Most likely...
Hata hivyo, nadhani pia kuwa, na majira na nyakati za mtindo wa uongozi wake umepita na amefanya kazi kubwa na nzuri sana kwa miaka zaidi ya 20 ya uongozi wake na kuziweka CHADEMA katika ramani za siasa za dunia. Freeman Mbowe anastahili maua yake...
However, It's now high time awaachie wengine waje na mbinu na mikakati mipya ya kukipeleka chama mbele zaidi katika majira na nyakati hizi za mtindo mpya wa siasa za Tanganyika..
Hotuba ya Tundu Lissu Jana ilisema na kutoa Nuru mpya kabisa. Ili address kila kitu
Bila shaka Tundu Lissu atakuwa Mwenyekiti bora sana sawasawa na alivyokuwa Freeman Mbowe na pengine kumzidi na tunataka iwe hivyo....
Uongozi wa Freeman Mbowe ni muda tu. Otherwise huyu Bwana ni mmoja wa wenyeviti wa CHADEMA aliyefanya kazi kubwa sana kukiongoza chama kukua na kuwa chama shindani kwelikweli na CCM...
Amefanya kazi kubwa sana na nzuri kabisa. Sasa anastahili kupumzika na kuwa mshauri mkuu wa chama...