Lissu: Naishi kwenye makazi ya balozi(Ujerumani) kwa sababu maisha yangu hayako salama, nitarejea Ubelgiji

Lissu: Naishi kwenye makazi ya balozi(Ujerumani) kwa sababu maisha yangu hayako salama, nitarejea Ubelgiji

..ukimuona mwanasiasa anazungumza mapungufu ya serikali yake nje ya nchi ujue kwamba hana uhuru wa kufanya hivyo akiwa ndani ya nchi.

..utawala huu umewanyima wananchi uhuru wa kuikosoa serikali yao na watendaji wake. matokeo yake ndiyo hayo, watu wanakwenda kuzungumzia nje ya nchi.

..wakati wa utawala wa Mzee Mkapa na Mzee Kikwete kulikuwa na uhuru fulani wa kuzungumza na kukosoa. Na kipindi hicho hatukumshuhudia Tundu Lissu akiikosoa serikali akiwa nje ya Tanzania. Hali hiyo imebadilika miaka ya karibuni wakosoaji wanaumizwa, wanasumbuliwa, wanatishwa, na ndio maana wengine wanasema-sema huko nje.
Kwenye kampeni mbona alikua na huo uhuru? Alitukana na kusema kila kitu hakuna aliyemsumbua?
Akibali tu kuwa watz ndio tumemvurumisha
 
Kwenye kampeni mbona alikua na huo uhuru? Alitukana na kusema kila kitu hakuna aliyemsumbua?
Akibali tu kuwa watz ndio tumemvurumisha

..sheria za uchaguzi zinaelekeza jeshi la Polisi kutoa ulinzi, wakati wa kampeni, kwa wagombea Uraisi.

..kwa hiyo kipindi cha kampeni Tundu Lissu alikuwa na ulinzi. Baada ya kampeni kukoma, ulinzi nao umekoma.

..Jeshi la Polisi lilitakiwa liendelee kumlinda Tundu Lissu kwasababu waliomshambulia bado hawajakamatwa.
 
Toka Kagoshima uridi Dar, Moro, Arusha or upareni. Bro, Mama alisha sema kama ile kazi ingekuwa ya serekali mngekuwa mnaita Marehemu ndio jina lake lifuate.
Kajifunze kwanza kuandika ndipo urudi JF
 
..Kama hakuna usalama wa kuzungumza ndani ya nchi, basi busara ni kuzungumza nje ya nchi.

..Matatizo ya nchi yanatatuliwa kwa njia na watu wengi, ikiwemo wa ndani na nje.

..Nategemea wazungu watasaidia kutatua mapungufu ya serikali ya Tanzania bila malipo, kama sisi Watanzania tulivyosaidia nchi za Kusini mwa Afrika bila malipo.

..Wazungu pia walisaidia ukombozi wa Kusini mwa Afrika bila malipo. Misaada ya kibinadamu[humanitarian] na mashinikizo ya kidiplomasia kutoka nchi za Ulaya yalikuwa na msaada mkubwa ktk harakati za ukombozi kusini mwa Afrika.
Mungu wangu🙈, naomba Mungu akusaidie ili uone hawa wazungu walichokifanya na wanachokifanya hapa Africa ili upate kufunuliwa na kuelewa kuwa hao wazungu ni majasusi wakubwa na sio watu wazuri. Nenda ukapitie historia tena.

Jamani, mzungu hafanyi kazi ya bure bila kunufaika, naomba muelewe hilo.
Wazungu wana matatizo chungu nzima huko nchini mwao , kwann wasiyatatue matatizo yao kwanza badala yake wakuletee ww misaada!!?? Pia hawa si baba, mama au wajomba zetu watupe vitu vya bure. Jamani, mzungu hafanyi kazi ya bure bila kunufaika.

Naomba upitie utafiti wako kwa kina kisha uufanyie tathmini. Ukimaliza naomba unijibu mmiliki wa migodi ya South Africa ni muafrika au mzungu!?
 
Hivi muuaji ni yule mwenye lengo la kuuza nchi yetu kwa wakoloni?
Au ni yule anayewabana wakoloni wasitunyonye?!!
Muuaji ni yule anayepiga watu risasi mchana kweupe!Muaaji ni yule ambaye amekatisha maisha ya wazanzibar utafikiri anaua nzi!
 
Njama, hila na ulaghai wa Lissu umeshajulikana. Yaani kipindi chote cha kampeni hakukuwa na tishio, iweje baada ya Uchaguzi awe anatishiwa?

Asichofahamu ni kudhani alikuwa anapendwa na watanzania kumbe wananchi walikuwa wanaenda kwenye kampeni zake kumfurahisha maana alikuwa anataka Kura za huruma.

Uzuri ni kuwa hata hao Wazungu anawalilia sasa hivi wameshamfahamu kwamba ana matatizo ya kisakolojia.
Wakati wa kampeni,kisheria usalama wa Taifa walikuwa wakimlinda,hivi sasa yuko kivyake..

Kiukweli alivyofanya Lisu ni sawa

Inasikikitisha kuwa Tanzania tumefika huko,Nchi ya Amani imekuwa Nchi ya wakimbizi wa kisiasa

Yote kwasababu chama fulani kinang'ang'ania kibaki Madarakani kwa njia yoyote ile..

Uchu na uroho wa Madaraka unawasumbua,lakini naamini hakuna kisichokuwa na mwisho

God bless Tanzania..
 
Muuaji ni yule anayepiga watu risasi mchana kweupe!Muaaji ni yule ambaye amekatisha maisha ya wazanzibar utafikiri anaua nzi!
Wale waliondamana walifanya vurugu na walivunja sheria, hawakufuata taratibu sahihi. Mwana kulifind mwana kuliget.
Umeambiwa usiandamane halafu unaandamana ukiwaona polisi unawarushia mawe, unataka wakuangalie tu.
 
Wale waliondamana walifanya vurugu na walivunja sheria, hawakufuata taratibu sahihi. Mwana kulifind mwana kuliget.
Umeambiwa usiandamane halafu unaandamana ukiwaona polisi unawarushia mawe, unataka wakuangalie tu.
Nadhani umemuelezea vizuri muuaji!
 
Hizi ni story za kwenye vijiwe vya kahawa...hivi wakitaka kummaliza wanashindwa kufika hapo ubalozini?
Hawawezi,inavyoonyesha hata Sheria za kimataifa huzijui

Jaribu Ku save muda wako usijibu kitu usichokijua .

Kuna jamaa,mmiliki wa tovuti ya Wikileaks anaishi ubalozi wa Ecuador nchi Uingereza miaka mingi sasa, serikali ya Marekani wanashindwa kumtoa huko

Wamarekani wanamtaka akajibu mashtaka Marekani
3000.jpeg
 
Mimi napata mashaka sana na kile kinachoitwa dhamira njema ya serikali hii ya ccm, Hivi mtanzania unakaa uhamishoni ndani ya nchi yako???? Hii hapana.

Huu ni uthibitisho tosha kuwa JPM ni Dikteta mshamba sana, anakanyaga katiba kwa kigezo cha kuleta maendeleo. Hii falsafa haitamuacha salama.
 
Wakati anapigwa risasi 16 walimpiga risasi kwakuwa alikuwa anataka urais waaje ?we kibwengo
 
Alikuwa na Tiketi ya kurudi tayari kwahiyo hakuna jipya hapo ni kick kwa Pikipiki
 
Umemuelezea vizuri muuaji ila ukasema alikuwa na sababu za kuua na mojawapo eti kwasababu waliouwawa waliandamana bila kibali,shwain kabisa!
Mwizi akija nyumbani kwako akataka au akahatarisha usalama wa maisha yako na watu wengine utamuangalia tu na kumchekea??
 
Yote haya ni kwasababu ya kudumu ktk madaraka fulani.Hakuna aliye salama hata mmoja.
 
"LISSU: Tuombe Mungu atupe uzima tujue miaka inayokuja itatuweka vipi lakini nachoweza kusema waziwazi ni kwamba harakati ni maisha yangu."
Hii ina maana ni kusema ni mwanaharakati na siyo mwanasiasa?
 
Mimi napata mashaka sana na kile kinachoitwa dhamira njema ya serikali hii ya ccm, Hivi mtanzania unakaa uhamishoni ndani ya nchi yako???? Hii hapana.

Huu ni uthibitisho tosha kuwa JPM ni Dikteta mshamba sana, anakanyaga katiba kwa kigezo cha kuleta maendeleo. Hii falsafa haitamuacha salama.
 
Back
Top Bottom