Pre GE2025 Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa

Pre GE2025 Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
ni muhimu kujiepusha na ukaidi, ni vyema kutii Sheria, makatazo na maonyo ya kiusalama bila shuruti,

vinginevyo,
jeshi la polisi litakabiliana na kiburi na majivuno ya mtu yeyote vizuri tu 🐒
Ingekuwa mbuzi na kondoo wanajipeleka wenyewe kuliwa na fisi kwa mujibu wa fikra zako
 
Ingekuwa mbuzi na kondoo wanajipeleka wenyewe kuliwa na fisi kwa mujibu wa fikra zako
ni Furaha iliyoje kwa wananchi wa mbeya na maeneo mengine kwamba uhalifu umedhibitiwa na wahalifu na majambazi wametiwa nguvuni baadhi yao,

hatuna budi kama Taifa kutoa kongole nyingi sana kwa uhodari wao kukabiliana na viashiria vya uvunjifu wa Amani 🐒
 
Kuto
Nisema Mimi 4 hizo CCM Haziwezi sababu hana mifumo ya haki.

Uvumilivu umewashinda
kutoka FOUR 4 nne R ara mpka ZERO 0 R ara 🤣🤣🤣🤣
Mama ni muongo na msanii, mtu mwenye ghubu, muoga sana, na mlanguzi wa maliasili za Tanganyika.


Huu ni wakati wa kutanguliza maslahi yetu WATANGANYIKA juu ya MAMA yetu TANAGANYIKA,kuliko maslahi ya vyama vyetu.

Enyi Mbogamboga CCM, tuachane na huyu Mama ,TANGANYIKA kwanza vyama baadae
 

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limewakamata watu wote waliokuwa ofisi za CHADEMA kanda ya Nyasa akiwemo Makamu Mwenyekiti CHADEMA Bara Mhe. Tundu Lissu, Katibu Mkuu. John Mnyika na Mwenyekiti wa Kanda Joseph Mbilinyi (SUGU) pamoja na viongozi wa BAVICHA.


Pia soma: Jeshi la Polisi lapiga marufuku mkutano wa BAVICHA siku ya vijana duniani

Viongozi hao wamekamatwa mda mfupi baada ya kumaliza kikao cha ndani kwenye ofisi hizo pamoja na viongozi waandamizi wa Bavicha na waandishi wa Habari wa Jambo TV Online waliokuwa wamepiga kambi kwenye ofisi hizo nao wamekamatwa


Lissu aliongea na vyombo vya habari leo ambapo alisema;

1. Kwa vile ofisi ya Kanda ya Nyasa zimetekwa nyara basi Leo atazigeuza ofisi hizo kuwa darasa ameliita ni darasa la kufundisha juu ya ukombozi ,yaani Teach in Resistance.

Pia soma: Msajili apiga Marufuku Kongamano la CHADEMA mkoani Mbeya, asema matamko yao yanahusisha vitendo vya uvunjifu wa amani

2. Kwa vile ofisi za Kanda ya Nyasa zimetekwa nyara Mh LISSU amesema atabaki hapo na ikibidi atalala hapo na amesema na yupo tayari kulala hapo na yeye amesema atakuwa Mwl wa kufundisha Hilo darasa la teach in Resistance. Ila kaomba iwepo namna ya kupasha joto mwili kwa sababu hali ya mbeya ni baridi,amewataka watu wakeshe pale.


3. Kwa vile ofisi za Kanda ya Nyasa zimetekwa nyara basi wataanzia safari Yao kuelekea Ruanda nzovwe kwenye ofisi hizo za Kanda ya Nyasa


4. Kwa vile ofisi za Kanda ya Nyasa zipo mateka amesema wananchi na vijana wasikubali kutishika na huyu mama ambaye hata hajachaguliwa na wananchi, amesema yeye atabaki ofisini hapo kufundisha darasa la teach in Resistance waje wankamatie pale.


Ipo siku hamtapata msaada wa polisii
 
Tulimwambia kuwa 4R ni usanii tu wa Samia kiko wapi sasa,watu wanatekwa kwa speed ya 5G.
'4R' - usanii?
Mtu mwenyewe ana uwezo mdogo halafu anatangaza jambo ambalo alipangiwa na wengine, huku yeye mwenyewe hajui inahusu nini!

Ulisha wahi kusikia akiizungumzia kwa umakini stahiki kuelezea 'philosophia hiyo ya 4R?
Alisha toa hotuba ya kufikirisha watu kuhusu hizo 4Rs?

Anachoweza yeye ni kuweka vimaneno vyepesi vyepesi tu na mipasho ya hapa na pale basi!
 
wakati wanakamatwa yeye alikuwa wapi? huyu jamaa sio wakuamini hatakidogo,
Jamaa anawalengesha wenzie wakamatwe halafu yeye aende kuwatoa ili aonekane yeye ndiyo mwenyewe? Kwa nini na yeye asiwe miongoni mwa waliokamatwa? Huu usanii haukubaliki!
 
ni Furaha iliyoje kwa wananchi wa mbeya na maeneo mengine kwamba uhalifu umedhibitiwa na wahalifu na majambazi wametiwa nguvuni baadhi yao,

hatuna budi kama Taifa kutoa kongole nyingi sana kwa uhodari wao kukabiliana na viashiria vya uvunjifu wa Amani 🐒
Fitna za za mapema kwenye sii hasaa
 
ni muhimu kujiepusha na ukaidi, ni vyema kutii Sheria, makatazo na maonyo ya kiusalama bila shuruti,

vinginevyo,
jeshi la polisi litakabiliana na kiburi na majivuno ya mtu yeyote vizuri tu 🐒
Kinachotokea ni Sawa na Kuwapa wananchi chanjo ya kupambana na polisi. Ni suala la muda tu kwa wananchi kuanza kupambana na polisi. Itakpotokea polisi watavikimbia vituo na kutupa uniform zao.. Rejea hadithi ya sativa.
 
Vyama visivyo na sera hatuwapi nafasi hata kidogo, tunakaba mpaka penati.

Ukiona chama hakina sera elewa kuwa hicho ni chama cha wahuni tu.

Upinzani wa CCM utatokea CCM. Kumbuka hilo.
Ni dharau kubwa kwa wananchi wenzako kusema chama chenhe ufuasi nchi nzima kuwa hakina sera. Mawazo yanaina yako ambayo yako kwa wenye mamlaka yatapelekea kutokea kwa machafuko nchini. (Wananchi kujitetea )
 
Hicho chama wakubwa wa chama wapo kimaslahi binafsi zaidi, siyo kwa ajili ya wananchi.

Ukiona misuguano huko ujuwe zinagombaniwa ruzuku tu.

Wajinga ndiyo waliwao.
Wauza rasilimali za nchi wanatumia pesa walizovuna kuchafua siasa.
 
ni Furaha iliyoje kwa wananchi wa mbeya na maeneo mengine kwamba uhalifu umedhibitiwa na wahalifu na majambazi wametiwa nguvuni baadhi yao,

hatuna budi kama Taifa kutoa kongole nyingi sana kwa uhodari wao kukabiliana na viashiria vya uvunjifu wa Amani 🐒
Unatia petrol kwenye mafuta kea kutumia lugha ya kukera. Ilichukua watu na.maneno ya aina hii kwa walio wengi kujenga hasira kali iliyosababisha mauaji ya kimbari
 
Ilisemwa mikutano ina viashiria vya uvunjifu wa amani. Vyama vilipoachwa kubughudhiwa (si kuruhusiwa) katika mikutano hakuna tukio la uvunjifu wa amani. Walionufaika ni Chadema wali 'prove' kwamba hakuna fujo

Pili, kuwazuia Chadema peke yao kunawapa ''mileage na sympathy' kutoka katika public na kuifanya Chadema '' relevant' kisiasa. In fact hii ni promo, zinazo trend ni habari hizo,si mikutano ya UVCCM au ACT

Tatu, Polisi hawatambui impact ya hili jambo. Ni kumhujumu Mh Rais, wanamfunga mdomo asizungumzie 4R kwa maana '' talks the talk but does not walk the walk''.
 
Back
Top Bottom