Ni kweli kabisa, mtoa mada. CDM wengi wakiona watu wanaokwenda kwenye kampeni za mgombea huko mijini wanadhani ndo wameshinda. La hasha, nimekuwa nikitoa mfano mdogo tu wa matokeo ya Uchaguzi wa mwaka 2025 katika vituo 3 vya kijijini nilivyoshuhudia. Ilikuwa kama ifuatavyo:-
Kituo A: CCM kura 312, CDM 21.
Kituo B: CCM kura 279, CDM 12.
Kituo C: CCM kura 327, CDM 18.
Wakati huo kura za vituo 3 vya mijini ilikuwa kama ifuatavyo:-
Kituo A: CCM kura 310, CDM 322.
Kituo B: CCM kura 293, CDM 311.
Kituo C: CCM kura 332, CDM 287.
Kwa mchanganuo huo, ukitaka kujua chama gani kitashinda Urais, jumlisha kura za kila chama za mijini na vijijini ndipo utagundua ni nani kapata jumla ya kura nyingi zaidi.
Kwa hiyo, hivi ndivyo itakavyokuwa hata uchaguzi huu wa mwaka 2020.
Advantage ya JPM ni kwamba, yeye hahitaji kwenda vijijini kuomba kura kwa sababu tayari yeye anafahamika na CCM inafahamika na inakubalika kwa asilimia kubwa huko vijijini.