Kinachokuuma ni nini?Kwani huyo lisu anajiona nani hasa hadi ampangie vya kufanyiwa ndo arudi? kwani kuna mtu kamuita au alivokaa huko miaka yote jua halikuwaka TZ au mvua haikunyesha? Ikiwezekana kae huko na afie huko hakuna amtakae. Waswahili wanakwambia ukitaka kudeka hakikisha yupo wa kukudekeza, sasa asilazimishe kudekezwa. Akitaka arudi apambane na hali yake kama hatak abaki huko, mxiuuuu
Bado hali sio shwari.Mimi namshauri Lisu arejee tu, sioni hayo madai yake yakitekelezwa. Ila nina uhakika hawezi kufanyiwa madhila yoyote, kwakuwa aliyekuwa anaagiza afanyiwe ule udhalimu alikuwa ni Magufuli kutokana na kiburi cha madaraka, na kutokutaka kukosolewa. Hayo madai yake mengine aje atayafuatilia akiwa hapa kwa yale yanayowezekana.
Na kweli, "asiludie" tena kukuuliza uliza maswali[emoji23][emoji23]Umri huu nilionao niludi shule nikafanye nini changamoto nilionayo ya kuwasomesha wadogo zako kwangu ni shule tosha kama umenielewa na ujumbe wangu umefika hizo tofauti za r na l si kitu kwangu
Bado hali sio shwari.
Kumbuka watu wa meko bado wana ile mentality ya unyama na uuaji.
Itachukua muda kidogo hawa wauaji kubadiki misimamo yao.
Bado wanatembea kwenye kivuli cha meko na ukatili wake.
Angalia tu a hata baadhi ya wana JF kwenye hii thread.
Bado wana ukatili na roho mbaya ambayo walimezeshwa na meko na kina heri wa uvccm.
Kwa hio bafo haki si shwari
Mama kadhika hatamu, yeye arudi tu kama ni wa kuru hayo masheriti anampa nani?Mna haja na nan?
Meko?
Usipoteze muda wako kumuamini ndungai.Kuhusu malipo ya Tundu Lissu kama posho na stahiki zake mbalimbali kwa mujibu wa Spika Ndugai, kuna maswali yanahitaji majibu;
1. Ndugai anasema Tundu keshalipwa
- Tshs. 200,000,000 (za nini?Haijulikani...!!)
...............................................................
- Tshs. 360,000,000 (za mini? Haijulikani...!!)
- Tshs. 500,000,000 (za mini? Haijulikani...!!
JUMLA Tshs. 1,060,000,000 (billion moja na sitini milioni..!!!)
................................................................
2. Je, Spika Ndugai anaweza kutoa uthibitisho Wa malipo haya kutoka Bunge kwenda kwa Tundu Lissu ili kukata mzizi Wa fitina..??
3. Kama Tundu Lissu amelipwa pesa zote hizi na serikali kupitia Bunge, iweje bado analalamika kudhulumiwa mafao na haki yake ya kulipiwa gharama za matibabu..??
4. Je Spika Ndugai anaweza kutoa mchanganuo wa pesa zote alizolipwa Tundu Lissu ni kwa ajili ya nini?
NB:
Mimi naamini mambo mawili juu ya sakata hili;
MOSI: fedha za mafao, gharama za matibabu, posho na mishahara ya Tundu Lissu kuanzia Septemba, 2017 hadi ukomo wa bunge la 11 zimelipwa lakini hazijaenda kwa muhusika..!
PILI; Spika Ndugai anaweza kuwa sahihi kwa sababu yeye (inawezekana) anapokea taarifa tu za utekelezaji na kisha kuzitetea tu bila kujiridhisha kuwa zina ukweli. Hapa tunaweza kusema (labda) anacheza ngoma ya watu wengine...!
TATU; Tundu Lissu, binafsi, naamini hawezi kudai pesa mara mbili huku akitambua kuwa ameshalipwa..!
NNE; Kama Spika anadai Lissu alishalipwa Tshs. bilini 1.06 halafu wakati huohuo muhusika anasema hajapokea hata senti, hapa inakuwa na maana gani hasa..?
Je, kuna uwezekano kuna ufisadi wa fedha bungeni kwa kutumia kivuli cha ugonjwa na kuvuliwa kwa ubunge wa Tundu Lissu...?
Uchunguzi ufanyike tu...
Mkuu; angekuwa hajawaagiza wale wote waliofanya ule unyama wangekamatwa fasta.Mkuu ule unyama wote ulikuwa unaagizwa na Magufuli. Hao wanyama ni kweli bado wapo, ila nani wa kuwapa maagizo? Hata hivyo sipingi angalizo lako.
Sijaelewa hi; kwamba Lissu akiwa hospitalini alikua anawekewa pesa za mafuta za kwenda jimboni kwake? Hapa wa kulaumiwa ni nani? Bunge au Lissu??? Somebody to help me pleaseHata hivyo, alisema kama angeendelea, wangekwenda mbali zaidi na kuhoji jinsi alivyotumia fedha za wananchi, mishahara ya dereva wake na mafuta ya kumpeleka jimboni wakati akijua anazitumia isivyo halali kwa sababu yupo nje ya nchi, jambo ambalo lingemletea shida kwa kutakiwa kuzirudisha.
Wewe unamwamini lissu kwa asilimia ngapi? mimi ni kwa 50% namndugai 50% sasa ilikutoa utata ARUDI TZ WAKAE PAMOJA KILA MTU ASIBITISHE ALIVYOTOA ALIMPA NANI NA LISSU AONYESHE KAMA HAJAPOKEA KWELI mhuniyule haaminikiTATU; Tundu Lissu, binafsi, naamini hawezi kudai pesa mara mbili huku akitambua kuwa ameshalipwa..!
Bwashee usisahau kuweka hapo ka kvant kadogo.Kuna wakati ni lazima unywe mbege kisado kimoja ili uwaelewe hawa Chadema!