Uchaguzi 2020 Lissu ni zaidi ya Lowassa, kaeni mkao wa kukabidhi Nchi kwa Amani

Uchaguzi 2020 Lissu ni zaidi ya Lowassa, kaeni mkao wa kukabidhi Nchi kwa Amani

Wanataka uhakika wa milo mitatu ya chakula kwa siku. Hawali majengo ama flyover za Ubungo ama ndege zenu hizo.

Watu wanataka na wanadai UHURU WAO!

Watu tunataka kuheshimiwa kwa Uhuru wetu wa mawazo.

Watu tunataka Uhuru wa kukusanyika na kuzungumza.

Watu tunataka Uhuru wetu wa kuchagua.

Watu hatutaki UTUMWA wa mkoloni mwaarabu na mzungu wa kutupangia tuseme nini? Tuende wapi? Tutazame TV gani? Tumsikilize nani na tusimsikilize nani? Tusome gazeti gani? nk nk

Ukienda Singida au Manyara au Arusha au Kigoma au Lindi na Mtwara kisha uwaoneshe watu picha hizi za kutengeneza kama kigezo cha kukuchagua uwe kiongozi wao na halafu uwaambie "HAYA NDIYO MAENDELEO", hutashuka salama jukwaani, lazima upigwe mawe mpaka ufe....!!

Watu wanataka SERA na MIPANGO inayotengeneza mazingira mazuri ya wakulima kushiriki kwenye shuguli yao ya KILIMO. Siyo SERA na MAAMUZI mkurupuko ya Ndg Magufuli Pombe na kuharibu sekta ya kilimo kwa ujumla.

Ameharibu soko na kisha kilimo cha Korosho na mbaazi huko mikoa kusini; ameharibu soko na kilimo cha Mkonge mikoa ya Tanga na Morogoro; ameharibu soko na kilimo kwa ujumla cha zao la pamba mikoa yote ya kanda ya ziwa!

Watu wanataka SERA na MIPANGO inayotengeneza mazingira favourable kwa ajili ya takayowezesha kufanya biashara, wavuvi kuvua, wajenzi kuendeleza shughuli yao ya ujenzi nk...

Kwa kuwa na SERA na MIPANGO inayotengeneza mazingira favourable ya watu kushiriki shughuli za kiuchumi zenye lengo la kuinua kipato cha familia moja moja, wewe ndiye kiongozi bora na unayefaahii kupewa dhamana ya kuongoza watu.

Wafanyakazi wanataka SERA na MIPANGO bora ya kuboresha kipato chao cha mshahara mwaka hadi mwaka ili waweze kuleta ufanisi katika maeneo yao ya kazi na wao kuweza kupata mahitaji yao ya msingi ya kila siku bila shida.

Kiongozi katika nchi HURU na ya KIDEMOKRASIA anayetumia fedha zote za umma kutengeneza vitu tu huku wananchi wake zaidi ya 90% wakiwa hawana uhakika wa kupata Milo mi3 kwa siku , wanaishi kwenye makazi duni na dhariri, hawana uwezo wa kununua mavazi yao ya kujisitiri, hawezi kuwa appreciated kinyume chake huyu hana tofauti na wakoloni wa kiarabu na wazungu tuliowafurusha miaka 60 iliyopita.
 
Hii kitu Wakaaa na tu Laptop vyumbani wakijadiliana namna ya kujibu lakini wanajikuta ili waeleweke ni lazima watafute siasa za kufikilirika. Wakaa na Laptop vyumbani kutengeneza Thread naona mnahangaika sana. Kwanini mnapata tabu hivyoooo.

Mnasifia asiyekuwa na shukrani 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣. Lissu hana Ajenda, anarukia rukia tu Mfano anashauri Wananchi wavae Barakoa wakati yeye Mwenyewe havai. Anaiichafua nchi kwa Wakenya kuwa Watanzania wanapata shida wakati Kenya Mpaka saizi wameelemewa, watu wanakufa
 
Nimefanikiwa kupitia mikoa zaidi ya saba bara tangu Lissu arejee nchini na kuonesha nia ya dhati ya kugombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, nimekutana na watu wengi lakini jambo kubwa ni upendo watu walionao kwa Lissu.

Naamini kama wameandikishwa kwenye daftari ya wapiga kura Lissu atabeba %80 ya kura zote kinachotakiwa ni ulinzi wa kura na kuweka mikakati ya kulazimisha kutangaza mshindi hili likifanikiwa Magufuli atavunja record sio tu ya kutawala kwa muhula mmoja bali kukabidhi nchi bila maandamano na kumwaga damu.
Umepitia mikoa saba kwa usafiri gani na nani alikutuma. Uwekezaji wa Lowassa kwenye siasa za urais wa nchi unaweza mlinganisha na huyo mpiga kelele wenu asiyejitambua. Nani ampe nchi yule.Magu anajizoelea 95% na 90% ya wabunge
 
Nimefanikiwa kupitia mikoa zaidi ya saba bara tangu Lissu arejee nchini na kuonesha nia ya dhati ya kugombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, nimekutana na watu wengi lakini jambo kubwa ni upendo watu walionao kwa Lissu.

Naamini kama wameandikishwa kwenye daftari ya wapiga kura Lissu atabeba %80 ya kura zote kinachotakiwa ni ulinzi wa kura na kuweka mikakati ya kulazimisha kutangaza mshindi hili likifanikiwa Magufuli atavunja record sio tu ya kutawala kwa muhula mmoja bali kukabidhi nchi bila maandamano na kumwaga damu.
Ni yeye lisu
 
ichumu lya,

Porojo aiseee. LISSU mwenyewe amekiri kuwa kwa maendeleo haya yaliyofanywa na RAIS WETU MPENDWA JPM tena kwa kipindi kifupi, Aisee PAMOJA na Marisasi ya kutengeneza na sanaa kutoboa ni kazi so wamekubaliana waanzishe mitafaruku akamatwe apate umaarufu wa huruma.

HAKUNA ANAYETHAMINI UPUUZI HUU VIJIJINI! MIJNI WANAHTAJI HELA MFUKONI SI TAKATAKA HIZO
 
Hivi bado naweza kujiandikisha maana mood imerudi kwa hali ya juu.Nilikata tamaa kama atarudi.
Hapa ndipo vyama vingi vinapokoseaga. Kuongea na kupiga kampeni bila kupiga kura hakunaga ushindi. Hakikisha unapiga kura kamanda bampami
CCM mapemaaa walipita kuhimiza wanachama wakajiandikishe kupiga kura na walijiandikisha kwa wingi kweli,
 
Makamanda kwa kutiana molali mko njema, uhalisia John pombe magufuli wa ccm atatangazwa mshindi baada ya kuongoza kwa kura nyingi sana.
Watakuja kukataa ili kuwaaminisha wanachama kuwa wanaonewa
 
Tofauti ya lowasa na Lisu ni Lowasa alikuwa na watu wafuasi wake na mashabiki kila mkoa na Wilaya ndani ya ccm na serikali, na walimkubali, pia walitumia sana pesa zake.

Lisu anawashabiki ndani ya chadema,na dunia hii hapwendi mtu ila pesa zake kwanza sasa lisu ajipange kwa sabuni ya roho kwanza
 
ichumu lya,

Hii habari yako naikubali kwa 100% maana nchini kote hasa cha ajabu safari hii hata vijijini na akina mama nao pia wimbo wao ni Lissu.
Niko Dar, kunasiku nimepiga simu kijijini huko ukerewe panaitwa kaseni, nikiwa na lengo la kuongea na dada kuhusu biashara ya samaki aina ya 'gogogo ' wakerewe wanaziita NGERE.. maana huyo dada ndo kazi yake ya kuwaandaa na kuwakausha kwa jua au moshi.

Kilichonishangaza baada ya kusalimiana nae kilugha alichoniuliza aliuliza hivi " LISU OMULOZILE NI MZIMA BEEE??' Akiwa na maana ya kwamba LISU ULIMUONA NI MZIMA KABISAA?? Nilishtuka sana....Ikabidi nimkubalie japo sikumwona kabisaa live lisu siku hiyo.
 
ichumu lya,

Porojo aiseee. LISSU mwenyewe amekiri kuwa kwa maendeleo haya yaliyofanywa na RAIS WETU MPENDWA JPM tena kwa kipindi kifupi, Aisee PAMOJA na Marisasi ya kutengeneza na sanaa kutoboa ni kazi so wamekubaliana waanzishe mitafaruku akamatwe apate umaarufu wa huruma.

Hayo yote yamwfanywa kwa fedha za Watanzania wala hakuna aliye toa fedha zake za mshahara. Wacheni kuwadanganya watu.
 
Wasichoelewa watu ni kwamba Magufuli na CCM yake wakati umewakataa!

Yaani majira hayakubaliani nao ingawa wanalazimisha!

Japo watu wanapuuza lakini CCM inaanguka mwaka huu... na Magufuli hana upepo kabisa!
Ccm na wagombea wake wanakutana na upepo mkali sana wa kisuri suri
 
Makamanda kwa kutiana molali mko njema, uhalisia John pombe magufuli wa ccm atatangazwa mshindi baada ya kuongoza kwa kura nyingi sana.
JPM katili sana, ndiye aliyebariki shambulio la Lissu kuchapwa zile mvua za risasi. Muda ukifika tutaweka wazi kila kitu.
 
yani ingekua mitandao ya jamii ndio inapiga kura uchaguzi ungekua ushaisha lakini sasa Watanzania ndo wanaopiga kura. ila Makamanda kwa kupeana moyo safi sana japo moyoni wanajua kabisa jamaa wao achomoki kwa jiwe. tena kipindi hiki jiwe anaenda kushinda kwa gap kubwa sana kuliko 2015. anyway makamanda kunja ngumi kunja ngumi peoples...
 
Lissu Ni mpuuzi Kama wapuuzi wengine, yaani kwa akili zako unafikiri watanzania tuko tayari kuongozwa na mtu aliekuwa anafunuliwa marinda na mtaro huko Ubeligiji??

Kwa taarifa Lissu tunaenda kumtembezea kipigo cha Mbwa mwizi na hataamini kitakachotokea.

Yaani vijana wa bavicha mmebaki na propaganda, Mlivyoenda kuchukuwa fomu mmeishia kuoga aibu? Jana Singida aibu tupu.

Tukutane tarehe 28/10/2020 tuwafundishe kwa vitendo kwanini
 
Back
Top Bottom