Uchaguzi 2020 Lissu ni zaidi ya Lowassa, kaeni mkao wa kukabidhi Nchi kwa Amani

Msijibu kwa Risasi nakumbuka Ben Rabuh Saa Nane alipogusa PHD ya mtesaji wetu mpaka leo hajulikani alipo sasa subiri ya Bashir kupelekwa gerezani
 
Msijibu kwa Risasi nakumbuka Ben Rabuh Saa Nane alipogusa PHD ya mtesaji wetu mpaka leo hajulikani alipo sasa subiri ya Bashir kupelekwa gerezani
Upuuzi wake ni kusema ukweli mnlo mwaka huu,pambana na hali yenu.
 
Makamanda ni watu mahiri sana katika kutiana moyo. Basi tusubiri na asijitokeze mtu kusema wameibiwa kura!
Wana takwimu wanazobuni wenyewe na kudanganyana kwingi tu.

October haiko mbali.
 
Nimefanikiwa kupitia mikoa zaidi ya saba bara tangu Lissu arejee nchini na kuonesha nia ya dhati ya kugombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, nimekutana na watu wengi lakini jambo kubwa ni upendo watu walionao kwa Lissu...
[emoji2788] [emoji2788] [emoji2788] [emoji2788] [emoji101][emoji101][emoji101][emoji101]

Nimtapata taabu sana mwaka huu, kwani
Naona gari ni lile lile mnabadilisha plate number tu !!

Mnapotembela hiyo mikoa mnafikia kwa shoe shine tena, wale waliosimika bendera za kikundi chenu.
Sasa hapo ndo unakimbilia JF na takwimu za kipumbavu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ndipo vyama vingi vinapokoseaga. Kuongea na kupiga kampeni bila kupiga kura hakunaga ushindi. Hakikisha unapiga kura kamanda bampami
CCM mapemaaa walipita kuhimiza wanachama wakajiandikishe kupiga kura na walijiandikisha kwa wingi kweli,
Si wakati ule wapinzani walipoitisha mikutano wakakamatwa kuwa hawana vibali au mim nasahau
 
Iwapo upinzani ulikuwa na nia thabiti ya kushika Dola mwaka huu, haya yalipaswa kufanyika mapema:-

1) Kuimarisha jumuia za makundi muhimu katika jamii km Vijana, Wazazi, Wanawake, Walemavu na Wazee, kuanzia ngazi za chini (Vitongoji na Mitaa).

2) Kuweka Utaratibu wa Ushirikiano kuanzia pia ngazi za chini.

3) Kuichambua Sera za CCM, chama Dola, zilizoanishwa kwenye Ilani yake ya Uchaguzi, 2015 ili kubaini mapungufu yake na mapungufu ya Serikali katika kutekeleza Ilani hiyo.

5) Wagombea wa Urais waliopitishwa wasibebe umaarufu wao kwenye majukwaa ya kampeni ila wajikite kwenye pendezo na. (4) kwa kuelezea Sera mbadala na utekelezaji wake (siyo ahadi hewa) kwa kuwa vyama vya upinzani havina mifano ya utekelezaji.

Izingatiwe kuwa katika kipindi cha miaka 5 ya Serikali inayongozwa na Magufuli, yako mambo mengi ya kimaendeleo yametekelezwa (pamoja na changamoto mbalimbali), ambayo yatatumika kuomba kura ili kushughulikia mapungufu yaliyojitokeza.

Wahenga walinena Mkono mtupu haulambwi.
 
Hakutakuwa na kumwaga damu atakabidhi kwa amani

Jr[emoji769]
 
 
Wasichoelewa watu ni kwamba Magufuli na CCM yake wakati umewakataa!

Yaani majira hayakubaliani nao ingawa wanalazimisha!

Japo watu wanapuuza lakini CCM inaanguka mwaka huu... na Magufuli hana upepo kabisa!
Magufuli atabebwa na kinachobezwa na wapinzani kuwa ni "maendeleo ya vitu" wakati wagombea wa upinzani wanategemea bwembwe zao majukwaani kwa kuilaumu Serikali, kwa matusi na madai yasiyomwongezea mpiga kura ugali mezani km Tume huru ya Uchaguzi, Demokrasia, utekaji watu nk.

Hakika Mtanzania aliyekuwa:

√ anatumia kibatari kwa mwangaza sasa anatumia mwanga wa umeme;

√ vijana wake walikuwa wakikimbilia mijini kutafuta ajira sasa kuna nishati ya umeme kufanya shughuli zake za kimaendeleo;

√ mja mzito aliyekuwa anasafiri umbali mrefu kufuata huduma ya afya, sasa iko umbali wa wastani;

√ aliyeshindwa kumwandikisha mtoto shule kwa sababu ya ada, sasa ni elimu bure;

√ aliyeshindwa kwenda kwenye shughuli zake za kijamii na maendeleo kwa sababu ya miundo mbinu mibovu ya usafiri, sasa hilo ni hadithi, nk,

Hakika hawa WaTz hawataacha kumpigia kura Magufuli.
 
Reactions: nao
Ukweli ni kwamba JPM kwa uchaguzi huu atapata kura nyingi zaidi ya uchaguzi uliyopita.

Huko ni kujifariji tu......Ukweli na Uhalisia ni kwamba Magufuli atakuwa na Hali mbaya Sana!!!
Mpaka Sasa hapati Usingizi....sanasana tegemeo lake ni TUME YAKE YA UCHAGUZI ISIYO HURU😎
 
Sio rahisi kihivyo.
 
Si wakati ule wapinzani walipoitisha mikutano wakakamatwa kuwa hawana vibali au mim nasahau
Hakukua na mikutano kwenye kuandikisha na kuboresha daftari la wapiga kura
 

Hizi ni propaganda tu zisizo na Uhalisia wowote kwa maisha ya Mtanzania!

1. Hivi unajua Kuna Shule za msingi na Sekondari Zina Mwalimu mmoja au 2 tu?

2. Hivi unajua Kama Kuna Shule hazina Samani na Vitabu vya kiada, hazina matundu ya vyoo, hazina vyumba vya madarasa, hazina umeme n.k.

3. Hivi unajua kuwa Kuna Zahanati, hospitali za mikoa na Rifaa hazina Madaktari na Wauguzi wa kutosha?

4. Hivi unajua kuna Watanzania wamemaliza elimu ya vyuo viwango vya Astashahada, Stashada na hawajapata Ajira kwa miaka 5 iliyopita?

5. Hivi unajua kuna Watanzania kwa mamilioni hawajawahi kupanda ndege za Bombadier, Dreamliner wala Airbus alizonunua Jiwe?

6. Hivi unajua kuna Watz walalahoi Wamestaafu miaka zaidi ya 2 iliyopita na hawajapata stahili/malipo yao ya Uzeeni/Pensheni?

7.n.k. na n.k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…