Nimesema jana!! Katika umri wangu na uzoefu wangu ikiwemo kusoma historia ya Tanzania. Nchi hii haijawai pata mwanasiasa kiwango cha Tundu Antiphas Lissu.
Si Kambona, si kolimba, Si Njelu kusaka na G55 yao, si mtikila, si tuntemeke sanga , si aboud Jumbe, si Maalim Seif, Mbowe, Lipumba, Magufuli, si Juma Duni Haji , Zi zitto, si Nyerere wala si kikwete.
Lissu ni alama ya kitu cha kipekee sana kwenye siasa za Tanzania. Ni alama kweli ya haki, uhuru, amani, upendo na kubwa zaidi Lissu ni kielelezo cha kutumia akili na si nguvu katika kusimamia kweli unaloliamini bila kujali matokeo yatakuwaje! Kitendo cha yeye mwenyewe jana kuongoza katika kusimamia analolitetea tena kwenye mazingira magumu vile( Mbele ya askari waliosheheni Silaha za kivita) huku akisimamia msimamo wake hadi mwisho kushinda ni kielelezo cha kipekee sana kwa jinsi gani huyu mtu ni special.
Jana Lissu kafanya kampeni kubwa sana, maana hata wale waliodhani angeshindwa mwishoni walipigwa na butwaa.
Lissu sio tu ni binadamu, ni binadamu na nusu
Lissu sio tu mwana siasa ni mwana siasa na nusu
Lissu sio tu mtu wa haki ni mtu wa haki na nusu
Hongera Lissu!!
Watanzania wote kwa pamoja tunasema Shkamoo!!