GE2025 Lissu: Nikitoka (gerezani) ni mchakamchaka, nikitoka ni barabarani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hapa kuna ukweli tushindane kwa hoja ndo siasa
 
Tundu aweza kuwa mwanasheria mzuri lakini hakujaaliwa karama na busara ya kuongoza watu.

Miezi 4 toka ashinde uchaguzi chama kina hali mbaya, yeye mwenyewe yuko ndani. Kama atatoka naona atakuwa kama akina Lipumba na CUF au Mbatia na NCCR.
 
Jina lipo tayari. That much I have no doubt.
Ulisha hitimisha, lakini naona ni kama hujui kitu chochote?
 
Tundu aweza kuwa mwanasheria mzuri lakini hakujaaliwa karama na busara ya kuongoza watu.

Miezi 4 toka ashinde uchaguzi chama kina hali mbaya, yeye mwenyewe yuko ndani. Kama atatoka naona atakuwa kama akina Lipumba na CUF au Mbatia na NCCR.
Sasa angalia unavyo jishusha hadhi mwenyewe ha a. kwa kuandika mambo ambayo hata wewe mwenyewe unaelewa siyo sahihi.
Hiyo miezi minne ulitaka awe amefanya mambo gani, ili umwone kuwa kiongozi mwenye uwezo? Miezi minne ya kupambana na hila zenu - Samia na GENGE lake lote?
Hiyo 'karama' ya uongozi anayo Samia au hata Kikwete viongozi wenu wa GENGE linalohujumu nchi hii? Hizo 'standard' za "karama" ni zenu mnaopenda kupoteza na kuuwa watu ili mbaki madarakani.
 
Wao (Tundu & Heche) wamepewa madaraka tarehe 21/ 01/2025. Ndani ya miezi 4 yafuatayo yametokea:-
1. Mwenyekiti Tundu amepanga uasi ili kuzuia uchaguzi wa kikatiba wa Oktoba
2. Mwenyekiti Tundu ameshtakiwa kwa kosa la uhaini na yuko rumande Ukonga
3. MAKAMU wake Heche amefukuza viongozi wa CDM kama 55 kisa hawaungi mkono kususia uchaguzi
4. Makamu Heche amekataa kusaini kanuni za maadili za INEC. Hivyo chama kiko nje ya uchaguzi automatically
5. Msajili kasimamisha shughuli za CDM kwa sababu kuna kesi ya kugombea mali za CHADEMA

Kimsingi CCM itatawala milele kama akina Tundu, Heche na Godbless Lema ndiyo viongozi wenyewe wa upinzani
 
Kimsingi CCM itatawala milele kama akina Tundu, Heche na Godbless Lema ndiyo viongozi wenyewe wa upinzani
Unayoizungumzia hapa siyo CCM. CCM mmekwisha iua, mnachotumia ni jina lake tu basi na cha kushangaza bado mnafikiri waTanzania hawajui ulaghai huo!

Sasa kama viongozi hao mnajuwa hawawezi uongozi, ni kipi hasa kinachowatia kiwewe kiasi hiki mlicho nacho sasa!

Angalia maandishi yako tu hapa; kimsingi unachosisitiza ni kukiuka HAKI; kufanya maovu ili mradi Samia na GENGE lenu liendelee kubaki madarakani. Huo ndio uongozi wa karama?

Samia na GENGE wanaogopa kitu gani wakati viongozi wa upinzani hawana uwezo kama unavyo eleza wewe?
Mbona akina Lipumba/Cheyo na hao wengine hawasumbuliwi; kwani wao siyo wa upinzani?
Unajiondoa akili maksudi, ili tu uonekane unachangia JF kutetea uongozi ovu?
 
Huko barabarani atakua peke yake, vijana wa hii nchi ni wapuuzi sana. Anapoteza muda na nguvu zake bure tu
 
Marehemu Magufuli alimshindwa iwe huyu Mama wa Kizimkazi ambaye kusoma sentesi moja kwa ufasaha kunamshinda.

Hakika Lissu ndiye yule Mkombozi wa Tanganyika.
 
Hebu niulize kwa faida ya wengi.
Kwani vyuo wanavyokwenda mawakili wa serikali ni tofauti na vyuo wanavyokwenda mawakili wa kujitegemea?
Nauliza kwasababu naona Hawa wa utetezi kina Lissu, Kibatala, Mzee Mpoki, Nshalla Wana akili nyingi na maswali ya mitego kuliko wale wa upande wa mashtaka?
Okay, Kama wote wanasomea Sheria sehemu moja, serikali inatumia vigezo Gani kuajiri mawakili.
Imagine Kibakala angekua upande wa serikali Kuna mhalifu angechomoka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…