Pre GE2025 Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Vyama visivyo na sera hatuwapi nafasi hata kidogo, tunakaba mpaka penati.

Ukiona chama hakina sera elewa kuwa hicho ni chama cha wahuni tu.

Upinzani wa CCM utatokea CCM. Kumbuka hilo.
Ccm ina sera gani.au unajiandikia tu ujinga.Nchi imeshawashinda ndo maana hamtaki siasa zakistarabu.miaka 60 mko madarakani bado mnaogopa upinzani hiyo maana yake mmeshindwa.
 
Mwabukusi where are you my friend!

Ccm chama changu hakuna haja ya kuogopa!!

Sasa basi kwakuwa chama kimekosa watu wenye akili za kisayansi wameshauri ujinga na ujinga huu unaenda kutugharim!!

Kongamano la Bavicha ndio litafana zaidi na kuwa kiki kubwa kisa hao jamaa wamekamatwa!!yaani mmewapa kiki Bavicha na watapata huruma ya wananchi!!

Mngefanya kama mlivyo handle maandamano yalivyolindwa na polisi na mkutano wao mngelinda hivyo hivyo !!

Mngewaita viongozi wa kamati kuu na kuwashauri mkutano uwe wa amani kuliko kuwakamata!
Sijui kwanini wanawapa air time ya bure...Daah!
 
Vyama visivyo na sera hatuwapi nafasi hata kidogo, tunakaba mpaka penati.

Ukiona chama hakina sera elewa kuwa hicho ni chama cha wahuni tu.

Upinzani wa CCM utatokea CCM. Kumbuka hilo.
Wewe ulikuwa ukimponda Magufuli....tumejua kumbe ulikuwa ukimponda kwa Chuki tu. Maana aliyofanya magu ndio hayo hayo unayakubali kwa Samia.

wanafiki sana nyie watu.
 
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limewakamata watu wote waliokuwa ofisi za CHADEMA kanda ya Nyasa akiwemo Makamu Mwenyekiti CHADEMA Bara Mhe. Tundu Lissu, Katibu Mkuu. John Mnyika na Mwenyekiti wa Kanda Joseph Mbilinyi (SUGU) pamoja na viongozi wa BAVICHA.

Pia soma: Jeshi la Polisi lapiga marufuku mkutano wa BAVICHA siku ya vijana duniani

Viongozi hao wamekamatwa mda mfupi baada ya kumaliza kikao cha ndani kwenye ofisi hizo pamoja na viongozi waandamizi wa Bavicha na waandishi wa Habari wa Jambo TV Online waliokuwa wamepiga kambi kwenye ofisi hizo nao wamekamatwa

Lissu aliongea na vyombo vya habari leo ambapo alisema;

1. Kwa vile ofisi ya Kanda ya Nyasa zimetekwa nyara basi Leo atazigeuza ofisi hizo kuwa darasa ameliita ni darasa la kufundisha juu ya ukombozi ,yaani Teach in Resistance.

Pia soma: Msajili apiga Marufuku Kongamano la CHADEMA mkoani Mbeya, asema matamko yao yanahusisha vitendo vya uvunjifu wa amani

2. Kwa vile ofisi za Kanda ya Nyasa zimetekwa nyara Mh LISSU amesema atabaki hapo na ikibidi atalala hapo na amesema na yupo tayari kulala hapo na yeye amesema atakuwa Mwl wa kufundisha Hilo darasa la teach in Resistance. Ila kaomba iwepo namna ya kupasha joto mwili kwa sababu hali ya mbeya ni baridi,amewataka watu wakeshe pale.

3. Kwa vile ofisi za Kanda ya Nyasa zimetekwa nyara basi wataanzia safari Yao kuelekea Ruanda nzovwe kwenye ofisi hizo za Kanda ya Nyasa

4. Kwa vile ofisi za Kanda ya Nyasa zipo mateka amesema wananchi na vijana wasikubali kutishika na Rais Samia, amesema yeye atabaki ofisini hapo kufundisha darasa la teach in Resistance waje wankamatie pale.
Ivi Lissu si alisema atatimkia ccm kama chadema itaacha misingi yake? Nafikiri anashuhudia ccm ilivyo au tuseme huwa ni njaa tu kufuata vyeo ilhali wanajua yaliyoko ccm
 
Naona ulichotaka hakikatimia moyo unakuuma.
 
GettyImages-948792730.jpg

Mama wa Bangladesh yuko wapi na UBABE wake?!
 
Jeshi la police nchini linashughulika na kila aina ya uhalifu na kila ishara au viashiria vya kihalifu popote nchini...

hakuna kuona aibu wala kuona haya kwenye kudeal na kupambana na wahalifu 🐒
We ni mpuuzi sana, respond my question objectively!
 
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limewakamata watu wote waliokuwa ofisi za CHADEMA kanda ya Nyasa akiwemo Makamu Mwenyekiti CHADEMA Bara Mhe. Tundu Lissu, Katibu Mkuu. John Mnyika na Mwenyekiti wa Kanda Joseph Mbilinyi (SUGU) pamoja na viongozi wa BAVICHA.

Pia soma: Jeshi la Polisi lapiga marufuku mkutano wa BAVICHA siku ya vijana duniani

Viongozi hao wamekamatwa mda mfupi baada ya kumaliza kikao cha ndani kwenye ofisi hizo pamoja na viongozi waandamizi wa Bavicha na waandishi wa Habari wa Jambo TV Online waliokuwa wamepiga kambi kwenye ofisi hizo nao wamekamatwa

Lissu aliongea na vyombo vya habari leo ambapo alisema;

1. Kwa vile ofisi ya Kanda ya Nyasa zimetekwa nyara basi Leo atazigeuza ofisi hizo kuwa darasa ameliita ni darasa la kufundisha juu ya ukombozi ,yaani Teach in Resistance.

Pia soma: Msajili apiga Marufuku Kongamano la CHADEMA mkoani Mbeya, asema matamko yao yanahusisha vitendo vya uvunjifu wa amani

2. Kwa vile ofisi za Kanda ya Nyasa zimetekwa nyara Mh LISSU amesema atabaki hapo na ikibidi atalala hapo na amesema na yupo tayari kulala hapo na yeye amesema atakuwa Mwl wa kufundisha Hilo darasa la teach in Resistance. Ila kaomba iwepo namna ya kupasha joto mwili kwa sababu hali ya mbeya ni baridi,amewataka watu wakeshe pale.

3. Kwa vile ofisi za Kanda ya Nyasa zimetekwa nyara basi wataanzia safari Yao kuelekea Ruanda nzovwe kwenye ofisi hizo za Kanda ya Nyasa

4. Kwa vile ofisi za Kanda ya Nyasa zipo mateka amesema wananchi na vijana wasikubali kutishika na Rais Samia, amesema yeye atabaki ofisini hapo kufundisha darasa la teach in Resistance waje wankamatie pale.
si wanasema chadema mbowe ameiua. haina lolote. ushindi ni wa kishindo
 
Watanzania tujiulize tumefikaje hapa!
Mkuu, tumekuwa na chama kimoja kinacho endesha Serikali for 60yrs, tangu tupate Uhuru ndio maana tupo hapa; laiti Nchi ingetawaliwa na vyama mbalimbali kwa kupokezana nadhani tusinge yaona haya. Hili ni tulionalo ni jambo la kawaida sana kiasi kwamba halinge julikana. Hii yote ni uroho wa madaraka.
 
Kwa mtamo wangu naona ni bora wafute mambo ya vyama vingine ili kibaki kimoja kama kukubali changamoto imeshindikaña
 
Back
Top Bottom