Zina umuhimunsana tunaona Trump hekahrka zote watt wake anao je vp kwa hawa
 
Mwaka huu mtahara damu!! mamaye! yaani mnajamba jamba wakati ndiyo shughuli inaanza? Ni hivi hatuhitaji kutekwa tena kwa ajili uchafuzi wenu nyoko nyie!!
Ngoma inayolia sana usiiweke sana juani, maana mara zote ni ya kwanza kupasuka ikipata joto hata kidogo tu. Hivyo ngoma yenu inayotoa mlio sana msiiweke juani. Watanzania hawako tayari bado kulinganisha na kushindanisha kati ya amani/utulivu waliyonayo na demokrasia waliyonayo. Jambo hili lazima mlielewe kuwa watanzania wengi bado hawajakerwa na kiasi cha demokrasia ilyoko nchini. Wapeni muda waendelee kukomaa, itafika wakati hawatahitaji kushawishiwa saaana na viongozi.
 
kwani watoto wa mwigulu wanasoma kayumba? watoto wako wewe wanasoma wapi? kama kuishi nchini ndiyo kuwqa na uchungu au uzalendo kwa nchi vipi kuhusu ABDUL mbona anaishi DUBAI na siyo KIZIMKAZI?
Siasa za ki propaganda hizo
huyu Mama yake ni Rais, bila shaka hata mtoto wa Biden, Hunter huko Marekani alikuwa na fursa nyingi kuliko wengine.Yaani kaka mnatumia njia nyepesi sana kuwashawishi watu wafanye jambo kubwa sana na hatari kwa manufaa yenu. Mimi niliwahi kulinda kura za mgombea ambae siku ya siku alirejea CCM na ubunge wetu. Hakuna mtu anawaamini nyie sasa hivi.
 
Ni bahati mbaya tu kwamba wananchi wengi hawana uwezo wa kudadavua mambo kujua chimbuko hasa la shida zao. Wananchi wa Libya kwamfano, walifikiri chimbuko la shida zao ni Gadafi, wakamuondoa lakini kumbe walikosea; kule Kenya walidhani chanzo cha neema zao atakuwa Ruto, looh! wamekosea, kule Nigeria walidhani Tinubu atakuwa mwarobaini wa Boko haram na umaskini wao lakini kumbe sivyo, kule DRC walidhani kama Mobutu akiondoka maisha yatakuwa tambarare, Zimbabwe walidhani Mugabe ndio kikwazo chao lakini kumbe sio. malawi, zambia, uganda, nk hivyo hivyo, lakini hali zao zimezidi ama kubaki vilevile au zimedidimia kabisa. Lazima Tanzania tujifunze kutokana na makosa ya wengine badala ya kusubiri kujifunza kurokana na makosa yetu tutakayofanya.; it will be to late to......

Hebu fikiria nchi ina Rais anaeitwa Tundu Lissu na Makamu wa Rais John Heche na waziri Mkuu Godbless Lema na waziri wa Mambo ya nje Maria Sarungi na Katinu Mkuu wa chama John Mnyika; mbali ya kuwa wote ni wa dini moja lakini fikiria watafanya kitu gani ambacho ni tofauti na anachofanya Samia. Watafanya nini kwenye masoko, elimu, kilimo, afya, uvuvi, ufugaji, na biashara tofauti na sasa. Je, Tanzania itabaki ileile, utulivu utabaki uleule?. Je, ni nani wako nyuma ya akina Lissu kwenda Ikulu, na Je Wafadhali wao wanataka nini baada ya Lissu kukamata dola? Haya ni maswali ambayo majibu yake ni lazima uwe nayo kabla ya ku accept any change/reform.

Watu walitaka kubatilisha katiba ili mama Samia asiwe Rais because ya Imani kama zako

But here we are tunataka mama akae miaka mia
 
Hata yakitokea machafuko, ni mtoto yupi wa kiongozi wa serikali kuanzia ngazi ya wilaya alieko nchini anaeweza kuwa hatarini? Si wote wanalindwa na vyombo vya usalama? Kwani Lema na Lissu wakizurika na machafuko, hao watoto walio ughaibuni watapata faida gani kwa kuondokewa na wazazi wao?
Itakufaidia nini kupewa unachokipata au kukaa nje ya nchi kama mzazi wako kauawa?
Swala la kuandamana sio lazima, atakae weka ruksa, asieweza pia aendelee na shughuli zake. Ikiwa kutakuwa na matunda yatokanayo na harakati hizi, atanufaika hata ambae alikuwa anapinga kama ambavyo wote tunavyoumia kutokana na mifumo mibovu ya kiutawala tuliyonayo.
 
NI watu wangapi nchini wanazo passport za kukimbia machafuko? watanzania wangapi wanaweza kupewa hifadhi kwenye ubalozi wa Ujerumani kama wakikimbizwa na wasirikali? Tusidanganyane alooo kuwa we are the same.

Tudai haki zetu za kidemokrasia polepole bila kupoteza hata mwenzetu mmoja, tuwaelemishishe watu faida na hasara za Katiba ya sasa na tume ya uchaguzi ya sasa ili watu waelewe nini wanakipata na nini wanakikosa kwenye mfumo huu tulionao. Waelezeni watu faida za kiuchumi, kijamii, kiafya na kielimu watazipata kama chadema ikiingia madarakani na sio kuorodhesha makosa ya CCM tu bila kutoa njia mbadala. Mfano, CCM wanajenga reli ya kasi chadema itajenga nini? CCM inaeneza maji, umeme, afya nchi nzima, chadema itapeleka nini kwa wananchi? CCM inakopa chadema itatoa wapi pesa?
 
Watu walitaka kubatilisha katiba ili mama Samia asiwe Rais because ya Imani kama zako

But here we are tunataka mama akae miaka mia
Kwangu mimi paka ni paka ilimradi anakamata panya, rangi ya paka sio muhimu kwangu. Mama Samia kama kuna kitu anakikosea lakini sio sana kama walivyokosea magufuli, Kikwete na Mkapa buana. Samia hakuuza nyumba za serikali, mashirika ya umma, na wala hakuna Richmond, Escrow, Meremeta na wala hakupakiza twiga wetu wazima kwenye ndege kwenda uarabuni wala meno ya tembo na faru. Samia ni mama anaetafuta kuweka rekodi ya kuwa Rais mwanamke tu baaaasi kwa kutenda mema ili kupunguza kama sio kuondoa fikra kuwa mwanamke hawezi baaaaaaaaaasi
 
Ngoja Tusubiri tuone !
Hakuna haja ya kugombea fito ikiwa kweli nia yetu ni kujenga nyumba yetu moja !

Nasisitiza IKIWA NI KWELI NIA YETU NI KUJENGA NYUMBA YETU MOJA 😳 !

Kwenye meza ya mazungumzo muafaka utapatikana !
Au nasema uongo ndugu zanguni ????!!!
 
Haya mambo yote yapo

Tofauti ni now hakuna mtu wa kusema na hakuna sehemu ya kusemea

Nenda ngorongoro creta ndio utaelewa

Hayo yote yapo tena kwa %

Ndege mpya ya kisasa na kifahari umeiona?

Why masaai wameama ngorongoro? Nenda one day utapata majibu

Now ni kula Urefu wa kamba yako
 
NI watu wangapi nchini wanazo passport za kukimbia machafuko? watanzania wangapi wanaweza kupewa hifadhi kwenye ubalozi wa Ujerumani kama wakikimbizwa na wasirikali? Tusidanganyane alooo kuwa we are the same.

Tudai haki zetu za kidemokrasia polepole bila kupoteza hata mwenzetu mmoja, tuwaelemishishe watu faida na hasara za Katiba ya sasa na tume ya uchaguzi ya sasa ili watu waelewe nini wanakipata na nini wanakikosa kwenye mfumo huu tulionao. Waelezeni watu faida za kiuchumi, kijamii, kiafya na kielimu watazipata kama chadema ikiingia madarakani na sio kuorodhesha makosa ya CCM tu bila kutoa njia mbadala. Mfano, CCM wanajenga reli ya kasi chadema itajenga nini? CCM inaeneza maji, umeme, afya nchi nzima, chadema itapeleka nini kwa wananchi? CCM inakopa chadema itatoa wapi pesa?
Kuna jambo hulielewi na namna siasa zetu za Africa zinafanya kazi.
Wewe ni wa kuuliza vyama vya upinzani wanafanya shughuli gani za maendeleo kama wanavyofanya CCM?
Ni kweli husikii chochote wanachokisema vyama vingine kwamba watafanya nini ikiwa wataingia madarakani?
Hebu nipe mfano wa mazingira ambayo mwanamageuzi yeyote anaweza kufanya shughuli za maendeleo.

Hebu jaribu kutofautisha utendaji kazi kati ya CCM na Serikali alafu unirudie.
 
Ngoja Tusubiri tuone !
Hakuna haja ya kugombea fito ikiwa kweli nia yetu ni kujenga nyumba yetu moja !

Nasisitiza IKIWA NI KWELI NIA YETU NI KUJENGA NYUMBA YETU MOJA 😳 !

Kwenye meza ya mazungumzo muafaka utapatikana !
Au nasema uongo ndugu zanguni ????!!!
Ni kwanini kura za mgombea zipunguzwe au ziongezwe bila kuhojiwa? Kama taifa mtu anaepunguza au kuongeza kura za wagombea lazima tumlaani vikali sana kwa nguvu zetu zote, maana anatutafutia amani na utulivu bandia. Lakini hatumlaani kwa kuzuia uchaguzi bali kwa kuketi mezani na huyo mjinga.
 
Naunga mkono hoja 💯 ✅🙏
 
Nina watoto watatu nimewaambia msiingie kwenye mkenge huu wa maandamano LABDA watoto wa Lissu,Lema ,Heche wawe mstari wa mbele
Ila wasubiri kupigwa risasi kwenye UCHAFUZI MKUU, sivyo?
 
Yaani watoto wao wanakula pizza huko Marekani na Kanada, wanataka wa kwetu wadhurike?
Umekatazwa na wewe watoto wako kula Baga. Je ni sahihi Omary Ramadhani Mapuri kuwa Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi?
 
Back
Top Bottom