Uchaguzi 2020 Lissu majibu umeanza kuyapata, unaonaje mahudhurio hapa Kanda ya Kaskazini?

Hawa cdm ni wakuchukulia kwa tahadhari zote. Tulimsikia Silinde baada ya Mbowe kuumia mguu na kutaka kuutumia kisiasa.

Hili suala la kuchomwa ofisi linaweza kuwa na viashiria vya ile njama iliyopangwa baada ya mguu wa Mkt kuvunjika ambayo Mh Silinde alisema kilicho kuwa nyuma yake.

Lissu na wengine wamesema ofisi imepigwa bomu, haya manenò si yakuchukuliwa poa/kiwepesiwepesi, je wanao ushahidi.? Hawawezi kutumia hilo kama ule mguu wa mkt ulivyotumika kupotosha ili kupata huruma ya kisiasa?

Hawawezi kutumia hili kufanya upotoshaji kuhusu ukweli wa nini hasa kimetokea mpaka ofisi ikaungua? Kama Lissu bila aibu ametumia vyombo vya habari vya Kenya na huko Ulaya kusema uongo na kupotosha ukweli kuhusu hali ya corona ilivyo sasa hapa nchini, hatatumia uongo huohuo kuaminisha watu ndani na nje ya Tanzania kuhusu kuungua kwa hii ofisi?
 
Huoni kama yeye amekwisha anza kampeni?

Hivi unajua maana ya kuanza kampeni mapema? 😂😂😂 au unaongea tuu kisa hauna akili.. Acha kutuchafua wanaCCM kwa kutoa statements zinazotufanya tuonekane vilaza. Sisi wanaCCM tuna akili sana na tunajua hakuna kosa linaitwa kuanza kampeni mapema.
 
Nipo ngurelo eneo halitoshi, unazungumzia arusha ipi mkui
 
Wanachama na wakereketwa wa Chama cha Chadema, najua mnajua kuwa hamuwezi kushinda, na Jambo lingine ambalo mnajua Ila hamlitaki kuliskia, ni kwamba hata Mh Lisu akija kwetu na Mimi nitakwenda kwenda kumpokea hasa kushangaa jinsi Mungu alivyomshindia,ingawa ukweli ni kwamba Kura yangu haipati

Kwa tarifa yenu ni kwamba miongoni pia mwa wanao hudhuria mikutano yake ni kidogo tu watakao mpa Kura, wengi Wao wanaokwenda kumpokea ni hao wanaokwenda kushangaa muujiza wa Mungu Kwa ndugu na damu yetu mh Lisu,

Tofauti yake ni kwamba, ninyi Chadema, hamtakwenda kabisa kwenye mikutano ya Mh Magufuli, mbali na Hilo, mikutano yake itakuwa inatapika watu kuliko miaka yote na makusanyiko yote ya Magufuli muwe na uhakika ndio watakaompa kura tofauti na makusanyiko ya Lisu ambapo wengi Wao watakwenda kushangaa matendo makuu ya Mungu pekee kama nitakavyokuwa nafanya mimi na Kura wasimpe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…