Wanataka uhakika wa milo mitatu ya chakula kwa siku. Hawali majengo ama flyover za Ubungo ama ndege zenu hizo.
Watu wanataka na wanadai UHURU WAO!
Watu tunataka kuheshimiwa kwa Uhuru wetu wa mawazo.
Watu tunataka Uhuru wa kukusanyika na kuzungumza.
Watu tunataka Uhuru wetu wa kuchagua.
Watu hatutaki UTUMWA wa mkoloni mwaarabu na mzungu wa kutupangia tuseme nini? Tuende wapi? Tutazame TV gani? Tumsikilize nani na tusimsikilize nani? Tusome gazeti gani? nk nk
Ukienda Singida au Manyara au Arusha au Kigoma au Lindi na Mtwara kisha uwaoneshe watu picha hizi za kutengeneza kama kigezo cha kukuchagua uwe kiongozi wao na halafu uwaambie "HAYA NDIYO MAENDELEO", hutashuka salama jukwaani, lazima upigwe mawe mpaka ufe....!!
Watu wanataka SERA na MIPANGO inayotengeneza mazingira mazuri ya wakulima kushiriki kwenye shuguli yao ya KILIMO. Siyo SERA na MAAMUZI mkurupuko ya Ndg Magufuli Pombe na kuharibu sekta ya kilimo kwa ujumla.
Ameharibu soko na kisha kilimo cha Korosho na mbaazi huko mikoa kusini; ameharibu soko na kilimo cha Mkonge mikoa ya Tanga na Morogoro; ameharibu soko na kilimo kwa ujumla cha zao la pamba mikoa yote ya kanda ya ziwa!
Watu wanataka SERA na MIPANGO inayotengeneza mazingira favourable kwa ajili ya takayowezesha kufanya biashara, wavuvi kuvua, wajenzi kuendeleza shughuli yao ya ujenzi nk...
Kwa kuwa na SERA na MIPANGO inayotengeneza mazingira favourable ya watu kushiriki shughuli za kiuchumi zenye lengo la kuinua kipato cha familia moja moja, wewe ndiye kiongozi bora na unayefaahii kupewa dhamana ya kuongoza watu.
Wafanyakazi wanataka SERA na MIPANGO bora ya kuboresha kipato chao cha mshahara mwaka hadi mwaka ili waweze kuleta ufanisi katika maeneo yao ya kazi na wao kuweza kupata mahitaji yao ya msingi ya kila siku bila shida.
Kiongozi katika nchi HURU na ya KIDEMOKRASIA anayetumia fedha zote za umma kutengeneza vitu tu huku wananchi wake zaidi ya 90% wakiwa hawana uhakika wa kupata Milo mi3 kwa siku , wanaishi kwenye makazi duni na dhariri, hawana uwezo wa kununua mavazi yao ya kujisitiri, hawezi kuwa appreciated kinyume chake huyu hana tofauti na wakoloni wa kiarabu na wazungu tuliowafurusha miaka 60 iliyopita.