Kuhusu malipo ya Tundu Lissu kama posho na stahiki zake mbalimbali kwa mujibu wa Spika Ndugai, kuna maswali yanahitaji majibu;
1. Ndugai anasema Tundu keshalipwa
- Tshs. 200,000,000 (za nini?Haijulikani...!!)
- Tshs. 360,000,000 (za mini? Haijulikani...!!)
- Tshs. 500,000,000 (za mini? Haijulikani...!!
...............................................................
JUMLA Tshs. 1,060,000,000 (billion moja na sitini milioni..!!!)
................................................................
2. Je, Spika Ndugai anaweza kutoa uthibitisho Wa malipo haya kutoka Bunge kwenda kwa Tundu Lissu ili kukata mzizi Wa fitina..??
3. Kama Tundu Lissu amelipwa pesa zote hizi na serikali kupitia Bunge, iweje bado analalamika kudhulumiwa mafao na haki yake ya kulipiwa gharama za matibabu..??
4. Je Spika Ndugai anaweza kutoa mchanganuo wa pesa zote alizolipwa Tundu Lissu ni kwa ajili ya nini?
NB:
Mimi naamini mambo mawili juu ya sakata hili;
MOSI: fedha za mafao, gharama za matibabu, posho na mishahara ya Tundu Lissu kuanzia Septemba, 2017 hadi ukomo wa bunge la 11 zimelipwa lakini hazijaenda kwa muhusika..!
PILI; Spika Ndugai anaweza kuwa sahihi kwa sababu yeye (inawezekana) anapokea taarifa tu za utekelezaji na kisha kuzitetea tu bila kujiridhisha kuwa zina ukweli. Hapa tunaweza kusema (labda) anacheza ngoma ya watu wengine...!
TATU; Tundu Lissu, binafsi, naamini hawezi kudai pesa mara mbili huku akitambua kuwa ameshalipwa..!
NNE; Kama Spika anadai Lissu alishalipwa Tshs. bilini 1.06 halafu wakati huohuo muhusika anasema hajapokea hata senti, hapa inakuwa na maana gani hasa..?
Je, kuna uwezekano kuna ufisadi wa fedha bungeni kwa kutumia kivuli cha ugonjwa na kuvuliwa kwa ubunge wa Tundu Lissu...?
Uchunguzi ufanyike tu...