Hilo la kusema ati Wapinzani kazi yao ni kulaumu,kupinga na kulalamika sikubaliani na wewe....!!!
Hivi ulitegemea Wapinzani wafanyeje au waseme Nini? Hivi unyama, ubabe na ukatili anaowafanyia Wapinzani huyu Rais Magufuli wanyamae tu kama mijikondoo? Tabia hii ya Jiwe ni mpya kabisa na haijawahi kufanywa na Marais wote walopita!!!
Hata leo hii ikatokea CCM wakawa upande pinzani wataanza kulalamika tu....!!
Naamini hoja zako zinawakilisha au ni "copy & paste" za viongozi wa upinzani, hasa CHADEMA. Ni hoja zinatokana na madai ya muda mrefu ya upinzani yanayosukumwa kisiasa (hawatoi ushahidi) kwa nia ya kupata huruma ya jamii ya kiTanzania na kiMataifa.
Kama upinzani kweli una nguvu, hasa Lissu, mgombea wake wa Urais, tungeshuhudia mafuriko kutoka CCM kuelekea ya upinzani, kwa watia nia ya Urais, Ubunge na Udiwani, walioshindwa kura za maoni, kama ilivyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu, 2015.
Ukweli unabaki kuwa miaka 5 ya utawala wa Magufuli, viongozi wa upinzani wamebaki kucheza na kauli zake na matukio, badala ya kujiimarisha toka ngazi za chini (vitongoji na mitaa). Kwa upande mwingine wa kisiasa, CCM imekuwa ikijiimarisha (kimuundo na kiuendeshaji) na pia kuisimamia Serikali katika ujenzi wa vitu vinavyochochea kukua kwa uchumi. Isitoshe, CCM ina Jumuia zenye nguvu kisiasa. Kususia kwa upinzani kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakuwa mtaji mkubwa wake kwenye Uchaguzi Mkuu.
Madai kuwa CCM inabebwa na vyombo vya Dola na Tume ya Uchaguzi, ni kukiri kuwa CCM ni moyo wa WaTz kwa mnaamini kuwa watendaji wa vyombo hivyo nao ni wapenzi/wafuasi wake.