Uchaguzi 2020 Lissu nimekusikiliza mwanzo mwisho ila haujasema kwanini tukuchague wewe na sio Magufuli

Uchaguzi 2020 Lissu nimekusikiliza mwanzo mwisho ila haujasema kwanini tukuchague wewe na sio Magufuli

Mimi nilitegemea leo ndio siku ya kuzindua kampeni na sera,!

Hebu chadema twambieni kulikuwa na nini leo Mbagala?
Ma UVCCM mnajifanyaga mna akili lakini ukweli ni kwamba kichwani mwenu mmebebelea makamasi badala ya ubongo. Ina maana hukumsikia Lissu akisema kwa nini hatatoa hotuba yake ya uzinduzi kama alivyokuwa ameandaa?
 
Wala msiisingizie NEC,hao walioenguliwa wamekosea kujaza form. Mnasingiziaje NEC hapa ?

Wewe mwanamnke wakati mwingine uwe unatumia akili. Kwa hiyo zaidi ya 90% ya wagombea wa ACT Zanzibar wamekosea kujaza fomu na 100% ya wagombea wa CCM wamepatia?

Uwe unaona aibu wakati mwingine kutetea ujinga!

Watu wanaporwa fomu chini ya mitutu ya bunduki, wengine wakurugenzi wanatoa fomu za uteuzi kwa wagombea feki na wengine wanashindwa kurudisha fomu kwa sababu wakurugenzi wamefunga ofisi achilia mbali wale kuenguliwa kwa mapingamizi feki halafu unasema eti hawajui kujaza fomu?—Acha matusi wewe!
 
Wewe mleta mada ni "kiazi". Hukufuatilia kilichosemwa, sasaivi unatoa lawama.

Waafrika bhana!


JESUS IS LORD!!!
 
Lissu nimekusikiliza mwanzo mwisho ila haujasema kwanini tukuchague wewe na sio Magufulli...Ninakuomba umwage sera na siyo historia ya yaliyotokea.
Kama ni kweli umemsikiliza mwanzo mwisho kama unavyodai, huu utumbo ulioandika unautoa wapi? Victoire kumbe na wewe unaweza kuwa mpuuzi kama walivyo asilimia 99% ya vijana wa Lumumba. Yaani kwa malipo yale kiduchu yanayotolewa unakubali nawe kutumika kipuuzi namna hii...kweli umdhaniye ndiye, siye.
 
Hakuna kitu humo zaidi ya mihemko
Uchaguzi wa mwaka huu utakua mwepesi sana
Na tunaona mwepesi sana kwani Tiss ndio maafisa wa Tume ya Uchaguzi hapa Zanzibar, uvamizi unaendelea na waislamu nani masheikh wako magerezani kwa kesi zani kubambikiziwa
 
Presidential Material inategemea na mtu anayeongea. Kwa sisi wengine tulivyoshuhudia hii miaka mitano iliyopita namuona Magufuli kama SIO Presidential Material kabisa.

Na mimi binafsi siwezi kabisa kumpigia kura mtu ambaye aheshimu utawala wa sheria kwa kuamua kujibinafsishia mamlaka ya taasisi zote kwake.

Sasa nimpe kura kwa lipi, kama ni miundombinu, hilo ni jukumu la kila serikali hata wakoloni walitengeneza miundombinu.

Lakini cha muhimu zaidi kwangu ni utawala wa sheria pamoja na kushindwa kuinua uchumi wa nchi na kubaki kuchakachua takwimu za kwenye makaratasi. Bure kabisa.
 
Mbona unaongea/kuandika kikike?
Unaushahidi wa Raisi kutoa amri au ushauri huo???
1. Hiwa najibu kulingana na hoja iliyopo
2. Ndyiyo, sababu presidential material lazima angekemea hayo.
3. Ndiyo sababu alitoa amri hiyo pale aliposema ole wake mkurugenzi atakayetangaza mpinzani kushinda.
Je, una swali lingine?
 
Apo Sawa.
Naona Pemba wameengua wagombea wite wa ACT.NEK imetusaidia kupata ushindi wa mezani.# NA BADO
Wakate rufaa kama wanaona wameonewa. Tatizo wapemba wengi shule zero. Chama kilitakiwa kiwaelekeze jinsi ya kujaza form.One mistake one goal.
 
Hujamsikiliza wewe, mbona kasema hotuba yenye kurasa 24 aliyoiandaa hataisoma leo?

Watu wengine hata akili kumkichwa hakuna.
Kuna watu wanajiona wajuaji wakati ni vilaza, mtu kasema ana hotuba hatoisoma kwa ajili ya upuuzi unaendelea mwingine anahoji hoja ccm wamechokwa sana.
 
Kwa sera za Lissu, na anapotoa historia hizo magufuli atashinda asubuhi na lissu hata 20% hatopata
 
Wewe mwanamnke wakati mwingine uwe unatumia akili. Kwa hiyo zaidi ya 90% ya wagombea wa ACT Zanzibar wamekosea kujaza fomu na 100% ya wagombea wa CCM wamepatia?

Uwe unaona aibu wakati mwingine kutetea ujinga!

Watu wanaporwa fomu chini ya mitutu ya bunduki, wengine wakurugenzi wanatoa fomu za uteuzi kwa wagombea feki na wengine wanashindwa kurudisha fomu kwa sababu wakurugenzi wamefunga ofisi achilia mbali wale kuenguliwa kwa mapingamizi feki halafu unasema eti hawajui kujaza fomu?—Acha matusi wewe!
Ndo wakate rufaa sasa. Haki ya mtu haipotei.
 
Siku kadhaa zilizopita Niliposema Lissu is not a " Presidential material", kwa wengi sikueleweka. Leo nadhani wengi watakuwa wameanza kunielewa!

Yaani badala ya kujenga hoja kwa wananchi wamchague, " Ni yeye" anaifitinisha Tanzania dhidi ya Jumuiya ya kimataifa. Tanzania ya watanzania tena ya wananchi wenye uwezo wa kumuweka madarakani.

Yaani anataka Jumuiya ya kimataifa ndiyo imuweke madarakani hapa nchini badala ya sisi watanzania ndiyo tumuweke madarakani. Sasa Lissu akisha wekwa madarakani na jumuiya hiyo ya Ulimwengu, atailipa nini!?

Siyo ndiyo, mwanzo wa Lissu kutuuza watanzania kwa mafungu...!!! Kwa hili, leo amepoteza nafasi adhimu ya kuwashawishi watanzania kwa hoja ili wamuweke madarakani.
Wanafitinishwa au wanajifitinisha?
 
Kuna watu wanajiona wajuaji wakati ni vilaza, mtu kasema ana hotuba hatoisoma kwa ajili ya upuuzi unaendelea mwingine anahoji hoja ccm wamechokwa sana.
Nyie ndo vilaza. Hivi mtu ana hotuba na asiisome Kweli ??Hebu tumieni akili basi. Hakuwa na hotuba yule. Siku ya jana ilikuwa muhimu sana kwa kunadi sera zao.
 
Lissu bwana tunajua wewe ulipigwa risasi, asante Mungu umepona.

Sasa tunakuomba usitumie muda wako wa kampeini kuongelea tu yaliyokupata miaka mitatu iliyopita.

Tuambie utafanya nini endapo utakuwa Rais, tuambie kwa nini wewe na si Magufuli tena.

Binafsi leo nilitegemea kusikia madini ni nini utaifanyia Tanzania/ Watanzania ambapo Magufuli kafail.

Ninakuomba umwage sera na siyo historia ya yaliyotokea.
Wewe inaonekana ni aina ya wanawake ambao hata kama mumeo akipata matatizo ( kama unae ) huwa unamshurutisha, kuwa unajua alipata matatizo ila unachotaka ni pesa
 
Mm nafikiri hujasikia vizuri, ni kwamba Leo ilani haijazinduliwa sababu ya kuweka sawa suala la wagombea walioenguliwa
Kiswahili ni kirahisi mno
Basi wametumia nafasi hiyo vibaya; ni afadhali wangeshughulikia hayo mapingamizi kwanza ndipo wazindua kampeini. Yeye Lissu alikuwa wa kwanza kutoa mapingamizi, kwa hiyo anakubali uhalali wa mapingamizi. Kwa vile ya kwake hayakufanikiwa haina maana kuwa ya wengine yasifanikiwe pia.
 
Wewe inaonekana ni aina ya wanawake ambao hata kama mumeo akipata matatizo ( kama unae ) huwa unamshurutisha, kuwa unajua alipata matatizo ila unachotaka ni pesa
Kama matatizo yalishaisha,la yupo kwenye stuation nzuri why asinipe pesa ?Tunaishi muda uliopo and hoping for the future. The past has already gone,why living the past ?While we know what has passed has passed.
 
Back
Top Bottom